Nimepita leo asubuhi, jukwaa la kijani limeshaporomoshwa chini, na tingatinga linaendelea kubomoa!
Nakumbuka uwanja huu uliachwa kwa nafasi yake katika historia ya UHURU wa Tanganyika, ndio maana Wachina wakajenga uwanja mpya pembeni.
Huyu aliyeamua ubomolewe; hata kama ni Magufuli, atuambie ametumia sheria ya mwaka gani?
National Stadium (Dar Es Salaam)
Mkuu umepost bila kuleta data za kutosha na "wanahistoria" wananchanganyikiwa kwa kuto kuwa na background ya kutosha.
Lakini hizi lawama ni za bure, si wengi wananelewa kuwa katika uhai wake ,kiwanja hiki cha uhuru kimepitia maboresho mengi sana.
"Green Stand" haikuwa hivyo zamani , ilikuwa ya steel structure ambayo ilikuwa hatari sana na kuna wakati ilipiromoka kwa uzito wa watazamaji.
Lango kuu la kutokea Indoor stadium miaka iliyopta halikuwepo na lilijengwa katika maadhimisho ya kitaifa zaidi ya miaka 30 iliyopita.
Hata hiyo tartan surface ya riadha imewekwa si miaka mingi iliyopita.
Zaidi ya yote si wengi wanaofahamu kuwa mahala hapa kilikuwa kiwanja cha ndege wakati wa vita kuu ya pili na Indoor Stadium ilikuwa hangar la ndege.Na mimi nikiwa mdogo nimechezea ndege zilizoharibika nyuma ya In Stad.
History is only relative
Hata hivyo Mkapa atakumbukwa kwa hii stadium mpya na ya kisasa, a stadium of International standards, lakini in 100 years itakuwa history.
Benjamin Mkapa National Stadium