Uwanja wa Taifa ni mchafu sana

Uwanja wa Taifa ni mchafu sana

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,409
Reaction score
13,262
Sisi wapenzi wa mpira tunapoenda kuangalia mpira Uwanja wowote ule kwa malipo maana yake sisi ni wateja inabidi tuheshimiwe kama wafalme kama kauli mbiu inavyosema kuwa mteja ni mfalme.

Nikizungumzia uwanja wa Taifa wa Mkapa ambao ndio uwanja mkubwa na bora kuliko vyote nchini kwakweli huduma zake ni duni sana na ni uwanja mchafu sana kuanzia vyooni hadi kwenye viti. Yaani unaweza kwenda uwanja wa taifa ukiwa msafi ukarudi mchafu kabisa na siyo mahali kwa kuvaa suti kule kama wenzetu Ulaya. Unafika unakuta viti ni vichafu sana yaani hata kufuta vumbi hawawezi wakati wanapokea pesa nyingi katika kila mechi inayofanyika pale. Hizo pesa wanapeleka wapi kama hata usafi hawawezi?

Unaweza kwenda Taifa ukarudi na magonjwa ya kuambukiza kutokana na vyoo kuwa vichafu sana na mfumo wa maji mbovu kabisa bomba nyingi zimenyofolewa na hakuna anayejali.

Ushauri wangu ni kuwa Uwanja wa taifa ubinafsishe kazi ya usafi au hata uwe inafanywa kwa ajira ya muda maalumu wa siku ya mechi tu. Iwepo kampuni ambayo itafanya usafi nan kukarabati bomba na mifumo ya maji kabla ya mechi lakini pia baada ya mapumaziko wakati washabiki wamerudi uwanjani wafanye usafi na kurekebisha pipes kama zimenyofoka na pia wafanye hivyo baada ya mechi wakati washabiki wameondoka mpaka tena mechi ijayo.

Kwa upande wa ndani wanaweza kuitisha hata vijana 200 au 300 kwa siku ya mechi wafute viti vyote kwa ujita wa 10000 kila mmoja na ofa ya kuangalia mpira ili washabiki wakiingia wakute viti visafi ili wasichafuke nguo zao.

Vile vile katika mechi ambazo hazina mashabiki wengi haina haja ya watu kutawanyika sana na kutumia viti ovyo au kuharibu. Wanaweza kuamua kuwa washabiki wakae viti vya orange au mwisho vile vya kati.

Naomba wahusika wazingatie usafi jamani wengine wanaaleji ya vumbi wakiingia wanakuta mavumbi kama yote. Haifai
 
Achana na vitu vidogo hivyo, tafuta katiba mpya itamaliza upuuzi wote huo
 
Unaweza kuwa unawalaumu bure kumbe kwenye bajeti hawamo hela yote inaenda serikalini
 
Hilo suala la uchafu ni kero kubwa, na ndio maana miundombinu inachakaa haraka.

Hiyo siku nilivaa raba zangu nyeupe kilichonikuta basi tu.
Vumbi ndio usiseme, unafika unaanza kufanya usafi kwanza!
 
Kwa walioenda kipindi vha ile mechi ya ufunguzi wa African Football League AFL hali ilikua hovyo pia?
 
Hata picha...!?

Haya mambo ya mtu mmoja kuona kitu halafu akataka kila mtu atakuwa kaona, ni mambo ya zamani saaana enzi za simu za kidole juu
 
Tanzania karibu kila taasisi, almradi pesa zinaingia watu hawajali suala la ubunifu, unadhifu na uboreshaji.

Tunaweza kuwalaumu wahusika bure wakati ndipo uwezo wao wa akili umeishia.

Taifa letu linahitaji mfumuko wa akili.
 
Nenda pale wizara ya ardhi mjini kati kabisa pembeni ya ikulu halafu cheki ile hygiene ndio utaelewa ni namna gani tuna shida, na kama vitu vidogo kabisa vinatushinda tutawezaje kuwahudimia watanzania kwamafanikio kama basic things zinashindikana
 
Wakulaumiwa ni nyinyi mnaohingia na mafuko ya mabajia na bisi ,aafu mnatupa chini ya viti ,wakati kuna madust bin kila kona.
mambo mingine ni ya kujitafutia wenyewe,usingoje kushitakiwa kwa kutupa taka hovyohovyo tumia wajibu wako.
 
Back
Top Bottom