Uwezekano wa Magufuli kuongoza nchi kwa kipindi cha pili haupo

Yupo vipindi vyote, akikaribia kumaliza kipindi cha mwisho wewe mwenyewe utarudi kuomba katiba ibadirike aongeze kipindi kingine cha tatu
 
Kuna wakati akili za mizimu nda akili sahihi zaidi kutumika kwa wakati huo, ukijifanya sober muda mwingine unapotea kijasiri bila mwenyewe kujua kama unapotea. Wacha movie iendelee
 
For what I know ,move ya lowasa ni strategic, Rostam is behind all the plan
 
Baabba Mmungu tunakuomba...
Hawa waattu ni wamelaaniwa na kuamua kumtumikia shetani...
Katika Jiinnaa la Yyessu Wasshhiindwe!.
P
Baaaabbababa "Mungu" wetu wa Tanzania, Africa na dunia kwa ujumla, bila kusahau Chatototo yetu, tunaomba uturudishie Ben, Azory, uruhusu demokrasia, uruhusu bunge live, ukemee utekaji, utupe nyongeza zetu makazini , Lisu asipigwe risasi tena. Hawa watu wanaokupinga washindwe kwa jina la Yesu ukisha warudisha hao niliowataja.
Kwa jina la Yesu AMEEN!
 
Baabba Mmungu tunakuomba...
Hawa waattu ni wamelaaniwa na kuamua kumtumikia shetani...
Katika Jiinnaa la Yyessu Wasshhiindwe!.
P
Umemalizana na Acacia? karibu tena kwenye siasa halisi, eti yule mtu wetu wanampigia tena chapuo kwanini humshauri akachunge ng'ombe kama alivyoahidi.
 
Nimepata mwanga kuhusu baadhi ya wanasiasa wa ccm wasiotarajiwa kujitokeza hadharani kuegemea upande mmoja kwenye sakata hili la waraka wa wastaafu wakati wengine wametulia wanatazama tu!
 
Wanaojua mzizi wa haya yanayoendelea ni wachache sana.

Hamjiulizi kwanini jiwe mpaka sasa kigugumizi? Hujuma anazofanyiwa ni reaction ya kitendo cha jiwe kujipeleka kwenye kambi ya Lowassa.

Hope hilo swali huwaulizi washambuliaji wa Uzi huu ambao hata wewe unaona wazo kuwa wako hapa siyo kwa madhumuni kushiriki mjadala kwa hoja bali kushambulia na kutisha!
 
Niliwahi kusema kuwa kile kitendo cha kumrudisha Lowassa chamani na kumrudisha Rostam Aziz nchini ni cha kuangalia kwa jicho la tatu!!!

Nimepata kumsikiliza Mzee mmoja mstaafu wa nchi hii akizungumza kwenye jukwaani moja la uongozi nje ya nchi. Aliwalaumu sana viongozi wa Afrika kwa ubinafsi uliopitiliza! Ndio haya ya kuwavuta na kuwakumbatia baadhi ya watu kwa maslahi binafsi ya kisiasa badala ya maslahi ya nchi.
 
Umemalizana na Acacia? karibu tena kwenye siasa halisi, eti yule mtu wetu wanampigia tena chapuo kwanini humshauri akachunge ng'ombe kama alivyoahidi.
Vitu vingine ni ndoto tuu za mchana, unaamua usichangie ili tuu kuheshimu mawazo ya watu. Utaratibu wa CCM kuhusu the incumbent president unajulikana, who would dare do anything?. Kinana, Makamba,Membe, Nape na January they are history!, they are things of the past, kama yalivyo ...ya jana, hayanuki!. Hakuna mtu CCM alikuwa na nguvu na wafuasi kama Lowassa, alipoondoka, aliondoka peke yake na watu wake wachache na hakukimega chama, hivyo wengine wote they are almost nothing.
P
 

Umechambua vema ila umeweka chumvi hadi kusahau Mpendwa wetu lowasa(kulingana na clip ya harusi ya mwanae) ni mgonjwa, naamini hataweza kugombea tena bali atampa saport magu.
 
Unachokisema kiongozi ni dhahiri kipo. Watu hawajui kuwa viongozi kama Lowassa na Rostam wana historia yenye ukakasi kidogo kama tulivyoaminishwa na wahusika. Wao kubadilika ghafla na kuwa wazuri,ni jambo la kushtua. Kuna mengi yapo njiani. Tukae hapa hapa "stendi"yatatukuta!!!πŸ‘ŠπŸΏπŸ‘ŠπŸΏπŸ‘ŠπŸΏ
 
Duh! Wewe ndio umechemka kabisa kumleta Ngoyai kwenye equation. Mtu ambaye yuko 'ICU' anawezaje kweli kugombea Urais?
Labda hujaona clipp yake ya hivi karibuni... Ngoyai keshajichokea. The best for him now ni kujiandaa kiroho kwa safari inayofuata...
Hoja yako haina mashiko.Hatakuwa wa kwanza.
Aliyekua rais wa Algeria amegombea misimu miwili akiwa mgonjwa taabani.
 
