Black Author
New Member
- May 5, 2024
- 1
- 1
TANZANIA TUITAKAYO
Black Author
Utangulizi
Dira halisi ya maendeleo ya taifa lolote linaloendelea,na lililoendelea katika mipango yake,huzingatia sana mambo mawili yafuatayo,Kwanza,ni nadhari na la mwisho ni vitendo ili kuifanya nadharia kuwa hai,viongozi Kwa ushirikiano,huweka mipango Yao ya muda mrefu na mfupi. wanatenga bajeti ya kimkakati ili kutekeleza mipango katika nadharia waliyojiwekea.Tukijitathmini katika nchi yetu pia,Kwa kuzichunguza fursa kubwa za rasilimali tulizo nazo,ni dhari kuwa tunao uwezo mkubwa sana wa kupanga mipango yetu ya muda mfupi na hata mrefu kama miaka 5 Hadi 25, Kwa guzigusa kikamilifu sekta zifuatazo.
Sheria za nchi, Uboreshaji wa sarafu ya Taifa, Miji na vijiji, Nguvu kazi na rasilimali watu, Habari,Wana habari na wazalishaji habari,Urasimishaji wa kazi na makazi na Mashamba na misitu,hapa ni Kwa kuanzia tu.
Sheria za nchi.
Kwa kuundwa Kwa katiba mpya na kuipitia kikamilifu kisha tukaielewa na kuutambua wajibu wetu Kwa Taifa Sisi kama raia,na kisha viongozi wa Taifa wa kila sekta katika jamii,kuyaelewa na kuyatambua majukumu Yao Kwa raia na Kwa Taifa zima Kwa ujumla,katiba mpya itakuwa na uwezo wa kutusaidia Kwa pamoja kuyafikia malengo ya Dira yetu Kwa pamoja kama Taifa.
Katiba mpya yenye usawa Kati ya kiongozi na raia wa Hali ya chini,isiyo na upendeleo,itatufikisha katika Dira timilifu ya maendeleo ya taifa letu Kwa faida ya Taifa zima.
Kitu kingine Kwa upande wa Sheria,ni sheria za kuwapigia Kura viongozi tusiokuwa na Imani nao katika utenda wao wa kazi,kuanzia kiongozi wa ngazi ya juu Hadi ya chini,hatua hii italeta ustawi Bora na uzalendo imara katika Taifa zima tutaweza kufika mbali Kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa raia mmoja mmoja na Taifa Kwa ujumla.
Lakini kukiwa na sheria za uzalendo,zitaweza kutufikisha mbali katika kupiga hatua ya kuyafikia maendeleo ya kweli Kwa Taifa zima Kwa muda usio pungua miaka mitano Hadi kumi na mitano.
Elimu ikipelekwa kikamilifu Kwenye jamii juu ya uzalendo na umuhimu wa kuzituza sheria zote za nchi Kwa manufaa ya Taifa zima.
Ubadilishaji wa sarafu ya Taifa.
Katika Tanzania ya miaka 5 tunaweza kubadili sarafu yetu kwa kutengeneza mfumo wa sarafu yetu mpya,itakayoendeshwa kwa madini yetu kama Tanzanite,Dhahabu,Almasi na hata Gesi,Kwa kuwekeza kikamilifu katika sekta ya madini na Vito vyote vya thamani kwa maslahi ya Taifa letu Kwanza na wananchi wetu Kwa ujumla.
Hapa chini ni mfano wa taswira ya sarafu itakayobeba taswira halisi ya utaifa wa Taifa la Tanzania.
Jina:TAHANIA (maana ya neno hili ni)- Pongezi zinazotolewa Kwa matendo mazuri yaliyotokea au yaliyotendwa.
Lakini neno hili lina uambatano sauti wa neno Tanzania.Hivyo neno hili litabeba uzalendo wetu,na U Tanzania wetu.
Mbunifu wa Alama hii ni: Emmanuel C. Owiti
Ufafanuzi wa alama Tt
T kubwa inawakilisha Tanzania na t ndogo inawakilisha tahania.
Ufafanuzi zaidi wa nembo hii ni kama ufuatao:T kubwa inawakilisha Tanzania bara na t ndogo inasimama kama Tanzania visiwani.
Mfano wa pesa; msaada google
Miji na vijiji.
