Uwekaji Meter za Maji Nje ya Nyumba na Wizi wa bomba zake ikidaiwa ni wauza Vyuma Chakavu

Uwekaji Meter za Maji Nje ya Nyumba na Wizi wa bomba zake ikidaiwa ni wauza Vyuma Chakavu

Bhaghosha

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2010
Posts
234
Reaction score
183
Wiki hii huko Arusha usiku wa manane watu wasiojulikana waling'oa mabomba yanayounganisha meter za maji na kuondoka nazo. Inasadikiwa siyo chini ya meter 25 katika eneo hilo. Wanainchi wanaamka asubuhi wanakuta maeneo yao yamefurika na maji.

Idara ya maji ilipojulishwa ilijivuta kuja kudhibiti uharibifu huo na pia kusema hawawezi kurudishia hizo meter, ila kila mmoja aende idara ya maji akanunue tena vifaa vya kuunganishia kwa gharama ya kama 60 elfu.

Chakujiuliza.
1. Kwa nini wizi au uharibifu huo utokee sehemu moja na wakati mmoja?

2. Kwa nini Idara ya maji isirudishie hayo mabomba kwa gharama zao, kwa sababu wao ndiyo waliotaka meter ziwe nje?

3. Haiwezi kuwa ni njama ya idara ya maji kujipatia pese tena kwa kusababisha uharibifu huo? Haiingii akilini muuza scrappper achukue risk ya kung'oa vi pipe viwili kweli.

4. Baada ya kuripoti, kwa nini Idara ya maji haijaja na polisi kuchukua ushahidi bali wanang'ang'ania watu wakalipie vifaa vya kuunganishia.

Idara ya maji Arusha mko nashida.
 
Back
Top Bottom