Uwepo wa mafuta katika eneo ninaloishi

Uwepo wa mafuta katika eneo ninaloishi

Smart Technician

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2015
Posts
653
Reaction score
824
habari wajna jamii forum
naomba msaada kwa wale wataalamu wa geology na petroleum engineering .

katika eneo nililopo kwa sasa bondeni kidogo kuna chemchem na maji yanapotoka hutoka na kitu kama mafuta huelea juu ya maji nakufanya maji kua na layer juu ya rangi kama umemwaga mafuta
pia sehemu nyingine maji yanatoka yakiwa meusi hadi kufanya ardhi kua na weusi kama oil chafu imemwagwa

eneo lenyewe lipo bondeni chini hivyo nauliza yaweza kua ni mojawapo ya sababu ya uwepo wa mafuta ? ili nimtafute mtalam wa hii field
 
Hata mimi naona chemichemi inatoa maji kama hayo ngoja tusubirie majibu ila ukipata picha weka.
 
Watakaokujibu kiufasaha na mimi uniambie. Maana mimi mwenyewe kuna eneo la bondeni nalifahamu liko na features za hivo lakini sijawahi kuliwazia kama linaweza kuwna mafuta.
 
Hahaha yatakuwa mauchafu kutoka viwandani yaliyopitishwa kwenye mabomba ya chini (underground pipes) hakuna mafuta hapo labda yawe body line,baby care au ya alizeti hapo sawa
eneo nililopo hakuna kiwanda hata kimoja kiwanda kilicho jirani kipo kama kilometer 4 hivi nao wana mabwawa yao ya maji taka
 
eneo nililopo hakuna kiwanda hata kimoja kiwanda kilicho jirani kipo kama kilometer 4 hivi nao wana mabwawa yao ya maji taka
Hayo mabwawa ndo yanayo leta hayo maji yenye mafuta.
Yatakuwa yamecrack kwa chini..[emoji124] [emoji124] [emoji124]
 
Tafuta mwekezaji kimya kimya na uanze kuchimba myaki myaki mpaka waje kustukia ushakuwa bilionea.
 
Si mafuta basi fanya simple practice, chukua njiti na ki beriti washa.. yAkiwaka...

Chukua fursa... hali ilipofikia ni kuchuma na kutulia kutumia 2020
 
Mafuta ghafi kutoka chini ya ardhi (oil seepage) nijambo ambalo limetokea Mara kadhaa katika field tofauti tofauti dunian na hii hutokea pale mgandamizo katika reservoir inapokuwa kubwa na h ivyo kuperekea mwamba ambao huzuia mafuta/gas kutoka kwenye reservoir (cap rock/seal) kuelemewa na hivyo mafuta huanza kupenyeza taratibu kupitia kwenye nyufa za miamba mbalimbali mpaka kufika juu ya ardhi lakini pale mafuta yanapotokea haimanisha kwamba mafuta yanapatikana usawa huo , hii itategemeana na mweelekeo wa mipasuko ya miamba huenda ikawa several kilometers kutoka hapo yanapotokea

Labda mkuu ungeweza kutufahamisha exact location ya hiyo seepage inapotokea
 
Duh sheria zetu si rafiki sana.Unaweza kumiliki ardhi lakini kilicho chini ya ardhi sheria ina sema ni mali ya serekali atakuja mzungu hapo baada akienda wizarani utashangaa eneo lote linachukuliwa na serekali ukileta ubishi Mkuu wa Mkoa anakuleta FFFU wa kutosha unaondolewa eneo husika mara moja.
 
Back
Top Bottom