Uwanja wa Taifa: Simba SC 5-0 Mbao | Ligi Kuu Soka Tanzania Bara | 26/02/18

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Leo ni kiputwe cha ligi kuu soka Tanzania Bara ambapo wekundu wa msimbazi Simba inawakaribisha Mbao FC kutoka jijini Mwanza.

Mbao ikiwa kama timu iliyoleta changamoto kwa Timu kubwa za Kariako yaani Simba na Yanga ambapo yanga Tayari kashachezea msimu huu kwa goli 2.

Kwa upande wa Simba, matokeo ya mzunguko wa kwanza ilikuwa 2-2 wakati mbao ikiwa nyumbani. Leo Simba atakuwa nyumbani uwanja wa Taifa, Dar.

Swali linalobakiwa ni hili; Je, Mnyama atafanikiwa kuzichanachana Mbao?


Kikosi cha Simba


Kikosi cha Mbao




0' Mechi inaanza

01' Simba wanaanza kwa kupigiana

02' Mbao nao wanapanga mashambulizi kwenye lango la Simba

04' Habibu Kyombo anafanya shambulizi kuelekea lango la simba ila anadhibitiwa na James Kotei.

06' Mbao wanafanya shambulizi lingine linadhibitiwa.

07'Mbao wanaonekana kujipanga vizuri japo Simba wanajitahidi kujipenyeza kupitia pembeni.

08' Simba wanafanya shambulizi kwenye lango la mbao na wanapata faul, faul imepigwa ila haijazaa matunda.

10'Simba wanapiga kros kupitia kwa Gyan, na Okwi anaikosakosa.

11'Kipa wa mbao anaonyeshwa kadi ya njano

12'Mbao wanafanya counter attack ila wanadhibitiwa.

14'Ndemla anapiga shuti golini ila kipa anaidaka

15'Mbao wanapigiana vizuri wenyewe kwa wenyewe

16'Mpira unapigwa kuelekea simba

17'Faul inapigwa kuelekea simba ni karibu na 18, simba wanadhibiti

20' Free kick kuelekea lango la mbao, ni nje kidogo ya 18. Golikipa anadaka

21'Okwi anafanya shambulizi lakini anadhibitiwa

24' Mbao wanafanya shambulizi hatari golini mwa simba ila mabeki wa simba wanasimama vizuri kudhibiti madhara
Kona imepigwa kwenye lango la simba inapigwa kichwa na kutoka nje.

26' Simba wanapanga tena mashambulizi kwenda lango la Mbao.

28' Mbao wanafika langoni mwa Simba mara nyingi zaidi, wanaonekana kuwa na kasi sana.

29' Mpira sasa ni kushambuliana kwa zamu

31' Anatoka Ndemla anaingia Mzamiri Yasin.

37' Goooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo

Simba inapata goli la kuongoza kupitia kwa Shiza Ramadhani Kichuya, ni baada ya kupokea pasi kutoka kwa Emmanuel Anorld Okwi na kuutundika wavuni.

41'Emmanuel Okwi anavutwa na beki wa Mbao David Mwasa na imeamriwa kupigwa penati na David mwasa anaonyeshwa kadi ya njano
Penati inapigwa na Okwi mwenyewe
41'Gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo

45'Mbao wanafanya shambulizi kwenye lango la Simba kupitia kwa Habibu Kyombo anatoa pasi lakini inatoka nje

Mpira ni Mapumziko

Kipindi cha pili kinaanza

45'Mbao wanajitahidi kulishambulia lango la Simba ila jitihada zinashindwa kuzaa matunda.

46' Okwi anawekwa chini, faul inapigwa

48' Shomari Kapombe yuko chini na anagangwagangwa na dkt. wa Simba

50' Simba wanapigiana vizuri huku wakipanga mashambulizi kuelekea Mbao

51' Mzamiru anapata nafasi nzuri ila anapiga shuti hafifu na kipa anaidaka

James Msuva, mdogo wake Simoni Hapigodi Msuva anatoka

52' Faul inapigwa na almanusra afunge japo kipa anaiokoa

54' Faul inapigwa kuelekea Simba, kipa wa Simba Manula anaidaka

55' Emmanuel Mvulukule wa Mbao anaoneshwa kadi ya njano

57' Anatoka Ibrahimu Njohole anaingia Said Said kwa upande wa mbao

59' Nicolaus Gyan anafanya shambuuliz matata ndani ya lango la Mbao, lakini anadhibitiwa na Yusuph Ndikumana.

62'Mbao wanafanya shambulizi kupitia kwa Habibu Kyombo lakini anaitoa nje.

63' Free kick kuelekea lango la Simba, inakuwa ni kona

65'Otecha anapiga shuti kali lakini halijalenga vizuri goli

66' Habib Kyombo anaachia shuti moja golini lakini inatoka nje

67'Simba wanaanzisha mashambulizi upya, wanapata kona inapigwa na Kichuya ila haijakuwa na madhara.

69' Gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
Emmanuel Okwi anawanyanyua mashabiki wa Simba kwa kutundika goli la tatu baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa James Kotei na kutundika kimiyani.

73' Kichuya anafanya shambulizi moja hatari lakini inakosekana wa kumalizia

75' Kichuya anapiga kona ila haijazaa matunda.

77'Okwi anatoka, anaingia Laudit Mvugo

78'Gyan anafanya shambulizi moja lakini linadhibitiwa

80'Gyan anapiga kros nzuri, Mzamiru anajitahidi kuimalizia ila inatoka nje

81' Erasto Nyoni anapiga faul ambayo inamparaza beki wa mbao na kuingia moja kwa moja golini

82'Gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo

84' Nahodha wa mbao Yusuph Ndikumana anaonyeshwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa na kadi mbili za njano

86'Goooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
Nicolaus Gyan anafunga goli la tano baada ya kupokea pasi toka kwa Asante Kwasi.

88' Mbao wanafanya shambulizi lakini haijazaa matunda

90' Simba wanapiga kona

Na mpira umekwisha
 
Niko njian naenda kumpa support mnyama
 
Mechi itaanza soon, wachezaji washatia timu uwanjani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…