Ndiyo unaweza kuona vipi wa Tanzania tuna matatizo ya kufahamu uzalendo na hiyo ni sababu tosha ya kushindwa kuendelea katika dunia hii, kwani haiwezi kuingia akilini eti Yanga ambayo ni timu yetu inawawakilisha wa tanzania, bado kuna wajinga wajinga eti wanajiita Simba eti wao hawawezi kuishangilia Yanga kwasababu ya utani ya jadi, jadi jadi ni aina mojawapo ya upumbavu tu, na nina maana hiyo hiyo kwa upande simba kama itakuwa hivyo, inabidi tufikie kipindi kuwa wamoja tunapowakilisha nchi yetu. Wakati nawakilisha haya mimi ni Simba tangu nilipojua kuna mpira wa miguu na timu za mpira katika dunia hii, lakini leo nitavaa jezi ya kijani kuiwakilisha Tanzania. Nione kama nitabadilika rangi.