Uwe ni utaratibu: Wagombea kupewa Usafiri bure katika chaguzi

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
1,446
Reaction score
1,645
Habari Tanzania !

Eti mpenzi unaonaje, Wagombea waliothibitishwa na Vyama vyao na Tume ya Uchaguzi wapewe vyombo vya usafiri hoja kubwa ni; Wanatumikia umma.

Hii itachochea wagombea kujitokeza kwa wingi pasipo uoga wowowte ule na kutakuwa na uchanuaji wa ushindani kikamilifu. Baada ya uchaguzi kuisha vyombo vya walioshindwa vinarudishwa Serikalini mpaka tena msimu ujao wa chaguzi.

1. Rais - Gari kubwa (Mkonga)
2. Mbunge - Gari kubwa (Mkonga)
2. Diwani/ Sheha - Gari ndogo mfano; IST
3. Mwenyekiti - Pikipiki

NB
1. Maintenance ni bure kipindi cha uchaguzi.
2. Mafuta watajipata wenyewe; hakuna bure kwenye hili.

Tujipe raha wenyewe maana mauchaguzi yenyewe yanafanyika mara moja kwa miaka 5. Wapeni watu raha kwenye nchi yao aisee.

Karibu.
 
Nina maswali, gari wanapewa moja kwa moja ama zinarudi INEC baada ya uchaguzi? Kama wanapewa moja kwa moja je zinakuwa za wagombea ama chama cha mgombea?
 
Hivi mna habari uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi wagombea wa ubunge wa vyama vyote walipewa ruzuku ya kampeni? Kuna watu waliopiga fedha za bure kwa kutumia vyama ambavyo hata vilikuwa siyo maarufu. Kna mwamba mmoja alichukuwa fedha akafungulia duka.
 
Hayo magari yanapotelea kusikojulikana CHADEMA wakiwepo
 
Zinarudi toka Tume. Tume watajua wapi kwa kuzipeleka baada ya uchaguzi.
 
Hivi mna habari uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi wagombea wa ubunge wa vyama vyote walipewa ruzuku ya kampeni? Kuna watu waliopiga fedha za bure kwa kutumia vyama ambavyo hata vilikuwa siyo maarufu. Kna mwamba mmoja alichukuwa fedha akafungulia duka.
Ikipendeza tupate wagombea wenye ushindani sawa. Lengo tupate watu bora kwenye viwango vikubwa.

Sioni raha kushindanisha watu tofauti tofauti kwa mizani tofauti alafu utegemee tupate wagombea wenye ubora wa kutuongoza vizuri?
 
Hayo magari yanapotelea kusikojulikana CHADEMA wakiwepo
Nimezungumzia mahusiano kati ya Mgombea na Tume hapo chama watakomaa labda na huduma nje na huo usafiri.

Acha imani potofu hata kama kuna kundi au watu unatofautiana nao usiwape mawazo mabaya.
 
Back
Top Bottom