Chakuzingatia tu, wakati huo (2020) kuna uwezekano baadhi ya watu hatutakuwa nao, kimwili au kisiasa, akiwemo Magufuli mwenyewe


Hiyo imenitisha!! kah!
 
Mkuu hizo ni ndoto za Alinacha za mchana kweupe rais ataongoza awamu ya 2 na kwa atakayofanya tutatammani tumuongeze mda tutampa miaka mingine 20 jmla iwe 20 rais gani ukiacha nyerere alifanya mambo makubwa kama haya?? Alofanya Magufuri??
Kafanya nini kikubwa sana ambacho kimetowa matunda kwa taifa?inaonekana wewe ni mshabiki Wa chama tu au umri wako Mdogo au uwezo wako Wa hisoria ya nchi huijui vizuri wewe tafadhali usiwabeze marais waliopita unamsifia huyo kwa vile amekuta waliomtangulia wamemsafishia njia mfano Mdogo kwenye udhibiti Wa bandari ingekuwa hajakuta tayari imeshatengenezwa system kubwa ya TANCIS angedhibitije kwa system ya zamani ya Asycuda +unakumbuka mtwara kusafiri kwa basi ilikuwa ngumu?je unajuwa bwawa la lihasi lilijengwa awamu ipi?unajuwa Tanzania barabara zilikuwa chache na mikoa michache?unajuwa nyerere aliacha megawati ngapi za umeme? Na rais huyu amekuta nchi ina mgwatts ngapi?usiwabeze waliopita wewe kwanza huenda wewe umesoma shule za kata ambazo nijuhudi za marais waliopita tuulize sisi tuliokuwepo awamu zote za nchi hii usinge sifiya uongizi Wa nyerere tumevaa kaptula zenye viraka viraka tumetembea peku shule nzima hakuna mwanafunzi anayevaa viatu 'kama upenda kusifu sifu lakini usimdhau baba au mlezi aliyekule mpaka ukapata digree uliyonayo
 
Huwa nacheka sana kila napomaliza kusoma habari za wanoandika Mh.Membe kugombea, pengine kupita na kama hizi za mtoa hoja..Mimi kwa kuitazama siasa ya Tanzania nilibaini kuwa CCM inapokuwa na migogoro tayari vyama vya upinzani huwa havina nguvu na matayarisho kwa ajili ya uchaguzi isipokuwa tu ujanja aliofanya Mh.Mbowe 2015 japo kuna watu walimbeza bila kujua nini maana ya Tactics. Mimi kitu nachokiona hapa katika kuelekea uchaguzi wananchi wapo njia panda katika mfumo wa kujiuliza nani atapitishwa..automatically wanakuwa wanajiandaa kuipigia kura CCM maana atakayepita kura ya maoni wanamchukulia kuwa ana uwezo na hakuna jinsi ya kumzuia..hivyo basi kwa kuwa kura ni siri watu humpigia kura mgombea urais CCM. Sababu kuu ni kwamba amepita ndani ya CCM huyu ni mwamba, pili wasiwasi kuwa vyama vingine vya siasa havijaonesha kuwa vina mwamba kwa ajili ya uchaguzi ujao au mwamba wao ameyumbishwa kisiasa.
Hoja ya eti kuna mpasuko wenye kundi la JK na kundi la Lowassa hii hutokana mtazamo wa siasa tu ndani ya CCM ambao mwisho wa siku halmashauri kuu humaliza hii hali na wanachama wa CCM hufikia makubaliano (rejea chaguzi zote tangu1995).
Watu wanajichanganya wanashindwa kubaini kuwa kama Mh.Magufuli hana kundi lenye nguvu basi ana watu watiifu wenye weledi na wanaoelewa nini maana ya kuwa mwenyekiti wa chama..pengine wapo katika kila kundi ila wanaamini katika mfumo wa CCM kupata mtu sahihi,yani wakiona huku kachukua fomu mtu fulani basi wakati wa kumpata mgombea wanajikuta wote wanaona bora huyu asiye na kundi kubwa ili nasi kundi letu tubaki salama.Makundi haya hutokana na tofauti za kiitikadi na huwa hayawezi kuwa na nguvu kuliko CCM.
Mimi binafsi naona nafasi ya Mh.Magufuli bado ni kubwa kugombea 2020 labda kama atakataa mwenyewe maana kuongoza Taifa hili yataka "Moyo wa Ujasiri na Uvumilivu".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…