Ladder 49
JF-Expert Member
- Dec 19, 2017
- 7,918
- 20,037
Ni wazi mpira wetu wa miguu Tanzania bara kwa sasa umekuwa, lakini kukuwa bila ya ongezeko la usajiri kwa wachezaji wazawa nje na ndani ya nchi ni kazi bure. Maana haitasaidia kwenye ongezeko la ajira kwa vijana na ukuaji kiuchumi ,bali kumnufaisha tu mmiliki wa timu.
Kuwekeza kwenye Data na Takwimu
Data na takwimu(Data and statistics) ndio msingi wa maendeleo katika jamii yoyote ile ikiwa ni pamoja na kwenye soka la mpira wa miguu.
Kuzingatia takwimu na vipimo (statistics and metrics) katika sera ya usajiri wachezaji wa mpira wa miguu kunafanana na ile kanuni ya ‘Mpira Pesa’ yaani “moneyball”
Moneyball ni wazo la kuthamini data zaidi kulingana na ushahidi ili kusajiri wachezaji bora wa mahitaji yako.
Usajiri unafanywa kuzingatia takwimu na data (statistics and data) za mchezaji katika mechi alizocheza hii itapelekea usajiri wa wachezaji kwenye ligi ya ndani kusajiriwa kwa wingi na kwa gharama ndogo, napengine kuwa na ubora ambao sawa tu na wachezaji wengine walionuunuliwa kwa thamani kubwa ya pesa.
Usajiri wa kuzingatia takwimu na data (statistics and data) unaangalia shughuli zote za ndani ya mchezo wa mpira wa miguu kwa maana ya kuchukua taarifa kwa wachezaji wote , wachezaji wa mbele mashuti waliyopiga golini wamefunga mangapi na mangapi wamekosa.
Kwa upande wa kama kiungo mkabaji amekaba mipira mingapi kwenye ligi ukilinganisha na wachezaji wengine.Kwa wachezaji wa pembeni amewatoka mabeki wangapi kwenye ligi, Kama ni golikipa umeokoa mashuti mangapi ya hapa na hapa na mengineyo mengi .
Hii yote Madhumuni yake ni kutathmini uchezaji wa mchezaji na kuweka katika chati(graph) ambazo zitaeleweka katika kujibu maswali yako ya mahitaji yako ya mchezaji unayemtaka.
Kwa hivyo, hii inatoa maarifa yenye lengo katika kuonesha ubora wa mchezaji katika uchezaji na uwezo mwingine wa wachezaji ambao utakuwa wa manufaa kwa kocha katika kuchagua kikosi cha kuanza na wachezaji wengine watakaofaa kwenye timu.
falsafa ya ‘Mpira wa Pesa’ na wazo la kutumia data kutafuta wachezaji vimebadilisha sana hali ya soka la mpira wa miguu. Sasa hivi vilabu vya mpira wa miguu utathmini takwimu na data (statistics and data) ili si tu kupata wachezaji wanaoweza kusajiliwa bali pia kuchanganua uchezaji wa mchezaji.
Sasa ni wakati wa kuangalia kwa kina jinsi tunavyoweza kutafuta wachezaji kwa kutumia data na takwimu na vipimo vingine,ili kupata picha bora ya uwezo wa mchezaji na kufanya maamuzi sahihi zaidi wakati wa kusajiri wachezaji kwa kuzingatia namba, badala ya maoni ya kibinafsi kama vile mapendekezo ya skauti na maoni ya skauti kuhusu uwezo wa wachezaji .
Hali iliyopo kwa sasa kwenye usajiri wa wachezaji wa mpira wa miguu ligi ya Tanzania bara.
Kwa muda mrefu sasa kumekosekana sehemu ya uhakika kwa timu kwenda kusajiri wachezaji wanaowataka, wachezaji wazawa kutokuwa na thamani yakuuzika kwenye ligi za nje, na pia kutokuwepo kwa upatikanaji wa data za wachezaji wa mpira wa miguu kwenye ligi ya Tanzania kuanzia kwenye ligi kuu mpaka kwenye madaraja mengine ya chini.
Timu zinaenda kwenye mataifa mengine kama Zambia, Rwanda,Burundi ,congo, bukina faso na mataifa mengine kuangalia mchezaji gani kule amekuwa MVP au amekuwa mchezaji bora au mfungaji bora.
