Uwekezaji wa bandari hauna shida kabisa

Uwekezaji wa bandari hauna shida kabisa

Rashda Zunde

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2022
Posts
204
Reaction score
231
Kwa yanayoendelea kuhusu uwekezaji wa bandari maoni yangu ni kwamba wasiwasi ndio akili lakini ndugu zangu Watanzania hakuna jambo baya linalofanyika au litakalofanyika.

Huu uwekezaji hauna shida kwani utakuwa na faida kadha wa kadha kwa nchi na sisi wananchi kwa ujumla.

Tutambue kwamba tusipokuwa na mwekezaji wa uhakika kama DP WORLD kwenye bandari yetu, SGR itajikuta inapaki kwa kukosa mizigo.

DP WORLD itasaidia kupunguza gharama ya usafirishaji wa shehena kutoka Dola za Marekani 12,000 hadi Dola za Marekani 6,000 au 7,000 kwa kontena linalokwenda Malawi, Zambia au DRC.

Ajira zitaongezeka kutoka 28,990 hadi 71,907 sawa na ongezeko la 148%.

Hivyo basi, uchumi utaimarika kama yalivyo malengo ya serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Tatizo watu wamechoka sana, iptl ilikuwa hivyohivyo, escrow ilikuwa hivyohiyo, gesi ya mtwara mkasema itareta nafuu maisha yawatanzania na mtauza mpaka nchi jilani yote ziro,hadi sasa gesi yakupikia wananchi hawamudu huku TFS wanabanana nawananchi kwenye mkaa, leo unasema wananchi watanufaika kwa mkataba wa bandari,wapi pametamka faida zitakazopatikana ktk mkataba huo? Kama nimakubaliano yaushirikiano wa nchi na nchi,kwanini yafanywe na bunge? bunge ilipaswa lisubiri mikataba itayoingiwa na makampuni yetu na ya dpw ili ipitie,ikibidi kushauri, nakama ikiwa namanufaa kwa nchi Bunge linaridhia na kuidhinisha,jambo jema namuhimu waitishe wanasheria wote wakae pamoja, wauchambue mkataba wote kifungu kwa kifungu na mjadara uwe wakitaifa uwe mubashara wachuane kwahoja mwisho watakubariana njia sahihi yakurekebisha, kama kuna watu hawataki kuelewa wenyenchi wanataka nini wao ndio wenye matatizo.
 
Kama kasuku, hizo asilimia umezitoa wapi?? Umepewa na DPW??

BTW kinachopigiwa kelele ni mkataba wa kijinga serikali imeingia. Na sio uwekezaji bandari.

Ingetangazwa tenda na DPW akashinda hakuna mtu angesema chochote.

Badala yake wamesaini ule upumbavu.
 
Tatizo watu wamechoka sana, iptl hivyohivyo mlisema escrow ilikuwa hivyohiyo gesi yamtwara mkasema itareta nafuu maisha yawatanzania na mtauza mpaka nchi jilani yote ziro,hadi sasa gesi yakupikia wananchi hawamudu huku TFS wanabanana nawananchi kwenye mkaa, leo unasema wananchi watanufaika kwa mkataba UPI uliotamka hayo? Kama nimakubariano kwanini iwe bunge? bunge ilipaswa lisubiri mikataba itayoingiwa na makampuni yetu na ya dpw ili ipitie nakupitisha, jambo jema namuhimu waitishe wanasheria wote wakae pamoja mjadara uwe wakitaifa uwe mubashara wachuane kwahoja mwisho watakubariana njia sahihi,,
Ipe heshima lugha ya taifa tafadhali.
 
Kwa yanayoendelea kuhusu uwekezaji wa bandari maoni yangu ni kwamba wasiwasi ndio akili lakini ndugu zangu Watanzania hakuna jambo baya linalofanyika au litakalofanyika.

Huu uwekezaji hauna shida kwani utakuwa na faida kadha wa kadha kwa nchi na sisi wananchi kwa ujumla.

Tutambue kwamba tusipokuwa na mwekezaji wa uhakika kama DP WORLD kwenye bandari yetu, SGR itajikuta inapaki kwa kukosa mizigo.

DP WORLD itasaidia kupunguza gharama ya usafirishaji wa shehena kutoka Dola za Marekani 12,000 hadi Dola za Marekani 6,000 au 7,000 kwa kontena linalokwenda Malawi, Zambia au DRC.

