SoC03 Uwekezaji sahihi kwenye sekta ya uzalishaji ndio mwarobaini wa tatizo la ajira nchini

SoC03 Uwekezaji sahihi kwenye sekta ya uzalishaji ndio mwarobaini wa tatizo la ajira nchini

Stories of Change - 2023 Competition

John Kwambaza

Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
6
Reaction score
4
Huku mitaani idadi ya vijana wasio na ajira ni kubwa na inazidi kuongezeka Kila uchao. Tatizo ni kubwa na linazidi kuongezeka kwa Kasi,ajira ndio msingi wa kipato na kipato ndio msingi wa maisha.

Yapo mawazo yanayowataka vijana wajiajiri,kinadharia ni dhana nyepesi kuizungumza lakini ngumu kiutekelezaji. Binafsi nilishafuata maelekezo hayo na kwakweli nilitumbukia kwenye shimo ambalo nilishindwa kutoka.

Katika kujiajiri zipo changamoto za kimsingi Sana ambazo ni lazima tuzizingatie, kwanza ni ukosefu wa mitaji ya kuanzishia na kuendeleza miradi, pili ni ukosefu wa maarifa ya kutosha kuhusiana na shughuli mtu anayopanga kuifanya, tatu ni ufahamu mdogo wa mtandao wa masoko na tabia zake.

na masuala na changamoto zilizopo najiridhisha kabisa kwamba huu ni wakati sahihi kwa jamii ya watanzania kite geneza mjadala mpana wa kitaifa wa njia mbadala za kupata fursa za ajira kwa watoto na vijana wetu/wenzetu. Ukweli mchungu ni kwamba vyovyote itakavyokuwa serikali pekeyake haiwezi na haitakuja kuweza kuwameza wote wanaohitaji na wenye sifa za kuajirika;hata iweje na hata serikali iongozwe na nani.

Kwahiyo ni lazima tulazimike kufikiri nje ya boksi. Katika kuchangia mjadala huu mpana mimi ninamaoni yafuatayo. Sisi Kama jamii tuanze kuwekeza kwenye sekta za uzalishaji kwa nguvu kubwa. Hii ndio iwe kauli mbiu na kauli Kiongozi wetu.Maeneo ya kiuzalishaji ya kimkamkati (current strategic productive areas)kwa Sasa ni Kilimo,uvuvi,uchimbaji na nishati.

Napendekeza uwekezaji katika maeneo hayo kwa sababu kadhaa kwanza hayo ni maeneo ambako ni rahisi kuwekeza hata kwa mtaji na utaalam wa kawaida,pili ni maeneo ambayo products zake zinahitajika katika maisha ya Kila siku na pia zinahitajika kwa upana,tatu ni maeneo ambayo upatikanaji wa soko ni rahisi, nne haya ni maeneo ambayo yanaweza kuajiri vijana wengi zaidi wasomi na wasiowasomi.

Mawanda ya kiutekelezaji(scope of operation) katika maeneo hayo au Moja kati ya maeneo hayo(kipaumbele) yanaweza kuzingatia kiwango Cha familia,mathalani Kila mwaka tunao wanajamii kadhaa ambao wanapata fursa ya kupata fedha nyingi kwa mkupuo kupitia akiba baada ya kustaafu au michezo ya kubahatisha.

Mimi naamini makundi haya ya watu wanaopata lapusam ya fedha yanaweza kuwa ni waanzilishi wa vibwenyenye uchwara katika kuanza uwekezaji kwenye sekta ya uzalishaji.

Mathalani Kila mkoa kukatwa na watu ishirini anayepata lapusam hiyo (kunawekwa mipango na taratibu sahihi zinazowahakikishia usalama wa fedha zao za uhakika wa faida)Kila mmoja akaenda kuwekeza kwenye kaeneo kake huko pengine akahitaji watu ishirini Kama wasaidizi na watendakazi wake tutakuwa na ajira mpya 400 kwa Kila mkoa kwa Kila mwaka.

Mfumo huu ukiendelea kwa wafanyibiashara na watu wengine wenye kipato tutakuwa tumeweka mfumo wa kusaidiana Sana.

Nafahamu yamekuwako mawazo ya kuwataka watu wapato fedha kwa mkupuo waziweke kwenye akaunti za malengo na dhamana mimi naona ni vema kuwekeza katika maeneo husika ili kuusisimia uchumi wa nchi na pia kutengeneza fursa.

Ni maoni yangu kwamba Kila mtu awaze Sana katika kutatua shida hii, mapendekezo haya ya kuibua na kuongeza idadi ya waajiri wapya Kila mwaka ni Moja TU kati njia nyingi tunazoweza kupendekeza.

Ahsanteni
 
Upvote 0
Back
Top Bottom