Uchaguzi 2020 Uwasilishaji wa sera za CHADEMA umeshiba na ndio unaoleta kizaazaa Lumumba

nina uhakika wahusika wameyaona maoni yangu na watayafanyia kazi.

ngoja niongee pointi zangu kwa volume kubwa...

1. kuhamasisha kupiga kura - doable
2. kura zihasebiwe vituoni - doable
3. wawakilishi kuhesabu kura - doable
Yote yanawezekana na yako kwenye uwezo wa NEC wakisimamia vizuri wasianze janjajanja
 
Tundu Lissu ni zawadi toka kwa Mungu.
Walimpiga risasi afe,ikashindikana.
Wakamvua ubunge na haki zake kuzipora,ikashindikana.
Yote hii ili Mtanzania aje apate ukombozi wa kweli.
Kura zote kwa Tundu Lissu.

LISSU; SAUTI YA HAKI ITAENDELEA KUNG’ARA

Nafsini waugulia, walotaka Lisu afe,
Sirini walivyomkalia, kula njama dhidi yake,
Wakitweta kwa kupania, eti Lissu aondoke,
Kung’ara itaendelea, SAUTI na nguvu yake.

Mjengoni walimtishia, kwa kugwaya hoja zake.
Na bila soni nje pia, kufisha maoni yake.
Wakishindana kumjazia, hata kesi ziso zake.
Kung’ara itaendelea, SAUTI na nguvu yake.

Pamoja na kumrarua, marisasi pale kwake.
Kwa jazba kumbania, hata salamu kwake.
Yarabi hakuridhia, mauti iende kwake.
Kung’ara itaendelea, SAUTI na nguvu yake

Pasi na kumchulia, nainuka peke yake,
Yale waliyomnuia, yamepita mbali yake,
Leo tumeshuhudia, kwa raha kurudi kwake,
Kung’ara itaendelea, SAUTI na nguvu yake.

Hakuna wa kuzuia, kishindo cha mwangwi wake,
Mola aliyemshindia, yupo na imara kwake,
Atazidi msimamia, kuokoa nchi yake,
Kung’ara itaendelea, SAUTI na nguvu yake.
 
Naona mode wamefuta ule uzi wa magufuli kukatiwa matangazo na TBCCM kisa kukataliwa huko kagera inawezekana jamiiforam ishafika bei.
Binafsi nimehudhuria mkutano wa CCM kuanzia Bukoba Mjini na Biharamulo. Kagera na haswa Biharamulo wamejitokeza kwa wingi kumpokea mgombea wa CCM John Magufuli, yanayosemwa ni uzushi tu..ukweli usemwe, Kama hukua eneo la tukio usipoteze muda kubishana
 
Elimu fake ya mkuu ilihojiwa na Ben akapotezwa hadi leo.


Bashite je? Ccm ukoo ule ule.

Ni yeye tu.
 
Lissu ni chaguo la Mungu aliye HAI.

Ndio maana ameshinda risasi 16.

Jiwe sijui ni mungu yupi labda wa Lumumba huko.
Angalia Mungu alivyotuvusha kwenye janga la Corona baada ya kumpa Magufuli maono.

Uyo Lissu wenu alikua anaandika ngonjera tu mitandaoni.
 
Wewe! demu akikubali kuingia gheto ndo tayari
 

Siyo kweli hata iwe HKL , PCM , M.D., Ph.D ya Korosho n.k mtindo ni huo huo 5W + H1

5W = Who? What? When? Where? Why?
1H= How?
 
Tundu Lissu ni zawadi toka kwa Mungu.
Walimpiga risasi afe,ikashindikana.
Wakamvua ubunge na haki zake kuzipora,ikashindikana.
Yote hii ili Mtanzania aje apate ukombozi wa kweli.
Kura zote kwa Tundu Lissu.
Tena ni baada ya kupiga ramli nakuona atakuwa raisi ajaye wakataka kumuua, wamesahau muona maoni hafi mpaka maono yatimie
 
[emoji23][emoji23][emoji111][emoji111][emoji106]
Sasa Unasema Ccm Hoyee
Watu Wanakunyooshea Vidole Viwili Juu
Mgombea Nafasi Ya Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Kwa Tiketi Ya Chama Dola
πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜πŸ˜€πŸ˜…πŸ˜„πŸ˜ƒ
 
mkuu NEC wasitegemewe kabisa kwenye hili.
my point is Chadema must proactively take a lead throughout.... wasiwe passive hata kidogo.
Chadema ndio sisi unataka chadema yupi tena
 
Angalia Mungu alivyotuvusha kwenye janga la Corona baada ya kumpa Magufuli maono.

Uyo Lissu wenu alikua anaandika ngonjera tu mitandaoni.
Na uganda M7 alipewa maono?? Vipi Sudani kusini kuna maono pia? Burundi je??
 
Tbc uliona walipozima Matangazo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…