Sio lengu langu kuunga mkono hatua ya mashabiki wa simba kuishangilia Zamalek, lakini pia mashabiki wa yanga hawana haki wala mamlaka ya kuwashambulia mashabiki wa simba, wengi wetu tulikuwepo uwanjani mkwaka jana wakati simba inacheza na TP Mazembe na kila mtu aliona ni jinsi gani yanga waliishangilia TP mazembe na hakuna shabiki wa simba aliyerusha ngumi, huu ugonjwa wa kuzishangilia timu pinzani haujaanza jana au juzi kwa hiyo sioni sababu za mashabiki kupigana, kuna mahali mpira wa tanzania ulifanya makosa na ndio umezaa mambo yote haya, lakini kumbukeni mpira sio vita ni burudani.