Uwekezaji wa nyumba za biashara unahitaji mipango ya muda mfupi na muda mrefu

Uwekezaji wa nyumba za biashara unahitaji mipango ya muda mfupi na muda mrefu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Mipango ya muda mrefu inahusu kufanya uwekezaji mkubwa. Tunaongelea nyumba zaidi ya 100 za kupangisha. Hii ni biashara watakayorithi watoto wako na wajukuu wako. Katika mipango hii nunua viwanja hata vikiwa mbali na mji, mji ukipanuka ardhi itaongezeka thamani.

Kwa wale waliopata kiinua mgongo wanataka nyumba ya kuongeza pension, ni bora ununue ardhi sehemu iliyochangamka. Ukinunua kiwanja cha milioni tano, utapata shida kupata mteja atakae lipa kodi yenye tija.

Rafiki yangu alifanikiwa kiweke milioni 60. Alinunua viwanja viwili pamoja maeneo yenye soko. Alipata milioni 60 nyungine akianza msingi wa maduka juu nyumba za kuishi. Baada ya hapo mambo yalikua mengi alikwama. Wafanya biashara walimuomba wao how mkataba wamalizie maduka walipane kwenye kodi. Kwakua sehemu Ina soko, alipata hata wa kumalizia flats zake juu.

Kuna dada mmoja kutoka Kenya aliniambia ardhi ni ng’ombe asiyekauka maziwa.
 
Ni kweli kabisa miaka kumi ijayo kiwanja ulichonunua leo kitakua na thamani zaidi.
 
Ni kweli kabisa miaka kumi ijayo kiwanja ulichonunua leo kitakua na thamani zaidi.
Kama una uwezo ukinunua viwanja vitatu leo, baada ya miaka kumi vitakuawa kwenye prime area na kama una staafu wakati huo unaweza kuongeza kipato na kodi ya wapangaji.
 
Mipango ya muda mrefu inahusu kufanya uwekezaji mkubwa. Tunaongelea nyumba zaidi ya 100 za kupangisha. Hii ni biashara watakayorithi watoto wako na wajukuu wako. Katika mipango hii nunua viwanja hata vikiwa mbali na mji, mji ukipanuka ardhi itaongezeka thamani.

Kwa wale waliopata kiinua mgongo wanataka nyumba ya kuongeza pension, ni bora ununue ardhi sehemu iliyochangamka. Ukinunua kiwanja cha milioni tano, utapata shida kupata mteja atakae lipa kodi yenye tija.

Rafiki yangu alifanikiwa kiweke milioni 60. Alinunua viwanja viwili pamoja maeneo yenye soko. Alipata milioni 60 nyungine akianza msingi wa maduka juu nyumba za kuishi. Baada ya hapo mambo yalikua mengi alikwama. Wafanya biashara walimuomba wao how mkataba wamalizie maduka walipane kwenye kodi. Kwakua sehemu Ina soko, alipata hata wa kumalizia flats zake juu.

Kuna dada mmoja kutoka Kenya aliniambia ardhi ni ng’ombe asiyekauka maziwa.
Mkuu yaani siyo tuu kuambiwa na huyo mdada, ardhi is everything!! Ukifanikiwa kujenga nyumba yako ya kuishi na kuachana na bugudha za wenye nyumba, the next good assert ni ardhi. Miaka ya mwanzoni mwa 1990's jamaa mmoja mji kasoro bahari alikuwa anatushawishi kwenda kununua mashamba kwenye vijiji huko Turiani, ambapo enzi hizo ukiwa na elfi 20 na kuwapa viongozi wa kijiji na wajumbe wao unakatiwa pori hata ekari 50. Siye jamaa tukawa tunamshangaa na kumuona mwehu tuu. Mwaka juzi nikabahatika hufika kwenye hivyo vijiji kikazi na kukaa kama wiki nzima. Ghafla nikakutana na yule jamaa yangu, akaniambia amekuja kukodisha mashamba yake na ana ekari Mia tatu. Huwa anakodisha ekari Mia mbili kwa wakulima wa Mahindi na Alizeti kila mwaka, ambapo kila ekari moja hulipwa elfu 50 na ekari anakodisha ni Mia mbili na hamsini na hizo hamsini analima mwenyewe. Amejenga nyumba kubwa shambani kaweka maji (kisima kirefu na matenki ya maji) umeme, mabanda kibao ya kuku, nguruwe na mbuzi, matrekta makubwa mawili, Fuso la mizigo, Toyota hilux double cabin na mazaga zaga kibao... Kiufupi jamaa yuko njema sanaa na hakuna mwaka anakosa wakodishaji kwa sababu ameweka vizuri sana miundombinu ya mashamba yake. Mkodishaji akitaka trekta la kulima, Lori za kubeba mazao, ghala la kutunza mazao vyote jamaa anavyo ila wanalipia...
 
Back
Top Bottom