Uwepo wa ukomo wa uongozi ni kigezo cha uwepo wa demokrasia?

Uwepo wa ukomo wa uongozi ni kigezo cha uwepo wa demokrasia?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Wakuu naomba kujuzwa. Uwepo wa ukomo wa uongozi ni kigezo muhimu cha uwepo wa demokrasia, au demokrasia haithiriki kitu bila uwepo wa ukomo wa uongozi?
 
Wakuu naomba kujuzwa. Uwepo wa ukomo wa uongozi ni kigezo muhimu cha uwepo wa demokrasia, au demokrasia haithiriki kitu bila uwepo wa ukomo wa uongozi?
Ukomo wa uongozi ni kitu muhimu katika demokrasia kwa sababu unatoa nafasi kwa watu tofauti na vizazi tofauti kuongoza. Baada ya muda fulani kiongozi mmoja anafikia "development fatigue" anakuwa hana mawazo mapya.

Pia, unapunguza uwezekano wa mtu mmoja kuhodhi madaraka na kujijengea ufalme. Zaidi unapunguza mianya ya rushwa na timu za upigaji kujijengea mizizi ya kuteka mifumo kwa kupitia kiongozi mmoja.

Ukomo wa uongozi unaongeza uwajibikaji kwa sababu kumuwajibisha kiongozi aliyekaa madarakani muda mrefu ni vigumu.
 
Wakuu naomba kujuzwa. Uwepo wa ukomo wa uongozi ni kigezo muhimu cha uwepo wa demokrasia, au demokrasia haithiriki kitu bila uwepo wa ukomo wa uongozi?
Nasikia Karia hana mpango wa kuachia ngazi...
Wadau "washazibwa mdomo" baada ya kupewa "kitu kidogo" Afrika n bala Giza Kila angle... Socially, economically and politically
 
Mangungu na yule msomali mwenzake aliyepo yanga wanapendekeza apitishwe bila kupiga kura.
Tenga aliacha mfumo mzuri Ila waliofata wanajali matumbo yao.
 
Back
Top Bottom