Uwezekano wa Magufuli kuongoza nchi kwa kipindi cha pili haupo

Haya yanakwenda kutimia, Mungu saidia kwa kuweka mkono wako.AMINA
 
Mbingu zimewakataa zilianza kwa bashite nae ajira yake inakoma rasmi October, watz si watu wa visasi kwa yote aliyowaumizia ataishi kwa furaha na amani. Muhimu tu apumzike kwa amani October asituumize Tena 5 yrs
 
Haupo...kulazimisha asije akawaponza NEC bure!!
 
Kosa kubwa walilofanya CCM ndani ya miaka 5 ni kujikita kununua madiwani na wabunge wakifikiri ndiyo njia pekee ya kuua upinzani.

Kosa lingine la kiufundi ilikuwa kuwazuia wapinzani wasiongee kwa miaka 5 mfululizo.

Sijui ni nani aliwashauri mbinu hizi za karne ya 18. Sasa majibu wameyapata toka kwa watanzania.

Bechi la ufundi ongezeni wasanii zaidi....kwenye safari za Mzee baba
 
Sidhani kama Umefanya Tathimini ya Awamu ya 5 na Vitu ilivyovifanya Ambavyo vimegusa Mwananchi mdogo kabisa. Ambao katika Awamu iliyopita walisahauliwa kabisa na kuishi kama wakimbizi kwenye Nchi yao.

Sisemi kwamba Rais wa Awamu ya 4 hakufanya kitu lahasha ila wasaidizi wake walimwangusha sana.

Tangu Alipokuja Ndugu Magufuli Amedhibiti nidhamu serikalini.. Amedhibiti uchezewaji wa PESA za serikali. Ameondoa wafanyakazi hewa Ambao walikua wanatafuna mabilioni ya walipa kodi na kupelekea Miradi mingi kushindwa kutekelezeka.

Amewekeza kwenye miradi mingi mikubwa Ambayo Impact yake itakuja kuwa kubwa sana kwa Taifa hili.

Sasa najua Baadhi ya watu wenye mawazo mgando wata beza na kushikilia hoja dhaifu kwamba hali ya Uchumi wa wananchi ni Mbaya.

Hapa naomba niseme. Wazi taifa hili watu wengi walikua hawajishugulishi na walikua Mission town na udalali. Sasa fedha zilizokua zinatakatishwa mitaani hamna kila Mbuzi Atakula kwa urefu wa namba YAKE.

Kama hufanyi kazi utalalamika na utakufa njaa Brother. Magufuli atachaguliwa na Atashinda kwa kishindo. Hakuna mbadala wake kwa taifa hiki tena Tutamwongezea miaka 10 mingine Atusogeze Mbele kwa kasi zaidi.
 
Na Anderson Ndambo.

Kuna mambo yanahitaji jicho la Tatu kuyaona na pengine kuyaamini. Tabia mojawapo ya siasa ni kubadilika badilika kulingana na majira na wakati kutokana na sababu za wakati husika, lakini kwa Tanzania mabadiliko haya yamekuwa na kasi kubwa mno, hicho si kitu cha kawaida, kama ambavyo Magufuli mwenyewe hakutegemea kuukwaa Urais wa Tanzania kwa kuchaguliwa kuwa mgombea wa ccm, vilevile mazingira kama yale yanaweza kubadilisha hali ya mambo na matokeo yakawa tofauti na tunavyodhani kuelekea 2020.

Rais Jakaya Kikwete aliingia madarakani kutokana na kuimarika kwa kundi lenye nguvu lililokuwa likiongozwa na Lowassa ndani ya ccm, na kwa wakati huo ndio lilikuwa kundi lenye nguvu ndani ya chama hicho (ccm) lililoweza kudhihirika na kuweza kutoa ushawishi na kulazimisha Kikwete kuingia madarakani na kundi hilo likamkaanga vikali, Salim na kumtowesha kabisa kwenye ulingo wa siasa za kitaifa ndani ya ccm na nchi kwa ujumla. Kundi hili lilianza kujijenga tangu wakati Nyerere akiwa madarakani na kimsingi lilikomaa sana wakati wa Mkapa kiasi kwamba Mkapa akashindwa kulidhibiti.

