SoC03 Uwazi katika huduma ofisi za ardhi

SoC03 Uwazi katika huduma ofisi za ardhi

Stories of Change - 2023 Competition

RAMAKISIMA

New Member
Joined
Jun 29, 2023
Posts
2
Reaction score
4
Ardhi ni rasilimali hitajika katika nyanja za kiuchumi, kijamii, kisiasa. Mahitaji ya ardhi yakuwa kwa kasi kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu na shughuli za kiuchumi. Serikali ya Tanzania Kwa kujua umuhimu wa ardhi imeweka wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi kwaajili ya kuratibu shughuli zote za umiliki wa ardhi ili kuondoa migogoro Kwa kugawa ardhi kulinga na shughuli hitajika Kwa wahusika.

Pamoja na juhudi kubwa zote bado sekta ya ardhi imekuwa na migogoro mingi saana kutokana na sababu zinazosababishwa na wananchi pamoja na Watumishiwa idara ya ardhi.

Sababu kubwa kwa wananchi ni uelewa mdogo wa taratibu za umiliki wa ardhi pamoja na tamaa wakati sababu kubwa kwa watumishi wa ardhi ni rushwa na tamaa. Wananchi wengi hawana uelewa wa taratibu, kanuni na sheria za ardhi hali inayochangia migogoro mingi saana baina ya wananchi na wananchi au wananchi na serikali. Uelewa mdogo huu umekuwa ukitumiwa na watumishi wengi ili kujinufaisha kwa;​
  1. Kuwauzia ardhi moja wateja zaidi ya mmoja​
  2. Kuomba gharama kubwa zisizotambulika kwaajili ya huduma​
  3. Kupora ardhi za wananchi​
  4. Kuchukua rushwa​
Uwepo wa ardhi unapaswa kuwa neema Kwa wananchi badala ya kuwa sababu ya vita. Migogoro huathiri saana shughuli za maendeleo na kupoteza amani baina ya wananchi kwa;​
  • Kutumia muda mwingi kuendesha kesi za migogoro na kufanya maeneo kuachwa bila kuendelezwa​
  • Kutumia fedha katika gharama za kesi badala ya fedha kutumika katika shughuli za kukuza uchumi​
  • Kutumia fedha kutibu majeruhi wa vita za migogoro ya ardhi​
  • Kutumia muda kuuguza majeruhi wa vita za migogoro ya ardhi​
Baadhi ya maswali yanayosumbua wananchi;
  • Mkataba upi wa mauziano ni sahihi kati ya ule wa mwenyekiti wa mitaa au kitongoji na ule wa mwanasheria?
  • Kiwanja kilichopimwa nitakitambua vipi?
  • Nitapataje ramani ya eneo ili kujua limepiwa au halijapimwa?
  • Ni sahihi kupimiwa na kampuni binafsi au lazima kupimiwa na serikali?
  • Bei halali za upimaji wa ardhi ni zipi?
  • Wanawezaje kulipia hati ya umiliki wa ardhi Kwa kuweka fedha kidogo kidogo?
  • Tofauti kati ya kiwanja na shamba ni ipi?
  • Nawezaje kubadili jina la hati ya umiliki?
  • Kodi ya kuuza kiwanja inajulikana vipi?
Kwakuwa serikali ya Tanzania inaamini katika dhana ya utawala bora yenye lengo la kuleta haki, usawa katika nchi kwa kuhakikisha uwajibikaji na ushirikishwaji wa wananchi katika shughuli za kuleta maendeleo katika nchi.

Hivyo wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi inapaswa Kuongeza uwazi katika taratibu za upatikanaji wa ardhi na urasimishaji Kwa kukuza uelewa wa wateja wake ambao ni wananchi kwa;​
  • Kuandaa nyaraka kwa Lugha ya kiswahili kuziweka mtandaoni na kuzisambaza katika ofisi za serikali za mitaa na vijiji zikiainisha. (a) Bei za gharama Kwa huduma, (b) Nyaraka hitajika, (c) Hatua za kufuata, (d) Wahusika wa kuwafuata ili kupata huduma. Wananchi wakitambua taratibu hizi itawaondolea uoga wa kufika ofisi za ardhi kwaajili ya huduma na kupunguza mianya ya rushwa Kwani kutokujua jambo husaidia​
  • Kuandaa kampeni zenye matangazo ya dakika 2 kupitia vituo vya redio na runinga zikieleza umuhimu na taratibu za umilikishwaji ardhi mfano kuwekan kauli mbiu "ardhi ni mtaji", au "rasimisha ardhi kuondoa migogoro"​
  • Kushirikiana na mitandao ya simu kuandaa jumbe fupi na kuzituma Kwa wananchi zikiainisha taratibu za umiliki wa ardhi na sheria za ardhi. Wananchi wengi Kwa sasa wanatumia simu kuwasiliana hivyo njia hii ni nyepesi saana kuwasambaza ujumbe Kwa wananchi kama ambavyo taasisi za polisi zinavyotuma jumbe za kutahadharisha juu ya utapeli wa mitandao.​
  • Kuanzisha chaneli ya mtandaoni "Ardhi tv" kwaajili ya kutoa elimu ya mambo ya ardhi. Taarifa za mara Kwa mara zinapotolewa husaidia kukuza ufahamu Kwa wananchi na kusaidia kusaambaa Kwa wepesi hali itakayosaidia kupunguza migogoro isiyo ya lazima.​
  • Kila ofisi ya ardhi ya wilaya kuwe na chati ya uongozi na mgawanyo wa majukumu ili kuwarahisishia wateja kujua kwenda ofisi ipi kulingana na hitaji husika.​
  • Kutengeneza programu tumizi ili kurahisisha watu kufanya baadhi ya huduma kupitia programu hizoo na si lazima kufika ofisi za ardhi.​
  • Kutumia wanasheria wasaidizi ngazi za vijiji kufanya mikataba ya mauziano ya ardhi ili kuepusha migogoro.​
  • Kuandaa dodoso la karatasi na la mtandaoni na kulisambaza Kwa wananchi ili kutoa maoni juu ya taratibu za huduma za ardhi. Hii itasaidia saana wizara kujitathmini juu ya mwenendo wake kwa kupata mrejesho Mmoja kwa moja toka kwa wateja.​
Hitimisho
Bila kuweka wazi taratibu za hudumaa za ardhi migogoro itazidi kukua na kushindwa kupatiwa ufumbuzi. Hali itakayofanya maendeleo kurudi nyuma. Mifumo ya mrejesho wa malalamiko ya wananchi lazima iwe hai na kutoa majibu sahihi Kwa wananchi. Uelewa Ukiona rushwa kwatika ardhi itapungu kwa kiasi kikubwa sana.


 
Upvote 3
Back
Top Bottom