Ili kuongeza presha ya maji, huwa tunatumia reducing socket au unequal tank connector. Kwenye hiyo reducing socket au unequal tank connector, upande ambao maji yanaingia kunakuwa kukubwa mfano inaweza ikawa nchi 1 au 3/4" , na upande ambao maji yanatokea, kunakuwa kudogo mfano inaweza ikawa 3/4" au 1/2"
Mbali na hivyo, tundu la kusambazia maji katika tank(tundu la chini), linatakiwa liwe katika urefu unaozidi urefu wa tundu la bomba la mvua. Mfano kama tundu la bomba la mvua lipo katika urefu (hapa nazungumzia height) wa futi 8 kutokea kwenye floor, tundu la tank la kusambazia maji linatakiwa liwe katika urefu wa angalau futi 12
Tank la maji huwa linatobolewa matundu mawili, juu kabisa na huku chini (lakini yote yanatobolewa pembeni). Tundu la juu ni la kuingiza maji kutoka kwenye bomba/dawasco kuingia kwenye tank, na tundu la chini ni la kusambaza maji ndani ambapo kunakuwa na koki inayoact kama main switch inavyofanya kazi kwenye umeme (ukipafunga hapo, hata kama ndani utafungua bomba, maji hayatotoka)
Lakini pia unaweza ukatoboa tundu lingine juu, ili maji yatakapokuwa yamejaa kupita kiasi kinachotakiwa kwenye tank, maji yapate outlet ya kutokea
Ramani, Makadirio au Ushauri kuhusu Ujenzi tuwasiliane