Mwaka 2015, kundi hili lilifikia hatua ya mwisho na ya juu kabisa ya kupasuka kwakwe, baada ya Kikwete ambae ni sehemu ya zao la kundi hilo kujichomoa na kumsaliti king mwenzie (Lowassa) na kutengeneza kundi jipya ndani ya ccm. Kutokana na nguvu ya Lowassa wakati ule ccm ambayo ilitokana na kundi lake la asili, kundi la Kikwete lilikuwa na wakati mgumu sana, kwasababu lilikuwa halina ukubwa na ushawishi mkubwa kama kundi ambalo kikwete amelisaliti isipokuwa tu kutokana na Ushawishi wake Kikwete kama Rais na mjumbe mzoefu alie asi na baadhi ya wajumbe wake na wote tunafahamu shughuli waliokuwa nayo walipo mkata Lowassa.

Sasa Magufuli amezaliwa kutokana na Kundi kubwa ndani ya ccm kuvunjika kwa kusalitiana na kwa bahati mbaya sana, makundi haya yote yalijikuta yako tena kwenye uwanja mmoja (ulingo wa siasa (ccm), na katikati yupo Magufuli. Kundi la Kikwete kwa sasa lina nguvu kubwa kutokana uwekezaji mkubwa wa kikwete ndani ya serikali na ccm, lakini kundi la Lowassa ni kubwa kutokana na uzito wa wajumbe wake ndani ya ccm na ushawishi wao kwa Rais magufuli. Vita inapamba moto. Na makundi yote haya mawili kwanza hayakubaliani, lakini kubwa zaidi haya mkubali Magufuli kwasababu mwenendo wa magufjli una athari zinazo fanana kwa makundi yote na timu yake. Kundi la lowassa linatumia fursa tu, na tusisahau Ndoto ya Lowassa kuongoza nchi haijafa.

Rais magufuli anadhani yuko salama, kwasababu kuna vita ya ziada kwa makundi haya mawili, anadhani kuliimarisha kundi la Lowassa kutamsaidia yeye kupita kiulaini 2020 kwasababu ya mvutano mkali utakaozidi kuimarika baina ya makundi haya mawili ambayo tayari vita hiyo imeanza kujidhihirisha hadharani baada ya matamshi ya Bashe yenye dhana ya kisasi dhidi ya watu wa kundi la Kikwete. Kitendo hiki kimemshawishi sana magufuli kwamba ataweza kuvuka kiulaini sana. Na hili linaonesha kupata mafanikio kwasababu kundi la lowassa sio tu linapewa nyadhifa sasa na magufuli bali, limeanza kuinunua vita ya magufuli na wakina musiba wanaanza kutoweka kiana.

Kinachokwenda kutokea..

1. Kwanza tuelewe, makundi haya yote yana ushawishi mkubwa ndani ya ccm kuliko magufuli mwenyewe.

2. Makundi haya yana ushawishi mkubwa ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama kuliko magufuli mwenyewe.

3. Magufuli sio tu, hana ushawishi mkubwa kwenye vyombo vya usalama kuliko mahasimu wake, Bali hata ndani ya ccm na hata kwenye nchi (Taifa) maana watu wamemchoka kabisa, kweli Raia tumemchoka kabisa.

4. Magufuli amenza kuunda chama chake kipya ndani ya ccm (ccm mpya), inayobebwa na kundi la watu ambao hawana ushawishi wowote ndani ya ccm, hawana uzoefu wa kutosha wa kuongoza nchi, hawana mizizi mirefu ndani ya siasa za ccm, kimsingi watu hawa ni wanasiasa kwenye taswira ya magufuli (magufulisim).

