dosho12
JF-Expert Member
- May 6, 2023
- 596
- 1,475
UWEPO WA VITABU NA MAKALA KWA LUGHA YA KISWAHILI NA ONGEZEKO LA MAKTABA KATIKA KUKUZA MAENDELEO
Elimu ni ufunguo wa maisha ni kauli ambayo wote tumezoea kuisikia, ila unajua asilimia kubwa ya elimu inapatikana kwenye vitabu. Vitabu hubeba historia na mitazamo mbali mbali ya watu ulimwenguni lakini kama vikisomwa na kueleweka vizuri kwa lugha inayoeleweka vizuri katika jamii husika, na kwa Tanzania Kiswahili ndio lugha ambayo inaeleweka vizuri na jamii huku vitabu vingi vilivyopo nchini vinapatikana kwa lugha ya kigeni ambayo watu wengi hawana ujuzi nayo, hii inawapa ugumu watu kusoma na kuelewa vitabu. Vile vile maktaba vinazotunza vitabu kuwa chache na mbali kufikika kwa wananchi wanaoishi maeneo ya mbali na yasiyo na maktaba, hivyo husababisha wananchi kukosa elimu ipatikanayo kwenye vitabu ambayo itasaidia kwenye utawala bora na kukuza maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
Chanzo google
Kwa kuzingatia hoja hiyo tuangalia manufaa mbali mbali yapaatikanayo kama vitabu vikiandikwa au kutafasiriwa kwa lugha ya Kiswahili ili kila mtu aweze kupata ujumbe uliopo kwenye vitabu
FAIDA ZA VITABU KWA LUGHA YA KISWAHILI
1.Husaidia kuwa na ulewa mzuri wa lugha ya Kiswahili, kwa kujua misamiati, aina za maneno na kila kitu kinachohusiana na lugha fasaha kwa kuwa vitabu vitaandikwa kwa lugha iliyo fasaha kufikisha ujumbe hasa kwa wanaojifunza lugha ya Kiswahili.
2.Husaidia kutoa wandishi wazuri, ili taifa liwe na watu wenye ujuzi mzuri kwenye kuandika kwanza inabidi wasome vitabu na kuvielewa, hivyo kwa kuwa na vitabu kwa lugha ya Kiswahili itakuwa ni chachu ya watu kuwa na kiu ya kusoma na kupata maarifa yatakayowasaidia kuuwa wandishi wazuri wenye kusambaza elimu waliyonayo kwa njia ya maandishi.
3.Huhamasisha ufikiri chanya, vitabu hubeba mitazamo mbali mbali na historia tofauti za watu ambao waliweza kufanikisha katika safari zao ziwe ni za bishara, afya elimu au nyanja yoyote ile ya kijamii na kiuchumi, kwa namna hiyo historia zao zitawasaidia watu kwenye kutokata tamaa katika safari zao kwa kuwa na fikra chanya, badala ya sitaweza kuwa nitaweza kwa sababu kuna mtu alifanikiwa na mimi nitafanikiwa .
4.Huongeza uwezo wa kufanya maamuzi na kutatua matatizo, usomaji wa vitabu husaidia kuwa na uwezo wa kufikiri kimantiki hivyo hufanya mtu atoe mamuzi yaliyokuwa ya uhakika na kusadia kutatua matatizo yake na kusadia katika kukuza maendeleo.
5.Kuongeza shauku kwenye kutimiza malengo ya maendeleo, kwa kuangalia njia mbali mbali walizopitia watu na mitazamo yao na kufanya mtu asikate tamaa na kuwa na hamu ya kupata maendeleao na kupata mbinu mbali mbali.
6.Husaidia kuongeza idadi ya watu wanaosoma vitabu, kama tunavyojua idadi kubwa ya watanzania hawapendi kusoma vitabu ila huenda ikawa ni kwa sababu ya kuwa na lugha ya kingeni huku idadi kubwa ya wasioelewa na wasijua kabisa lugha ya kigeni ikiwa ni kubwa ila kama vitabu vitachapishwa na kutafasiriwa kwa lugha ya Kiswahili itasadia watu kupenda kusoma vitabu.
7. Kupata ujuzi na taarifa mpya,kwa kusoma vitabu kwa lugha ya Kiswahili watu wataweza kupata taarifa na ujuzi mpya kama vile kujua mbinu mpya za ujasiriamali, teknolojia, Sanaa na michezo ambazo itakuwa ni nyenzo ya kuwa na madaraka bora na kukuza uchumi wa Tanzania.
Hizo ni faida zinazopatikana kwa kusoma vitabu hasa vkiwa kwa lugha tunayoielewa vizuri lugha ya Kiswahili.sasa tuangalie faida za kuwa na maktaba nyingi na karibu.
Chanzo google
FAIDA ZA KUWA NA MAKTABA NYINGI NA RAHISI KUFIKIKA.
1.kuwa na uwezo mkubwa wa kutunza elimu na taarifa zipatikanazo kwenye vitabu, kwa kuwa maktaba zitakuwa nyingi
2.Kurahisisha ufikiaji na upatikanaji wa vitabu kwa wepesi, wananchi hawatapata tabu kupata elimu iliyopo kwenye vitabu
Hitimisho
Tumeangalia faida za vitabu vikiwa kwa lugha ya Kiswahili ambayo inatokana na mada inayozungumzia” uwepo wa vitabu na makala kwa lugha ya Kiswahili na ongezeko la maktaba katika kukuza maendeleo” pamoja na faida za wingi na ufikiaji rahisi wa maktaba.
Kwa maoni yangu nahisi serikali inaweza ikashughulikia na kundoa matatizo hayo na kufanya Tanzania kuwa na utawala bora na kupata maendeleo, nimejaribu kutengeneze njia za suluhisho ambazo serikari ningependa ishughulikie
1. Serikali isimamie na kutekeleza zoezi la utafsiri wa vitabu vya kigeni ili wananchi waweze kupata urahisi wa kusoma na kuelewa vitabu
2. Waandishi waandike vitabu na makala kwa lugha ya Kiswahili
3. Kuwa na vituo vya kutosha vya uchapaji wa vitabu na makala
Suluhisho la uwepo wa maktaba
1. Serikali ijenge angalau maktaba moja kila kata, hii itasaidia wananchi kutokuhangaika kwenda mbali, kwa sasa nahisi kila mkoa kuna maktaba moja na mikoa mingine hakuna maktaba kabisa
2. Maktaba zilizopo ziboreshwe na kujazwa vitabu vya kutosha,kwa maktaba zilizopo serikali iboreshe na kuongeza vitabu vya kila aina ili wananchi wasipate tabu kwenye kutafuta elimu
Kama serikali ikifanya hivyo kutakuwa na wananchi walio na elimu na uelewa wa kufikiri na kufanya mamuzi na kutatua matatazo yao na kusaidia kuwa na utawa bora na kusaidia kwenye kukuza maendeleo ya kiuchumi, kijamii na nyanja zote za maendeleo

Upvote
3