Nimejaribu kusoma kwa makini maeleze yako kuna vitu vichache nimegundua (Unaweza kunisahihisha kwani lengo ni kukusaidia)
1. Wewe bado ni mdogo kiumri.
2. Unajaribu kujitetea sana ili uonekane huna kosa ndio maana unatumia sana neno kwa bahati mbaya.
3. Hauna uelewa wa elimu ya uzazi.
Malengo mliojiwekea ya kutokufanya mapenzi kabla ya ndoa ni mazuri, hivyo ni vyema ukajiepusha na vishawishi vya kimapenzi hasa usipendelee kukaa sehemu zilizo faragha wewe na huyo mpenzi wako.
Kulingana na maelezo yako, sina uhakika sana kama uume wa mpenzi wako uliingia wote, ullingia nusu au uliishia tu kwenye nyama ya juu ya uke pasipo kuzama ndani.
Kama uume uliingia wote na wewe siku za mzunguko wako ni zile hatarishi basi jiandae tu kuwa mama, vinginevyo ondoa woga na wakati mwingine mjifunze kutembea na kinga hata kama nia yenu ni kutoshiriki mapenzi kabla ya ndoa(askari utembea na silaha hata kama hakuna vita).