Uwanja wa Taifa | Vodacom Premier League: Simba SC 3 - 0 Mwadui FC

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001

====

BAADA ya kutoka sare katika mchezo wao uliopita dhidi ya Ruvu Shooting, hatimaye kikosi cha Simba kimeibuka na ushindi wao wa kwanza leo dhidi ya Mwadui, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam tangu kurejea kwa Ligi Kuu Bara, Juni 13.

Ligi Kuu Tanzania Bara ilisitishwa Machi 17 kutokana na janga la virusi vya corona huku Simba wakiwa vinara wa Ligi hiyo, wakiwa na pointi 71 kabla ya kurejea na kuvuna pointi nne katika michezo miwili waliyocheza.

Katika mchezo wa leo, Simba wameishushia kipigo Mwadui cha mabao 3-0 huku wakicheza soka la kuvutia tofauti na ilivyokuwa katika mchezo wao wa kwanza ambapo walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting.

Mabao ya Simba, mawili yalifungwa kipindi cha kwanza na Hassan Dilunga huku la pili beki wa Mwadui, Augustino Samson akijifunga baada ya kupigwa kwa pasi mpenyezo na Shomary Kapombe aliyepanda kushambulia.

Bao la tatu la Simba, lilifungwa na nahodha wa kikosi hicho, John Bocco baada ya shuti la Luis Miquissone kugonga nguzo na kumalizia kwa kichwa mpira ulioshiwa kutazamwa na kipa wa Mwadui, Mahmoud Amir.

Baada ya kupata mabao hayo matatu, Simba walifanya mabadiliko kwa kuwatoa, Bocco,Fraga,Kapombe, Dilunga na Luis nafasi zao wakaingia, Meddie Kagere, Francis Kahata, Cletous Chama, Yusuf Mlipili na Mzamiru Yassin.

Chama ambaye mchezo wa leo ulikuwa wa kwanza kwake tangu arejee nchini akitokea kwao nchini Zambia alionekana kuwakosha mashabiki wa Simba kutokana na mbwembwe za hapa na pale ambazo alikuwa akizifanya.
 
Shadeeya karibu ushuhudie kandanda safi kutoka kwa mabingwa wa nchi Mnyama mkali Simba.
Njoo na wana Masumbwi wenzako mshuhudie burudani.

Simba nguvu moja
 
Hicho kikosi ilitakiwa atumie mfumo wa 3:4:3, ili Simba ikiwa haina mpira inarudi kwenye 5:2:3, na ikiwa inashambulia Luiz na Dilunga wanaingia kati uku Kapombe na Zimbwe wana overlap pembeni.
Hapo timu ingekua imara kwenye kushambulia na kujilinda.
Ila kocha ndo anajua atatumia mfumo gani, maana yeye ndo ame train na timu.
Simba Nguvu moja
 
huyu kocha anazidi kunichefua na upangaji wake wa list najua tutashinda ila kishingo aondoke Dilunga na boko walikuwa flop mechi ya mwisho lakini bado anawapa kipaumbele kuna wachezaji kama kina Deo Kanda wakiona wanawekwa benchi na hali wana uwezo wanaweza kuikimbia timu
 
Huyu kishingo naona anatafuta kufukuzwa kazi sio bure, na ashinde akirogwa apate droo tu imekula kwake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…