Ajira zitaongezeka kutoka 28,990 hadi 71,907 sawa na ongezeko la 148%.

Hivyo basi, uchumi utaimarika kama yalivyo malengo ya serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Fanya utafiti vizuri na hii ndio shida ya watanzania, uvivu wa kufikiri.
 
Acha ufinyu wa akili ndugu mwanachama.

Huo ufinyu wa mizigo utasababishwa na nini? Serikali inachukua watu wasio na ufanisi na kuwaweka hapo port unategemea nini?

Rushwa na ubadilifu na janja janja zimekithiri

Mkataba mama walioingia serikali na Dp world ni mkataba wenye ibara za ajabu sana, then unasema hakuna baya litakalotokea, kweli?

Naomba nijue elimu yako aiseeee, Kuweni na uchungu na hili taifa,

Kuweni na uzalendo kutoka ndani ya mioyo yenu na sio midomoni mwenu.

Nyie ndio mnafanya tuone tuliwahi sana kupata uhuru, kuna muda mtu unaweza kuwaza kuwa Baba wa taifa aliwahi kuzaliwa.
 
Tatizo watu wamechoka sana, iptl hivyohivyo mlisema escrow ilikuwa hivyohiyo gesi yamtwara mkasema itareta nafuu maisha yawatanzania na mtauza mpaka nchi jilani yote ziro,hadi sasa gesi yakupikia wananchi hawamudu huku TFS wanabanana nawananchi kwenye mkaa, leo unasema wananchi watanufaika kwa mkataba UPI uliotamka hayo? Kama nimakubariano kwanini iwe bunge? bunge ilipaswa lisubiri mikataba itayoingiwa na makampuni yetu na ya dpw ili ipitie nakupitisha, jambo jema namuhimu waitishe wanasheria wote wakae pamoja mjadara uwe wakitaifa uwe mubashara wachuane kwahoja mwisho watakubariana njia sahihi,,
Ungeandika tu kiinglish au hata kinyarwanda, tunaelewa kuliko kututia taabuni hivi
 
Licha ya kwamba hauna shida,sisi watanzania lazima tubadilike.Ushamba ni mwingi kiasi ambacho kwamba unakuta mtu anatoa mimacho na kashfa kwa kujifanya kutetea vizazi vijavyo.kwanza vizazi vipi ? mimi toka nina miaka miwili naaelezwa kuhusu kutunza rasilimali zetu kwa vizazi vijavyo,Sasa hivi nina miaka karibia 70 na kizazi kijacho bado hatujakifikia.Tengeneza vizuri sasa ili kizazi kilichopo kifaidi na kizazi kijacho kifaidi zaidi kwa sababu kitaboresha zaidi na hata teknologia itakuwa iko juu zaidi.
Sasa kwa sababu ya ushamba ,utakuta mtu anjiita wakili msomi huku amechooooka yaani yupo chali anatoka povu kukataa uwekezaji wa Bandari.Povu linamtoka na hasira,jazba huku akitweza hata utu wa binaaadam wenzake kwamba hata shetani aliyelaaniwa ana afadhali kuliko wao.Tunakwenda wapi jamani ? Hivi swala ni Bandari tu au kulikuwa na ajenda zilizofichika ?
Nduguzanguni watanzania,bila kuthubutu hatusogei hapa tulipo.Kuna nchi ndodgo ndogo kama Malta,ukitembelea kule utadhani ndiyo umeingia Peponi kwa jinsi tunavyosifiwa uzuri uliopo Peponi.Hawa walithubutu na wapo hapo walipo na bado hata wao wana vizazi vijavyo vitaboresha zaidi.
Mama,ukiona hawakuelewi,achana nao.Waachie libandari lao kwa sababu wanakutafutia visababu.Wacha wazidi kuibiwa na kupoteza wateja na hapo ndipo itakuwa burudani na starehe kwa hao wanaojiita mawakili wasomi.Wanatutajia mpaka vyuo walivyosoma huko Marekani ili tufanyeje ? Unaweza ukawa na mashahada kibao na bado ukawa akili huna za kutosha kutafakari mambo.
Tuache ushamba tubadilike,Na hata hawa wazee wa kimila nao waelimishwe waelewe kuwa dunia inaenda kasi na kuna kitu kinaitwa teknologia kikishakupita hata ukikimbiza hukipati asilan.
 
Back
Top Bottom