Uwezekano wa Barcelona kufungiwa kushiriki Kombe la Mabigwa Ulaya (UEFA)

fyddell

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2011
Posts
12,026
Reaction score
22,549
Chama cha Mpira barani Ulaya UEFA, inaichunguza timu ya Barcelona juu ya madai ya kuilipa kampuni ya Jose Mara Enriquez Negreira ambaye ni Makamu wa Raisi mstaafu wa chama cha marefa Hispania.

Nyaraka za mahakama zinaonesha kuwa, Barcelona imelipa kiasi cha €7.3m ambayo ni sawa na paundi 6.5m kuanzia mwana 2001 mpaka 2018 kwa kampuni hiyo.

Uchunguzi huu ukikamilika inaweza kupelekea Barcelona kufungiwa kujihusha na mashindano yote yanayoandaliwa na UEFA.

Uchunguzi huu umeombwa na bodi ya uongozi UEFA na mpaka kufikia sasa uchunguzi huu umeshaanza kufanywa na waendesha mashtaka wa nchini Hispania.

Source: Sky Sports

images (7).jpeg

Huu ni ugomvi wa kisiasa kati ya Rais wa la Liga Javier Tebas na Joan Laporta Rais 2a Barcelona.

Tokea Laporta awe rais wa Barca mwaka 2021 na tokea Laporta awe na msuguano na Tebas kuhusiana na superleague na mkataba wa CVC

Tebas alitaka vilabu vyote Hispania waingie mkataba na CVC na mkataba wa CVC una kipengele cha kutokubali superleague

Laporta amekuwa mstari wa mbele kuikataa CVC na kuhamasisha superleague tokea hapo Tebas amekuwa na malumbano na Laporta na Barcelona na amekuwa na stance ngumu kwa Barcelona kwenye maamuzi mengi tokea
2021 Hadi sasa

Juzi Tebas anasema jambo jema kwa chama cha soka Spain ni kumuondoa Laporta Barcelona?sababu
Kubwa ni msuguano wa superleague kadhihirisha chuki zake wazi

KESI YA NEGREIRA

NEGREIRA alikuwa makamu rais wa chama cha marefa Spain.Negreira ana
Kampuni yake inayojihusisha na uchambuzi wa maamuzi uwanjani na makosa ya wachezaji ni kama vile kipindi Cha kipenga Cha Azam..

Sasa Barcelona waliingia mkataba na
Kampuni ya NEGREIRA Ili kuwapa technical report ya makosa na masuala mengine ya uwanjani na ushauri nk

Mahakama ya Spain inasema ktk uchunguzi wao hawajakuta rushwa yeyote Kwa marefa

-Hawajakuta uthibitisho wa malipo kwa refarii yeyote yule

-kipindi Cha malipo NEGREIRA hakuwa refarii

-hakuna uthibitisho kwamba malipo kwenye kampuni hio ya uchambuzi yaliweza kuathiri matokeo

Javier Tebas ndiye aliyepeleka KESI hii mahakama ya Spain ,na ndiye ameipeleka
UEFA na akifeli amesema ataipeleka fifa

Tebas ana chuki na Laporta na yote hayo ni
Sababu ya Laporta na superleague na sababu zinginezo
Hadi anasema anataka Laporta aondoshwe

1679601523673.jpg
 
Barcelona na acmilan Nesta alimsukuma Messi kabla kona haijapigwa refa akatoa penati , pamoja na ubora wa Barcelona kuna baadhhi ya matukio yalikuwa yanaacha maswali
 
Huu ni ugomvi wa kisiasa kati ya Rais wa la Liga Javier Tebas na Joan Laporta Rais 2a Barcelona...
Babu, Barcelona walikua wakibebwa iko wazi na kila mtu alikua akilalama,dhidi ya Chelsea Hadi drogba akataka kumpiga refa, kadi ya pili ya njano ya van persie katika game ambayo Barcelona alikua kapigwa mbili Emirates na unamjua van persie,final 2006 hata refa mwenyewe alikiri kufanya makosa
 
Nakumbuka ilikuwa 2016-17 UEFA ile PSG wakiongoza kwa goli 4 second leg hatua ya 16 bora mwishoni mabao ya jumla yakawa 6-5[emoji1787][emoji119]
Sasa kwenye like game walipendelewa NINI ??! Tuanze hapo
 
Babu, Barcelona walikua wakibebwa iko wazi na kila mtu alikua akilalama,dhidi ya Chelsea Hadi drogba akataka kumpiga refa, kadi ya pili ya njano ya van persie katika game ambayo Barcelona alikua kapigwa mbili Emirates na unamjua van persie,final 2006 hata refa mwenyewe alikiri kufanya makosa
KESI yenyewe unafahamu inahusiana
Na nn?

NEGREIRA alikuwa la Liga na hii KESI ni kati ya la Liga na Barcelona na sio UEFA sababu hakuna refa wa kispain anayeweza kuchezesha timu za taifa lake UEFA..

Haihusiani na michuano ya UEFA KESI
Hii ya NEGREIRA sawa.
 
Connection matters
 
Huu ni ugomvi wa kisiasa kati ya Rais wa la Liga Javier Tebas na Joan Laporta Rais 2a Barcelona.

Tokea Laporta awe rais wa Barca mwaka 2021 na tokea Laporta awe na msuguano na Tebas kuhusiana na superleague na mkataba wa CVC

Tebas alitaka vilabu vyote Hispania waingie mkataba na CVC na mkataba wa CVC una kipengele cha kutokubali superleague

Laporta amekuwa mstari wa mbele kuikataa CVC na kuhamasisha superleague tokea hapo Tebas amekuwa na malumbano na Laporta na Barcelona na amekuwa na stance ngumu kwa Barcelona kwenye maamuzi mengi tokea
2021 Hadi sasa

Juzi Tebas anasema jambo jema kwa chama cha soka Spain ni kumuondoa Laporta Barcelona?sababu
Kubwa ni msuguano wa superleague kadhihirisha chuki zake wazi

KESI YA NEGREIRA

NEGREIRA alikuwa makamu rais wa chama cha marefa Spain.Negreira ana
Kampuni yake inayojihusisha na uchambuzi wa maamuzi uwanjani na makosa ya wachezaji ni kama vile kipindi Cha kipenga Cha Azam..

Sasa Barcelona waliingia mkataba na
Kampuni ya NEGREIRA Ili kuwapa technical report ya makosa na masuala mengine ya uwanjani na ushauri nk

Mahakama ya Spain inasema ktk uchunguzi wao hawajakuta rushwa yeyote Kwa marefa

-Hawajakuta uthibitisho wa malipo kwa refarii yeyote yule

-kipindi Cha malipo NEGREIRA hakuwa refarii

-hakuna uthibitisho kwamba malipo kwenye kampuni hio ya uchambuzi yaliweza kuathiri matokeo

Javier Tebas ndiye aliyepeleka KESI hii mahakama ya Spain ,na ndiye ameipeleka
UEFA na akifeli amesema ataipeleka fifa

Tebas ana chuki na Laporta na yote hayo ni
Sababu ya Laporta na superleague na sababu zinginezo
Hadi anasema anataka Laporta aondoshwe

View attachment 2563326
Umeeleza vizuri SANA SANA na huu ndo uchambuzi
 
Back
Top Bottom