Sasa, mwisho wa kukomaa kwa vita hii kubwa ya mafahari wawili, itapelekea nchi kuwa kwenye hali mbaya zaidi kiuchumi, kisiasa na kijamii. Jamii itazidi kuyajua maovu mengi yaliofichwa dhidi ya ccm, bila kujali ni ccm asilia au mpya au nani, na kimsingi jamii itakuwa imejaa chuki kubwa dhidi ya ccm yote, bila kujali huyu anatoka kundi gani, kwasababu wote hawa nje ya ccm wanajulakana kama ni ccm tu. Magufuli hatokuwa kwenye nafasi ya kufanya mambo mapya, kwasababu ya mtifuano huu na mtifuano huu ndio utakao chukua nafasi kubwa zaidi kuelekea 2020 kwenye masikio ya watu na si magfuli, kimsingi magufuli atakpjikuta anafika 2020 akiwa anachukiwa kuliko mwanzo.

Itakapofikia hapo, wakati wa kufanya maamuzi ya nani anapaswa kuivusha ccm, itategemea mshindi wa kati ya makundi haya mawili, lile la Kikwete na lile la Lowassa, na kimsingi, vyombo vya dola na usalama vitakuwa kwenye nafasi kubwa ya ushawishi ndani ya nchi na ccm yenyewe kuliko wakati wowote ule, na jamii itakuwa ikiamini zaidi kwa wapinzani, hapa ndipo maamuzi ya ama magufuli au mwingine ndani ya ccm atapaswa kuwekwa kama mgombea yanaweza sio tu kufanyika na ccm wenyewe, pengine Jeshi la nchi, na kwa vyovyote vile, jeshi la nchii kwa sisi wachambuzi wa mambo haliwezi kumruhusu magufuli kuendelea na awamu ya pili. Chakuzingatia tu, wakati huo (2020) kuna uwezekano baadhi ya watu hatutakuwa nao, kimwili au kisiasa, akiwemo Magufuli mwenyewe. Hapa ndipo namuona Lowassa akiibuka tena.

Watu wanaosema, ccm imekuwa ikifikia hatua kubwa ya mpasuko, na huweza kujinasua upya, wanasahau wakati huo, kulikuwa na kundi moja, na baadae likaongezeka hili la pili ambalo limejengeka kwenye msingi wa visasi, na sasa tuna makundi mawili yenye nguvu yasiokuwa tayari kupatana na kukaa meza moja, kitu ambacho hakijawai kutokea huko nyuma.

Hichi kinacho onekana Lowassa na Rostam kumuunga mkono Magufuli si kitu cha kufuraia sana, usishangae 2020 mgombe wa ccm akawa Edward Lowassa na sio Magufuli tunae dhani ndie. Mwelekeo wa mambo wa sasa unabadilika kwa kasi kubwa sana, na kuna kila dalili za ccm kufikia tamati, ijapokuwa kweye mazingira tata sana. Lowassa ni mzuri sana kwenye kuficha na kulinda hadhi yake yeye binafsi. Mwaka 2015 kuna utafiti ulionesha ndie amgombea pekee aliekuwa na ushawishi mkubwa kuliko wanasiasa wengine kwa tofauti ya asilimia 11 akifuatiwa na Dr. Slaa. Huu ni ushawishi binafsi bila chama. Na kimsingi anajua jinsi ya kuwatumia wengine, na ana watu wenye weledi mkubwa kwenye kumlinda tofauti na magufuli anaetetewa na vichaa kama musiba.

Naendelea kutoa ushauri kwa vijana wa ccm, kujaribu kuchagua upande sahihi mapema na sio kukesha kupyauka, leo unamtukana huyu, kesho unamtukana yule, mwisho unajikuta unatakiwa kumsifia mtu uliemtukana jana, utasimamaje? Vijana muwe wenye hekima sana, na pengine mjitaidi kunyamaza kimya, unaedhani ana nguvu leo, kesho unaweza kumkuta ni laini kama siagi......kuni zinawaka moto sana....