Timu zetu za ndani kubwa zinatumia pesa nyingi sana kusajili wachezaji wa kigeni lakini baada ya nusu msimu au msimu mmoja tu wanamuacha mchezaji wanaingia hasara.
Kumekuwa na ubahatishaji sana kwenye sajili za wachezaji kwenye ligi kuu ya soka Tanzania bara.Mchezaji aliyesajiriwa kwa gharama kubwa kutoka nchi nyingine kumbe anakiwango kidogo au sawa na mchezaji wa timu ya ligi kuu ya tanzania bara.
Kwa wachezaji wa ndani hawawezi kuonekana kutokana na hakuna sehemu yoyote namba zake zinaweza kuonekana baada ya msimu kuisha, mara nyingi wanaangalia tu kwa macho ulivyocheza wanakusajiri baada ya nusu msimu wanakuacha unakiwango kidogo.
Haiwezekani kusajiri mchezaji kwakuangalia kwa macho tu, ndio maana hao wachezaji wanashindwa,na tumewaona wengi tu kwenye ligi kuu Tanzania bara.
Baada ya ligi kuisha hakuna data na takwimu kwa wachezaji nani amefanya vizuri kwenye upande wa namba,kuwepo kwa namba ingepelekea wachezaji wa ndani kugombaniwa wakati wa usajiri na wachezaji kujituma,maana namba zitanitambulisha tu sio kusubiria mpaka ucheze na timu zenye majina makubwa ndio uonekane.
Suluhisho .
Wasimamizi wa ligi/timu binafsi kuunda Mfumo wa Takwimu na data za Wachezaji wa mpira wa miguu Kupitia Video za mechi husika.
kuwepo na kitunzia taarifa(database) za wachezaji kulingana na takwimu na data,hata kama ligi daraja la pili haioneshwi lakini namba zioneshe mchezaji gani alikaba au kunyang’a mipira mingi sana. Jumla ya pasi alizopiga msimu mzima na alizofanikiwa,mipira mirefu mingapi amepiga,idadi ya mashuti yaliyolenga goli na umefunga magoli mangapi, kwa beki mipira mingapi ya vichwa ameruka na kuokoa. Mchezaji gani Aliye watoka mabeki wengi(dribbling) na mipira mingapi aliyopoteza.
Matokeo Chanya ya Suluhisho.
Inakuwa rahisi kumshawishi mtu hao ndio wachezaji bora kwenye ligi ya Tanzania, namba zinaongea zenyewe sio mapenzi ya mtu na mchezaji.Ingeboresha ligi ya Tanzania kwa kiasi kikubwa sana na kuuza wachezaji na kuongeza usajiri wachezaji wa ndani na kuuza taarifa za wachezaji.kwa maana tofauti na hivyo ni ngumu sana mchezaji kusajiriwa nje na ndani ya nchi japokuwa anauwezo wa kucheza vizuri tu.
Hii itapelekea kupunguza timu zetu kupata hasara kwenye usajiri wa gharama kubwa,mchezaji anasajiriwa kwakuambiwa tu maneno yule yuko vizuri, akija kucheza kwenye ligi nusu msimu tu anaachwa.
Kwa kusajiri vijana wa ndani kutawapa ajira vijana nakukuza uchumi wa nchi,Hii pia itasaidia kwa timu ndogo zisizokuwa na uwezo wa kipesa kusajiri kwa gharama ndogo sana wachezaji wa ndani na kuwapa mazoezi kidogo ya kuwaboresha na wachezaji hao kufanya vizuri kwenye ligi na kuwauza kwa gharama kubwa kwa timu zingine.
Hitimisho.
Statistics na data ndio dunia ya mpira kwa sasa ilipo,lazima tutumie namba kuangalia ubora wa mchezaji, na sio tu mpaka tusubirie mechi za kimataifa ndio tuajiri mashirika mengine kutupa namba za wachezaji wa timu pizani hata kwenye ligi yetu tunaweza kufanya hivyo.
Sasa ndio wakati wa wachezaji wetu kuwa na data na takwimu kwa ajiri ya kuwauza nje na ndani ya nchi na kuleta ukuajiwa wa soko la Ajira na Uchumi katika mchezo wa mpira wa miguu ligi Tanzania bara.

Upvote
7