Uwepo wa Rev. Fr. Charles Kitima kwenye utiwaji saini wa Mkataba wa DP World unahitaji majibu

Daisam

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2016
Posts
2,625
Reaction score
3,141
Tumsifu Yesu Kristu.

Leo tarehe 22.10.2023 umehudhuria kikao cha utiaji saini HGA kwa ajili ya uendeshwaji na uendelezwaji wa Bandari ya Dar es Salaam.

Kwa kuwa wewe ndo uliyekuwa kinara wa kupinga uwekezaji wa DP World hapa Nchini, na leo umehudhuria kikao cha utiaji saini jambo lile lile ulilolipinga kwa nguvu zote, Waamini wa Kanisa Katoliki Tanzania tunaomba utoe ufafanuzi wa kina tena bila kupepesa macho kuhusu suala hili. Kama ufafanuzi wa kina hautatolewa haraka:-

(1) Binafsi sitatoa sadaka wala mchango wowote ule Kanisani, kwani sitakuwa tena na Imani na Kasisi yeyote yule. Lakini pia nitawashawishi na Waamini wengine kuchukua hatua nilizochukua.

(2) Nitajiuzuru nyadhifa zangu zote katika Kanisa na kuwashawishi wengine kufanya hivyo.

Tunaomba bila kupoteza muda mwingi jitokezeni kutoa maelezo ya kina.
 
Umemsikiliza rais?
1. Hujaona kuwa mkataba umerekebishwa na sasa una ukomo wa miaka 30?
2. Hukumbuki kuwa TEC ilipinga baadhi ya vipengele hasa mkataba kutokuwa na ukomo na sasa umerekebishwa?

3. Hujamsikia rais kuwa walilazimika kuwaingiza baadhi ya wadau kufanya majadiliano ya kurekebisha mkataba ni pamoja na TEC...LABDA?
 
Uzuri sikuizi Kilamtu kageuka kuwa mtumwa wa tumbo lake
Na huko tuendako watu wataanza kufiri kwa kutumia matumbo badala ya vichwa
 
Nilifikiri wote waliopaza sauti kupinga waliweka wazi kuwa hawapingi uwekezaji, bali vipengele katika mkataba. So kama kwa sasa vipengele vimemridhisha mhusika, sioni ubaya kwake kushirikiana nao. Mtazamo wangu.
Uko sahihi,
 
Kiini cha mtoa mada umekielewa au unaendekeza uchawa mbuzi??
 
TEC walisema mkataba ni mbovu ufutwe, hawakupinga vipengele tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…