DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Juzi niliona taarifa inaenea kwenye vyombo vya habari kuhusu Mkataba wa ujenzi wa viwanda Pwani.Katika muktadha wa mkataba huo wa uwekezaji unaotajwa kufikia thamani ya Dola za Marekani bilioni 7, ni muhimu kwa Serikali kueleza wazi iwapo ilifanya tathmini huru na ya kina (due diligence) kuhusu uwezo wa kifedha wa mhusika binafsi anayeingia katika makubaliano haya makubwa kwa niaba ya kampuni zake.
Kwa kuzingatia ukubwa wa mtaji unaotajwa, wananchi wana haki ya kufahamu kama tathmini hiyo ilihusisha uhakiki wa vyanzo vya fedha, rekodi za kifedha za kampuni husika, historia ya utekelezaji wa miradi mikubwa kama hii, pamoja na uwezo wake wa kutimiza ahadi za uwekezaji kwa wakati na kwa viwango vilivyokubaliwa. Uwazi katika hatua hii ni muhimu ili kuondoa mashaka iwapo mkataba huu umejikita kwenye uwezo halisi wa kifedha au ni makubaliano yanayotegemea ahadi za baadaye zisizo na dhamana ya kutosha.
Aidha, ufafanuzi wa Serikali unahitajika kuhusu taasisi au mamlaka gani za ndani zilihusika kufanya tathmini hiyo, vigezo gani vilitumika, na kama kulikuwa na ushirikishwaji wa wataalamu huru wa kifedha. Hili litasaidia kujenga imani ya umma kwamba Serikali inalinda maslahi ya Taifa na kuhakikisha kuwa uwekezaji unaosainiwa leo haugeuki kuwa mzigo wa kiuchumi, kisheria au kisera kwa Taifa katika siku zijazo.
Lakini jambo lingine muhimu, Serikali ieleze kama ilifanya tathmini ya hatari zinazotokana na vikwazo vya kiuchumi na kifedha vinavyoikabili Belarus, hususan kuhusu athari zake katika uhamishaji wa teknolojia, malipo ya kimataifa na utekelezaji wa mkataba huu, ili kuhakikisha kuwa maslahi ya Taifa hayapo hatarini.
Belarus imekuwa ikikumbana na vikwazo kutoka baadhi Mataifa jumuiya, ikiwemo Umoja wa Ulaya (EU), Marekani, Uingereza, Canada na washirika wao wa karibu. Vikwazo hivyo vinatokana na sababu mbalimbali ikiwemo ukiukwaji wa haki za binadamu na utawala wa Sheria.
Uwekezaji mkubwa ni fursa, lakini bila uwazi na uwajibikaji unaweza kuwa mzigo kwa Wananchi na vizazi vijavyo. Serikali ina wajibu wa kutoa ufafanuzi wa kina ili kuondoa hofu ya wananchi walio wengi ambao wamebakia katika sintofahamu.