A. Ndambo
Maneno mengi yasiyo na faida

Mi hua nawaelewa ninyi,nyote ninyi mnaomponda JPM ni watu wa makundi matatu makubwa

1. Vyeti feki

2. Wala rushwa (fisadi) mliobanwa msituibie wananchi

3. Wenye uchu wa madaraka kutafuta pesa na heshima

Sisi wananchi 85% kama si 90% tunamuelewa sana JPM na anatutendea vyema

Acheni kuja na maneno elfu saba mia3 ishirini na4 hayatusaidii..tendeni haki ktk idara zenu na kama mlifukuzwa mkome,nendeni Tabora huko au Rukwa bado kuna ardhi kubwa sana ya kulima
 
Nipo uswaz huku siasa Sina mda nayo Sana but mie KM NAONA USHINDAN HAMNA VILE MAGU KAPITA NA TULIA HUKU KWETU KAPITA

SIJUI HUMU JF WATU MNAJIPA MOYO GANI ILA NAONA KAMA LISSU HANA NGUVU KIVILE

MUDA UTAONGEA
 
[emoji2][emoji2]Tena bila kupingwa
Jf iko tofauti sana na maisha halisi ukiwa humu utadhani Tz imesimama
Nipo uswaz huku siasa Sina mda nayo Sana but mie KM NAONA USHINDAN HAMNA VILE MAGU KAPITA NA TULIA HUKU KWETU KAPITA

SIJUI HUMU JF WATU MNAJIPA MOYO GANI ILA NAONA KAMA LISSU HANA NGUVU KIVILE

MUDA UTAONGEA
 
DAY DREAM PLUS DOUBLE KICK SPIRITY
Herode
Mzee wa Mifadhaiko alipoona mhanga wa Risasi ni mzima yuko Nairobi akatuma watu(kina Samia)
Mhanga yule akarudi, wakaanza kuweweseka, imekuwaje risasi 16 zishindwe wakati 3 huwa zinamaliza kila kitu?
 
Mtoa post naomba unipe sifa tano za kiongozi bora ili tujue Kati ya lisu na magufuli nani tumpe kura oct 28/2020
Nasubir majibu
 
Na Anderson Ndambo.

Kuna mambo yanahitaji jicho la Tatu kuyaona na pengine kuyaamini. Tabia mojawapo ya siasa ni kubadilika badilika kulingana na majira na wakati kutokana na sababu za wakati husika, lakini kwa Tanzania mabadiliko haya yamekuwa na kasi kubwa mno, hicho si kitu cha kawaida, kama ambavyo Magufuli mwenyewe hakutegemea kuukwaa Urais wa Tanzania kwa kuchaguliwa kuwa mgombea wa ccm, vilevile mazingira kama yale yanaweza kubadilisha hali ya mambo na matokeo yakawa tofauti na tunavyodhani kuelekea 2020.

Rais Jakaya Kikwete aliingia madarakani kutokana na kuimarika kwa kundi lenye nguvu lililokuwa likiongozwa na Lowassa ndani ya ccm, na kwa wakati huo ndio lilikuwa kundi lenye nguvu ndani ya chama hicho (ccm) lililoweza kudhihirika na kuweza kutoa ushawishi na kulazimisha Kikwete kuingia madarakani na kundi hilo likamkaanga vikali, Salim na kumtowesha kabisa kwenye ulingo wa siasa za kitaifa ndani ya ccm na nchi kwa ujumla. Kundi hili lilianza kujijenga tangu wakati Nyerere akiwa madarakani na kimsingi lilikomaa sana wakati wa Mkapa kiasi kwamba Mkapa akashindwa kulidhibiti.

Mwaka 2015, kundi hili lilifikia hatua ya mwisho na ya juu kabisa ya kupasuka kwakwe, baada ya Kikwete ambae ni sehemu ya zao la kundi hilo kujichomoa na kumsaliti king mwenzie (Lowassa) na kutengeneza kundi jipya ndani ya ccm. Kutokana na nguvu ya Lowassa wakati ule ccm ambayo ilitokana na kundi lake la asili, kundi la Kikwete lilikuwa na wakati mgumu sana, kwasababu lilikuwa halina ukubwa na ushawishi mkubwa kama kundi ambalo kikwete amelisaliti isipokuwa tu kutokana na Ushawishi wake Kikwete kama Rais na mjumbe mzoefu alie asi na baadhi ya wajumbe wake na wote tunafahamu shughuli waliokuwa nayo walipo mkata Lowassa.

Sasa Magufuli amezaliwa kutokana na Kundi kubwa ndani ya ccm kuvunjika kwa kusalitiana na kwa bahati mbaya sana, makundi haya yote yalijikuta yako tena kwenye uwanja mmoja (ulingo wa siasa (ccm), na katikati yupo Magufuli. Kundi la Kikwete kwa sasa lina nguvu kubwa kutokana uwekezaji mkubwa wa kikwete ndani ya serikali na ccm, lakini kundi la Lowassa ni kubwa kutokana na uzito wa wajumbe wake ndani ya ccm na ushawishi wao kwa Rais magufuli. Vita inapamba moto. Na makundi yote haya mawili kwanza hayakubaliani, lakini kubwa zaidi haya mkubali Magufuli kwasababu mwenendo wa magufjli una athari zinazo fanana kwa makundi yote na timu yake. Kundi la lowassa linatumia fursa tu, na tusisahau Ndoto ya Lowassa kuongoza nchi haijafa.

Rais magufuli anadhani yuko salama, kwasababu kuna vita ya ziada kwa makundi haya mawili, anadhani kuliimarisha kundi la Lowassa kutamsaidia yeye kupita kiulaini 2020 kwasababu ya mvutano mkali utakaozidi kuimarika baina ya makundi haya mawili ambayo tayari vita hiyo imeanza kujidhihirisha hadharani baada ya matamshi ya Bashe yenye dhana ya kisasi dhidi ya watu wa kundi la Kikwete. Kitendo hiki kimemshawishi sana magufuli kwamba ataweza kuvuka kiulaini sana. Na hili linaonesha kupata mafanikio kwasababu kundi la lowassa sio tu linapewa nyadhifa sasa na magufuli bali, limeanza kuinunua vita ya magufuli na wakina musiba wanaanza kutoweka kiana.

Kinachokwenda kutokea..

1. Kwanza tuelewe, makundi haya yote yana ushawishi mkubwa ndani ya ccm kuliko magufuli mwenyewe.

2. Makundi haya yana ushawishi mkubwa ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama kuliko magufuli mwenyewe.

3. Magufuli sio tu, hana ushawishi mkubwa kwenye vyombo vya usalama kuliko mahasimu wake, Bali hata ndani ya ccm na hata kwenye nchi (Taifa) maana watu wamemchoka kabisa, kweli Raia tumemchoka kabisa.

4. Magufuli amenza kuunda chama chake kipya ndani ya ccm (ccm mpya), inayobebwa na kundi la watu ambao hawana ushawishi wowote ndani ya ccm, hawana uzoefu wa kutosha wa kuongoza nchi, hawana mizizi mirefu ndani ya siasa za ccm, kimsingi watu hawa ni wanasiasa kwenye taswira ya magufuli (magufulisim).

Sasa, mwisho wa kukomaa kwa vita hii kubwa ya mafahari wawili, itapelekea nchi kuwa kwenye hali mbaya zaidi kiuchumi, kisiasa na kijamii. Jamii itazidi kuyajua maovu mengi yaliofichwa dhidi ya ccm, bila kujali ni ccm asilia au mpya au nani, na kimsingi jamii itakuwa imejaa chuki kubwa dhidi ya ccm yote, bila kujali huyu anatoka kundi gani, kwasababu wote hawa nje ya ccm wanajulakana kama ni ccm tu. Magufuli hatokuwa kwenye nafasi ya kufanya mambo mapya, kwasababu ya mtifuano huu na mtifuano huu ndio utakao chukua nafasi kubwa zaidi kuelekea 2020 kwenye masikio ya watu na si magfuli, kimsingi magufuli atakpjikuta anafika 2020 akiwa anachukiwa kuliko mwanzo.

Itakapofikia hapo, wakati wa kufanya maamuzi ya nani anapaswa kuivusha ccm, itategemea mshindi wa kati ya makundi haya mawili, lile la Kikwete na lile la Lowassa, na kimsingi, vyombo vya dola na usalama vitakuwa kwenye nafasi kubwa ya ushawishi ndani ya nchi na ccm yenyewe kuliko wakati wowote ule, na jamii itakuwa ikiamini zaidi kwa wapinzani, hapa ndipo maamuzi ya ama magufuli au mwingine ndani ya ccm atapaswa kuwekwa kama mgombea yanaweza sio tu kufanyika na ccm wenyewe, pengine Jeshi la nchi, na kwa vyovyote vile, jeshi la nchii kwa sisi wachambuzi wa mambo haliwezi kumruhusu magufuli kuendelea na awamu ya pili. Chakuzingatia tu, wakati huo (2020) kuna uwezekano baadhi ya watu hatutakuwa nao, kimwili au kisiasa, akiwemo Magufuli mwenyewe. Hapa ndipo namuona Lowassa akiibuka tena.

Watu wanaosema, ccm imekuwa ikifikia hatua kubwa ya mpasuko, na huweza kujinasua upya, wanasahau wakati huo, kulikuwa na kundi moja, na baadae likaongezeka hili la pili ambalo limejengeka kwenye msingi wa visasi, na sasa tuna makundi mawili yenye nguvu yasiokuwa tayari kupatana na kukaa meza moja, kitu ambacho hakijawai kutokea huko nyuma.

Hichi kinacho onekana Lowassa na Rostam kumuunga mkono Magufuli si kitu cha kufuraia sana, usishangae 2020 mgombe wa ccm akawa Edward Lowassa na sio Magufuli tunae dhani ndie. Mwelekeo wa mambo wa sasa unabadilika kwa kasi kubwa sana, na kuna kila dalili za ccm kufikia tamati, ijapokuwa kweye mazingira tata sana. Lowassa ni mzuri sana kwenye kuficha na kulinda hadhi yake yeye binafsi. Mwaka 2015 kuna utafiti ulionesha ndie amgombea pekee aliekuwa na ushawishi mkubwa kuliko wanasiasa wengine kwa tofauti ya asilimia 11 akifuatiwa na Dr. Slaa. Huu ni ushawishi binafsi bila chama. Na kimsingi anajua jinsi ya kuwatumia wengine, na ana watu wenye weledi mkubwa kwenye kumlinda tofauti na magufuli anaetetewa na vichaa kama musiba.

Naendelea kutoa ushauri kwa vijana wa ccm, kujaribu kuchagua upande sahihi mapema na sio kukesha kupyauka, leo unamtukana huyu, kesho unamtukana yule, mwisho unajikuta unatakiwa kumsifia mtu uliemtukana jana, utasimamaje? Vijana muwe wenye hekima sana, na pengine mjitaidi kunyamaza kimya, unaedhani ana nguvu leo, kesho unaweza kumkuta ni laini kama siagi......kuni zinawaka moto sana....

A. Ndambo
Pole sana ndugu yangu!Magufuli anashinda kwa kura nyingi tu.Nitarudi hapa tarehe 29/10,/2020.Kukumbusha .
 
Ni JPM TENA October 28th tutapiga kura nyingi sana za upendo mkubwa kwa JPM

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Back
Top Bottom