Miji yote mikubwa(makao yote makuu ya mikoa) itakapokua na uwezo wa kuwekezwa kisasa ndani ya miaka 10 Hadi 25,Kwa kuwekeza kikamilifu katika miundombinu muhimu Kama vile barabara kutokea mijini Hadi vijijini,viwanda vikubwa na vya Kati,majengo marefu ya kisasa kisha kuchunguza vijiji vyenye rutuba na kuvigeuza kutoka matumizi ya makazi,na kuvifanya kuwa Mashamba ya kisasa Kwa ajili ya kilimo chenye tija,pamoja na ufugaji wa viwango vya juu,tutafika mbali ndani ya miaka mitano Hadi ishirini na tano.Lakini Sheria za umiliki ardhi ni Bora zikachunguzwa upya,na kuundwa upya ikiwezekana serikali iwe na umiliki wa ardhi Kwa asilimia 70% na kuipima kikamilifu,wamiliki watambulike na serikali kuu,kisha iwekezwe Kwa tija Kwa wakulima wenye mitaji mikubwa,ama serikali iweze kurudisha Mashamba ya ushiri,ili vijana ambao kwa kawaida ni nguvu kazi ya Taifa,waingie shambani Kwa kutumika Kwa ajili ya ustawi wao na wengine kuajiriwa kwenye viwanda vya ushirika,ili kuinua vipato vyao.
Picha hizi zimebuniwa na kuchorwa na:
Emmanuel C. Owiti.
Habari,Wana Habari na wazalishaji habari.
Tasnia ya Habari,Wana habari na wazalishaji habari nchi,ikiwekewa mkazo katika kuhimiza uwazi,ukweli,kuepuka uchochezi,sifa zilizopitiliza na kukera Kwa niaba na maslahi ya kundi flani,ili kuweza kupata upendeleo flani katika ngazi flani.Vihubiri siasa Safi,Utamaduni wetu,uhuru,Haki,uweledi,na miiko ya kiandishi katika tasnia ya habari ndani ya miaka mitano,inaweza kutufikisha katika viwango vya Hali ya juu .
pia tukiweka utaratibu wa kusambaza habari zetu kuanzia ngazi ya mikoani Hadi kwenye ngazi za wilaya na vijiji Kwa kuweka maduka ya kudumu yanayotambulika kisheria na yaliyosajiliwa kisheria,Kwa ajili ya usambazaji na upokeaji wa habari mbalimbali kutoka Kwa wazalishaji na wasambazaji wa ndani na nje ya nchi,miaka kumi Hadi kumi na mitano.
Nguvu kazi na rasilimali watu.
Eneo lingine la kuchunguza,ni nguvu kazi na rasilimali watu.Tukiwatumia vyema vijana katika uzalishaji Mali,Kwa kusimamia kikamilifu Haki zao katika maeneo yote ya uzalishaji Mali,iwe ni nje ya nchi hata nchini,ndani ya miaka mitano Hadi kumi,tutaweza kufika mbali Kwa kuweza kukusanya Kodi na kuwa na ustawi wa mtu mmoja mmoja.
Kwa kuweza kuizuia mianya yote ya matumizi ya dawa za kulevya,kuweka sheria Kali Kwa wauzaji na watumiaji wa dawa hizo, kuondoa tamaduni zisizorafiki Kwa vijana wetu,Kwa kuwawekea mazingira ya kisheria zaidi na kuwapa mbadala wa kazi,itasaidia kuondoa wimbi zito la upotevu wa Nguvu kazi na rasilimali watu hasa Kwa upande wa vijana wengi ambao ndio wapo hatarini.
Urasimishaji kazi na makazi.
Miaka mitano Hadi kumi tukifanikiwa kurasimisha kazi zote zenye uwezo wa kuingiza pato la uhakika Kwa mwezi ,tutakuwa tumepiga hatua kubwa ya kimaendeleo,Kwa kuweza kukusanya pato la Taifa Kwa viwango vya juu.Kurasimisha makazi kikamilifu Kwa kufikisha huduma muhimu kwa raia wetu,itatusaidia kupunguza,ama kuondoa kero zilizo ndani ya uwezo wetu Kwa jamii yetu nchi nzima.
Mashamba na misitu.
Kwa kutenga maeneo maalum ya mashamba na misitu kutatusaidia kufika mbali na kuepusha migogoro na hasara nyingi zinazojitokeza Kwa kutokuwa na umiliki wenye tija wa ardhi Kwa Taifa na hata Kwa raia Kwa ujumla.Serikali pamoja na wananchi tukija pamoja katika majadiliano,nakuweza kukubaliana kuhusu njia sahihi za kuwekeza Kwa tija,tutafika mbali Kwa kuweza kupata faida Kwa kila mmoja wetu kupitia kilimo na misitu.
Hitimisho.
Kwa ufupi na Kwa kuzingatia mambo mawili,maono na vitendo katika serikali yetu,Kwa vipengele vilivyoainishwa Katika andiko hili,ni wazi na dhahiri kuwa tunaweza kufika mbali,Kwa kutekeleza kikamilifu mipango yetu ya muda mrefu na mifupi Kwa kuzingatia na kusimamia bajeti yetu kikamilifu katika kila sekta.

Upvote
2