Uwe na mguso chanya

Uwe na mguso chanya

nickvalerion2810

Senior Member
Joined
Mar 31, 2015
Posts
112
Reaction score
36
Katika maisha au ktk nyanja yeyote ya maisha unatakiwa uwe na mguso chanya..Uwepo wako lazima utambulike sio kwa kujaribu kujiinua mbele za watu na kujivika vazi la ukuu bali kwa kuwa na mguso chanya.

Uliwekwa ulimwenguni sio uje kusindikiza maisha au uje kuishi tu bali ktk maisha yako lazima uwe ma mguso ambao utakutengenezea utambulisho wako...huhitaji kuwa na ukamilifu au utajiri bali unatakiwa uwe na tabia chanya ambayo italeta majibu ya maswali yanayoumiza watu.

Usiwe moja ya matatizo bali tafuta kuwa suluhisho la matatizo...hii inawezekana pekee kwa kuwa na fikra huru ambazo zina utajiri wa ufahamu na hekima...

Kuwa wa tofauti...simaanishi kila kitu uwe mpinzani...la hasha bali uwe na uwezo wa kufikiri kwa upana...uwe na uwezo wa kujipambanua kimawazo...na uwe na uwezo wa kufikiri nje ya jedwari la UKAWAIDA...kuwa na ziada ya UKAWAIDA.

Usijifiche nyuma ya vivuli vya watu..usijifiche nyuma ya maoni ya watu...usijifiche nyuma ya makundi ya watu...ukiona unakubali kila kitu pasipo kutoa changamoto za kifikra jua huna mchango ktk eneo lile....Sikika, onekana....zungumza....toa mawazo yako....onyesha uasilia wako...

Hayo ni machache ila la msingi...Jiamini kuwa una uwezo wa kuleta mabadiliko chanya ktk ulimwengu....na unaanza kujifunza kubadili ulimwengu kwa kuleta mabadiliko ndani ya fikra zako na eneo ulilopo kwa kuwa na mguso chanya

Natumaini hii itakusaidia.
 
Back
Top Bottom