SoC01 Uwekezaji kwa ajili ya Mtiririko wa Pesa (Cashflow investment)

Stories of Change - 2021 Competition

Masibayi

Member
Joined
Jan 2, 2018
Posts
19
Reaction score
65
Nukuu kutoka kwa Bibi;
Mjukuu wangu; pesa haitafutwi kama kutafuta mtu. Ni lazima uchimbe mfereji ambao utazileta kwako. Ukifanikiwa zitakuja kama maji,cha msingi wewe uwe mwisho wa mfereji ili kuzipokea. Ukinielewa utatajirika. (Maneno ya Bibi yangu, aliyasema mwaka 2014 kufuatia kufeli jaribio langu la biashara ya samaki.​
Uwekezaji kwa ajili ya mtiririko wa pesa unajikita katika kukupa kipato mara kwa mara. Hii ni tofauti na ule uwekezaji wa kuongeza mtaji ambapo bidhaa ikishaenda hupati hela mpaka ununue bidhaa nyingine tena.

Funzo kutoka kwenye ranchi:
Ukienda kuangalia ranchi za ng'ombe wa maziwa na ng'ombe wa nyama utaona tofauti kubwa sana.

Katika ranchi ya maziwa faida hutegemea na utunzaji wa ng'ombe mmoja mmoja. Ng'ombe huyo akitunzwa vizuri mwekezaji humpatia maziwa mengi kila siku.

Katika ranchi ya nyama faida hutegemea utunzaji wa ng'ombe na kubwa kuliko ni idadi yao. Ili mwekezaji anufaike ni muhimu awe na ng'ombe wa kutosha kuchinja ili kukidhi mahitaji. Baada ya hapo anatakiwa kutafuta ng'ombe wapya. Hapa ndipo kazi inapokuwa kubwa zaidi.

Gharama za kuendesha ranchi ya nyama ni kubwa kuliko ranchi ya maziwa.

Uwekezaji kwa ajili ya mtiririko wa pesa, cashflow, ni mithili ya ranchi ya maziwa.

Nini kiwe kipaumbele?
kimsingi sikwambii nini ufanye ila nakupa taarifa ili uamue nini ufanye.

Ikiwa utawekeza kwa ajili ya mtirirko wa pesa utapata faida ya msamaha mkubwa wa kodi, utapata nguvu dhidi ya mfumko na mdololo wa bei pamoja na pia utakuwa na uhakika wa kuingiza pesa katika hali zote za uchumi. Je, kwa nini uwekeze kwa ajili ya ongezeko la mtaji?

Ingawa kuna faida ya kukopesheka kirahisi kutokana na uwekezaji wa ongezeko la uchumi, bado kiwango cha dhamana kwa mtu aliyewekeza kwa ajili ya mtiririko wa pesa ni kikubwa kuliko yule wa ongezeko la mtaji.

Hii ni kwa sababu benki huangalia uwezekano mkubwa wa kupata pesa yao baada ya kuwa wamekupa bila kujali hali ya uchumi.

Je, wewe ni mgeni katika dunia hii?
Ni mgeni pekee ndo hajui kuwa haijalishi vyuma vimekaza au la biashara ya vinywaji, madawa, chakula, makazi, mafuta, usafiri na mawasiliano huwa hazilali.

Watu wakiwa na msongo wa mawazo hunywa pombe,pia wakiwa na furaha hunywa pombe. Watu wakiwa na hali mbaya huwasiliana kama vile wakisa na hali nzuri. Tajiri na maskini wote wanahitaji paa la nyumba juu ya vichwa vyao, wanahitaji madawa wakiumwa, wanahitaji kusafiri na pia wanahitaji kuweka chakula juu ya meza.

Hizo ni fursa chache tu kwa kuzitaja. Ziko nyingi zaidi ya hizo.

Mchezo wa pesa
kanuni ya mchezo wa pesa katika uwekezaji inasema kuwa ukifanikiwa kuwafanya watu wakutumie hela zao kwa wingi tena mara kwa mara unakuwa umeula.

Wafanye watu wakutumie hela zao. Huo ndiyo ukiritimba, monopolism.

Nani kala zaidi?
Wote wanaowekeza kwa ajili ya ongezeko la mtaji au mtiririko wa pesa wameula. Lakini anayewekeza kwa ajili ya vyote ameula zaidi.

Kwa mfano; huduma ya kutuma pesa kwa kutumia mitandao ya simu. Hapa mwekezaji hupata kamisheni kwa kila mwamala. Watu wengi wanatumia huduma hizi na miamala mikubwa inafanyika. Unaweza kuona kaula kiasi gani ukilinganisha na mama n'tiliye ambaye wateja wasipokuja mtaji unageuka kuwa mlo wa usiku kwake.

Akili kubwa
Dunia ni kubwa sana, inahitajika akili pana ili kuishi. Anayepingana na mfumo huondolewa tofauti na yule anayeamua kuutumia mfumo kwa ajili ya manufaa yake mwenyewe.

Tumia akili kuwekeza kwa ajili ya vyote, upate ongezeko la mtaji na upate mtiririko wa pesa.

Mfano; mtu mwenye biashara ya nyumba ya kupangisha anaweza kuchukua mkopo benki. Mkopo huo unalipwa na wapangaji wake na atapata msamaha wa kodi kutokana na deni hilo.

Ikiwa mkopo ni mkubwa kushinda thamani ya nyumba tayari tunaona kapata faida ya ongezeko la mtaji wake bila kulilipia kodi kisheria kabisa. Kwa kuwa bado anapangisha pia tunaona anapata faida ya pili ambayo haitozwi kodi katika viwango vya kipato cha kawaida kama ilivyoainishwa kisheria.

Kutegemea na mfumo wa biashara yake kama ni kampuni (corporation) pia ataruhusiwa kufanya matumizi kabla ya kukatwa kodi na hivyo atalipa kodi kidogo tofauti na mwajiriwa aliyesajiriwa.

Hiyo ni akili kubwa sana.

Rai yangu
Sheria ya kodi imewekwa ili kuhamasisha uzalishaji na utoaji wa huduma ambazo ni kipaumbele kwa serikali. Hiki ndicho kinachosababisha viwango vya tozo kutofautiana katika makundi mbalimbali pamoja na namna ya tozo.

Ili kunufaika na sheria hii ni muhimu kufanya mageuzi kwa kuhamia upande ambao unapata nafuu ya kodi. Huo ni upande wa wafanya biashara na wawekezaji.

Wekeza leo kwa ajili ya mtiririko wa fedha ufaidike dhidi ya mfumko wa bei, kodi na hali zote za uchumi.

Asante.​
 
Upvote 5

Dah umenifungua mkuu[emoji1666][emoji1666][emoji1666]

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom