Uwezekano wa Magufuli kuongoza nchi kwa kipindi cha pili haupo

Uwezekano wa Magufuli kuongoza nchi kwa kipindi cha pili haupo

Na Anderson Ndambo

Itakapofikia hapo, wakati wa kufanya maamuzi ya nani anapaswa kuivusha ccm, itategemea mshindi wa kati ya makundi haya mawili, lile la Kikwete na lile la Lowassa, na kimsingi, vyombo vya dola na usalama vitakuwa kwenye nafasi kubwa ya ushawishi ndani ya nchi na ccm yenyewe kuliko wakati wowote ule, na jamii itakuwa ikiamini zaidi kwa wapinzani, hapa ndipo maamuzi ya ama magufuli au mwingine ndani ya ccm atapaswa kuwekwa kama mgombea yanaweza sio tu kufanyika na ccm wenyewe, pengine Jeshi la nchi, na kwa vyovyote vile, jeshi la nchii kwa sisi wachambuzi wa mambo haliwezi kumruhusu magufuli kuendelea na awamu ya pili. Chakuzingatia tu, wakati huo (2020) kuna uwezekano baadhi ya watu hatutakuwa nao, kimwili au kisiasa, akiwemo Magufuli mwenyewe. Hapa ndipo namuona Lowassa akiibuka tena.
Umeupiga mwingi sana Bwana Ndambo, hii inaonyesha kuwa wewe ni political pundit 🙏🤝 Nimeipenda hii paragraph niliyoinakili, hii inaonyesha kabisa kuwa wakati sisi "wananchi wa kawaida" tunaona kifo cha Magufuli kama "mipango ya Mungu", lakin kwa nyinyi wataalamu wa siasa mliliona hili mapema kama kuondoka kwa Magufuli ni lazima by any means necessary. Hasa ulipo sema : Nina quote

" JESHI LA NCHI HII, NA KWA VYOVYOTE VILE, JESHI LA NCHI HII KWASISI WACHAMBUZI WA MAMBO, HALIWEZI KUMRUHUSU MAGUFULI KUENDELEA NA AWAMU YA PILI, CHA KUZINGATIA TU WAKATI HUO WA (2020) KUNA UWEZEKANO BAADHI YA WATU HATUTOKUWA NAO, KIMWILI AU KISIASA, AKIWEMO MAGUFULI MWENYEWE".

Na imetokea kweli, kwamba hakuruhusiwa kuendelea kuongoza na wenye nchi. Timing tu ndo imebadilika,waliona kuwa bora waache uchaguzi upite kwanza kupunguza rabsha, halaf warekebishe waweke mtu wao mwingine. Kwa maana hiyo sasa kwa mujibu wa makala yako ni kwamba timu ya Kikwete imeishinda tena ile ya Lowassa. Na hii nafikiri ni kwakuwa Lowassa sasa afya yake haimruhusu kuendelea na mapambano. Angekuwa bado yupo vizuri, shuguli Ingekuwa pevu. Lakin credit pia iende kwa mkwere anajua kuzichanga karata zake vizuri, maana anakijua chama kindakindaki. Lakin kwa mimi naomba niseme kuondolewa kwa jiwe is a good riddance. Alikuwa hana mission wala vision. Na alitaka kuichange system kwa muda mfupi sana, wakati wenzake wapo kwenye game muda mrefu na wanaijua nchi nje ndani. Ukweli ni kwamba nchi ilikuwa inaenda shimoni. Watu wangekuwa masikini wa kutupwa, tungerudi nyuma kisiasa miaka 50. Kweli hii nchi ina wenyewe 🙌🙌
 
Sina usemi mkuu.
Mipango ya Mungu siyo sawa na yawanadamu mkuu.
Hata wewe na Mimi twaweza kufa kwa sekunde mbili tu zijazo

Basi tukawe wenye utu, wanyenyekevu, wasikivu na wenye huruma.

Hii ya kujiita mawe, kuwa hatatushiki wala kutikiswa hailipi!

Kwamba kina Ben, Mawazo, Azory, Lissu, wa kwenye viroba nk hayakuwa mapenzi ya Mungu bali ya binadamu mmoja, basi ndiyo maana leo tunakumbushana.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Duh! Wewe ndio umechemka kabisa kumleta Ngoyai kwenye equation. Mtu ambaye yuko 'ICU' anawezaje kweli kugombea Urais?
Labda hujaona clipp yake ya hivi karibuni... Ngoyai keshajichokea. The best for him now ni kujiandaa kiroho kwa safari inayofuata...
Nakusalimu kwa jina la jamhuri ya muungano
 
Basi tukawe wenye huruma, wasikilize na wenye huruma.

Hii ya kujiita mawe, kuwa hatarishi wala kutishika hailipi!

Kwamba kina Ben, Mawazo, Azory, Lissu, wa kwenye viroba nk hayakuwa mapenzi ya Mungu bali ya binadamu mmoja, basi ndiyo maana leo tunakumbushana.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Hahaa all those you have mentioned,were eliminated by nature.
Their fates were meant to be.katika maisha yao amini amini nakuambia walizopitia ilikuwa sehemu ya ratiba katika maisha yao waliopangiwa kuwepo duniani .
Kama ingekuwa mipango ya mwanadamu wasipitia hayo.
Maisha ya Mwanadamu ni fumbo kubwa Sana ambalo kila mtu hajui hatima yake.ila kwa imani tunapanga maisha yetu ya kesho with no any guarantee that we will see tommorow.
 
Hahaa all those you have mentioned,were eliminated by nature.
Their fates were meant to be.katika maisha yao amini amini nakuambia walizopitia ilikuwa sehemu ya ratiba katika maisha yao waliopangiwa kuwepo duniani .
Kama ingekuwa mipango ya mwanadamu wasipitia hayo.
Maisha ya Mwanadamu ni fumbo kubwa Sana ambalo kila mtu hajui hatima yake.ila kwa imani tunapanga maisha yetu ya kesho with no any guarantee that we will see tommorow.

Hahaahaaa. Acha hizo wewe. Mtumishi wa Mungu alitamka kuwa pana vifo aina nne:

1. Uzee (wa miaka ma Mia wako hapa)
2. Vya kusababishwa na kusababishiwa (wa viroba wako hapa)
3. Mapenzi ya Mungu (vya kina Nyerere viko hapa).
4. Vya kijinga (kudharau corona vipo hapa)

Unataka clip mtumishi?
 
Na Anderson Ndambo.

Kuna mambo yanahitaji jicho la Tatu kuyaona na pengine kuyaamini. Tabia mojawapo ya siasa ni kubadilika badilika kulingana na majira na wakati kutokana na sababu za wakati husika, lakini kwa Tanzania mabadiliko haya yamekuwa na kasi kubwa mno, hicho si kitu cha kawaida, kama ambavyo Magufuli mwenyewe hakutegemea kuukwaa Urais wa Tanzania kwa kuchaguliwa kuwa mgombea wa ccm, vilevile mazingira kama yale yanaweza kubadilisha hali ya mambo na matokeo yakawa tofauti na tunavyodhani kuelekea 2020.

Rais Jakaya Kikwete aliingia madarakani kutokana na kuimarika kwa kundi lenye nguvu lililokuwa likiongozwa na Lowassa ndani ya ccm, na kwa wakati huo ndio lilikuwa kundi lenye nguvu ndani ya chama hicho (ccm) lililoweza kudhihirika na kuweza kutoa ushawishi na kulazimisha Kikwete kuingia madarakani na kundi hilo likamkaanga vikali, Salim na kumtowesha kabisa kwenye ulingo wa siasa za kitaifa ndani ya ccm na nchi kwa ujumla. Kundi hili lilianza kujijenga tangu wakati Nyerere akiwa madarakani na kimsingi lilikomaa sana wakati wa Mkapa kiasi kwamba Mkapa akashindwa kulidhibiti.

Mwaka 2015, kundi hili lilifikia hatua ya mwisho na ya juu kabisa ya kupasuka kwakwe, baada ya Kikwete ambae ni sehemu ya zao la kundi hilo kujichomoa na kumsaliti king mwenzie (Lowassa) na kutengeneza kundi jipya ndani ya ccm. Kutokana na nguvu ya Lowassa wakati ule ccm ambayo ilitokana na kundi lake la asili, kundi la Kikwete lilikuwa na wakati mgumu sana, kwasababu lilikuwa halina ukubwa na ushawishi mkubwa kama kundi ambalo kikwete amelisaliti isipokuwa tu kutokana na Ushawishi wake Kikwete kama Rais na mjumbe mzoefu alie asi na baadhi ya wajumbe wake na wote tunafahamu shughuli waliokuwa nayo walipo mkata Lowassa.

Sasa Magufuli amezaliwa kutokana na Kundi kubwa ndani ya ccm kuvunjika kwa kusalitiana na kwa bahati mbaya sana, makundi haya yote yalijikuta yako tena kwenye uwanja mmoja (ulingo wa siasa (ccm), na katikati yupo Magufuli. Kundi la Kikwete kwa sasa lina nguvu kubwa kutokana uwekezaji mkubwa wa kikwete ndani ya serikali na ccm, lakini kundi la Lowassa ni kubwa kutokana na uzito wa wajumbe wake ndani ya ccm na ushawishi wao kwa Rais magufuli. Vita inapamba moto. Na makundi yote haya mawili kwanza hayakubaliani, lakini kubwa zaidi haya mkubali Magufuli kwasababu mwenendo wa magufjli una athari zinazo fanana kwa makundi yote na timu yake. Kundi la lowassa linatumia fursa tu, na tusisahau Ndoto ya Lowassa kuongoza nchi haijafa.

Rais magufuli anadhani yuko salama, kwasababu kuna vita ya ziada kwa makundi haya mawili, anadhani kuliimarisha kundi la Lowassa kutamsaidia yeye kupita kiulaini 2020 kwasababu ya mvutano mkali utakaozidi kuimarika baina ya makundi haya mawili ambayo tayari vita hiyo imeanza kujidhihirisha hadharani baada ya matamshi ya Bashe yenye dhana ya kisasi dhidi ya watu wa kundi la Kikwete. Kitendo hiki kimemshawishi sana magufuli kwamba ataweza kuvuka kiulaini sana. Na hili linaonesha kupata mafanikio kwasababu kundi la lowassa sio tu linapewa nyadhifa sasa na magufuli bali, limeanza kuinunua vita ya magufuli na wakina musiba wanaanza kutoweka kiana.

Kinachokwenda kutokea..

1. Kwanza tuelewe, makundi haya yote yana ushawishi mkubwa ndani ya ccm kuliko magufuli mwenyewe.

2. Makundi haya yana ushawishi mkubwa ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama kuliko magufuli mwenyewe.

3. Magufuli sio tu, hana ushawishi mkubwa kwenye vyombo vya usalama kuliko mahasimu wake, Bali hata ndani ya ccm na hata kwenye nchi (Taifa) maana watu wamemchoka kabisa, kweli Raia tumemchoka kabisa.

4. Magufuli amenza kuunda chama chake kipya ndani ya ccm (ccm mpya), inayobebwa na kundi la watu ambao hawana ushawishi wowote ndani ya ccm, hawana uzoefu wa kutosha wa kuongoza nchi, hawana mizizi mirefu ndani ya siasa za ccm, kimsingi watu hawa ni wanasiasa kwenye taswira ya magufuli (magufulisim).

Sasa, mwisho wa kukomaa kwa vita hii kubwa ya mafahari wawili, itapelekea nchi kuwa kwenye hali mbaya zaidi kiuchumi, kisiasa na kijamii. Jamii itazidi kuyajua maovu mengi yaliofichwa dhidi ya ccm, bila kujali ni ccm asilia au mpya au nani, na kimsingi jamii itakuwa imejaa chuki kubwa dhidi ya ccm yote, bila kujali huyu anatoka kundi gani, kwasababu wote hawa nje ya ccm wanajulakana kama ni ccm tu. Magufuli hatokuwa kwenye nafasi ya kufanya mambo mapya, kwasababu ya mtifuano huu na mtifuano huu ndio utakao chukua nafasi kubwa zaidi kuelekea 2020 kwenye masikio ya watu na si magfuli, kimsingi magufuli atakpjikuta anafika 2020 akiwa anachukiwa kuliko mwanzo.

Itakapofikia hapo, wakati wa kufanya maamuzi ya nani anapaswa kuivusha ccm, itategemea mshindi wa kati ya makundi haya mawili, lile la Kikwete na lile la Lowassa, na kimsingi, vyombo vya dola na usalama vitakuwa kwenye nafasi kubwa ya ushawishi ndani ya nchi na ccm yenyewe kuliko wakati wowote ule, na jamii itakuwa ikiamini zaidi kwa wapinzani, hapa ndipo maamuzi ya ama magufuli au mwingine ndani ya ccm atapaswa kuwekwa kama mgombea yanaweza sio tu kufanyika na ccm wenyewe, pengine Jeshi la nchi, na kwa vyovyote vile, jeshi la nchii kwa sisi wachambuzi wa mambo haliwezi kumruhusu magufuli kuendelea na awamu ya pili. Chakuzingatia tu, wakati huo (2020) kuna uwezekano baadhi ya watu hatutakuwa nao, kimwili au kisiasa, akiwemo Magufuli mwenyewe. Hapa ndipo namuona Lowassa akiibuka tena.

Watu wanaosema, ccm imekuwa ikifikia hatua kubwa ya mpasuko, na huweza kujinasua upya, wanasahau wakati huo, kulikuwa na kundi moja, na baadae likaongezeka hili la pili ambalo limejengeka kwenye msingi wa visasi, na sasa tuna makundi mawili yenye nguvu yasiokuwa tayari kupatana na kukaa meza moja, kitu ambacho hakijawai kutokea huko nyuma.

Hichi kinacho onekana Lowassa na Rostam kumuunga mkono Magufuli si kitu cha kufuraia sana, usishangae 2020 mgombe wa ccm akawa Edward Lowassa na sio Magufuli tunae dhani ndie. Mwelekeo wa mambo wa sasa unabadilika kwa kasi kubwa sana, na kuna kila dalili za ccm kufikia tamati, ijapokuwa kweye mazingira tata sana. Lowassa ni mzuri sana kwenye kuficha na kulinda hadhi yake yeye binafsi. Mwaka 2015 kuna utafiti ulionesha ndie amgombea pekee aliekuwa na ushawishi mkubwa kuliko wanasiasa wengine kwa tofauti ya asilimia 11 akifuatiwa na Dr. Slaa. Huu ni ushawishi binafsi bila chama. Na kimsingi anajua jinsi ya kuwatumia wengine, na ana watu wenye weledi mkubwa kwenye kumlinda tofauti na magufuli anaetetewa na vichaa kama musiba.

Naendelea kutoa ushauri kwa vijana wa ccm, kujaribu kuchagua upande sahihi mapema na sio kukesha kupyauka, leo unamtukana huyu, kesho unamtukana yule, mwisho unajikuta unatakiwa kumsifia mtu uliemtukana jana, utasimamaje? Vijana muwe wenye hekima sana, na pengine mjitaidi kunyamaza kimya, unaedhani ana nguvu leo, kesho unaweza kumkuta ni laini kama siagi......kuni zinawaka moto sana....

A. Ndambo
Ulitabiri vizuri lakini kutoendelea kutawala kwa Magufuli si kwa maana ya matukio ya kisiasa bali kwa karma.

Wat goes around comes around.
Cha kushangaza wananchi wengi wameyapokea mabadiliko kwa bashasha.
 
"Naendelea kutoa ushauri kwa vijana wa ccm, kujaribu kuchagua upande sahihi mapema na sio kukesha kupyauka, leo unamtukana huyu, kesho unamtukana yule, mwisho unajikuta unatakiwa kumsifia mtu uliemtukana jana, utasimamaje? Vijana muwe wenye hekima sana, na pengine mjitaidi kunyamaza kimya, unaedhani ana nguvu leo, kesho unaweza kumkuta ni laini kama siagi......kuni zinawaka moto sana...."

vijana wa CCM kuna ujumbe wenu hapa. kama utabiri umekamilika, basi chukueni huo ushauri utawasaidia na hasa MATAGA
 
uchambuzi mzuri magu akitoboa 2020 kwanzia 2022 atakuwa na hali mbaya adi wenye viti wa mtaa wa CCM watakuwa wanamtukana. kipindi hiki cha miaka mitano watu wako kimyaa maana wanajua anaweza akaendelea, baada 2020 magu ujeuri lazima umuishe na ndo atapata picha halisi ya CCM.
hawa wote wanaomwabudu watakuwa wameshamkimbia na kufwata upepo wa Raisi anaefuata.

Heshima kwako mkuu. Taabu ni kuwa mamburula huwa akili kubwa hawazielewi hadi yawakute!
 
Magu amekuwa Phased out State House kwa sababu ya kuwa Encircled na Washamba, Wewe unatoa watu Jalalani na kwa Wala Vumbi la Chaki unawaleta waje wakuzunguke kama inner circle yako hio haifai, mana hao academicians mostly ni theoretical based, Na izo PhD pamoja na Mzee kuwa na Hazina still wamezidiwa ujanja, Alivyotoka Kijazi ambae yeye yupo vizuri tukajua mfalme nae anafikiwa sasa
With all huwezi ku lead kwa udictator kama huna hata Millitary background
 
Back
Top Bottom