Uwekezaji wa Rais Samia Katika Afya Waondoa Changamoto za Huduma za Kibingwa Handeni
Hapo zamani wakazi wa halmashauri ya wilaya ya Handeni na vijiji vyake walilazimika kwenda Tanga mjini hospitali ya Bombo au kwenda Muhimbili Daresalaam kwaajili ya huduma za kibingwa, lakini kwa uwekezaji uliofanywa na Rais Samia kwenye afya, shida hizo zimetatuliwa.
Hawa ni baadhi ya wakazi wilayani Handeni wakiizungumzia Hospitali ya Sheikh Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah iliyopo wilayani Handeni na namna ilivyotatua kero za kiafya wilayani humo.