Uwekaji wa tank la maji

Uwekaji wa tank la maji

Tempest

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2022
Posts
245
Reaction score
430
Habari wadau

Nataka kuweka tank juu la 3000 lita liingize maji ndani sababu maji ys dawasa hayaeleweki yaani kutoka siku tatu mfululizo ni bahati kwahyo ikitokea hakuna ni mwendo wa kutoka na ndoo nje kuchota kwenye tank

Je tank likiwa juu presha ya maji inakuwa nzuri kutumia kama kwenye shower na mambo mengine kama inavyokuwa majinya dawasa kwenye ubora wake

Na pia utaratibu umekaaje kwenye kulijaza tank yaani yanaingia kwenye tank na kisha yanatoka kwenye tank kuingia ndani? Au kuna namna gani ya kuuweka sawa huu mfumo

Na makadirio ya gharama kufanikisha hili

Ahsanteni.
 
Ili kuongeza presha ya maji, huwa tunatumia reducing socket au unequal tank connector. Kwenye hiyo reducing socket au unequal tank connector, upande ambao maji yanaingia kunakuwa kukubwa mfano inaweza ikawa nchi 1 au 3/4" , na upande ambao maji yanatokea, kunakuwa kudogo mfano inaweza ikawa 3/4" au 1/2"

Mbali na hivyo, tundu la kusambazia maji katika tank(tundu la chini), linatakiwa liwe katika urefu unaozidi urefu wa tundu la bomba la mvua. Mfano kama tundu la bomba la mvua lipo katika urefu (hapa nazungumzia height) wa futi 8 kutokea kwenye floor, tundu la tank la kusambazia maji linatakiwa liwe katika urefu wa angalau futi 12

Tank la maji huwa linatobolewa matundu mawili, juu kabisa na huku chini (lakini yote yanatobolewa pembeni). Tundu la juu ni la kuingiza maji kutoka kwenye bomba/dawasco kuingia kwenye tank, na tundu la chini ni la kusambaza maji ndani ambapo kunakuwa na koki inayoact kama main switch inavyofanya kazi kwenye umeme (ukipafunga hapo, hata kama ndani utafungua bomba, maji hayatotoka)

Lakini pia unaweza ukatoboa tundu lingine juu, ili maji yatakapokuwa yamejaa kupita kiasi kinachotakiwa kwenye tank, maji yapate outlet ya kutokea

Ramani, Makadirio au Ushauri kuhusu Ujenzi tuwasiliane
 
Vipi kwa jengo la ghorofa. Tank Tower linatakiwa liwe kimo gani?.
 
Kwa majengo ya ghorofa, mara nyingi matank huwa tunayaweka juu ya mfuniko (slab) wa ngazi za kupandia floor ya chini kwenda floor ya juu, haina haja ya kujenga mnara
 
Back
Top Bottom