Uwezekano wa mradi wa mabasi ya 'Mwendo basi' ku collapse!

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2016
Posts
8,658
Reaction score
15,793
Tunapofanya evaluation ya viability ya mradi tunaangalia maeneo mbali mbali kama financial risks, operational risk etc.

Leo ningependa kuchambua haya maeneo mawili ili kuwasaidia kimawazo waendeshaji wa mradi huu wa mabasi ya 'mwendo basi'...

Financially mradi uko viable

Kulingana na takwimu walizotoa waendeshaji wa mradi huu wa mabasi, walisema kuwa kwa siku huwa wanasafirisha hadi abiria laki moja na arobain na sita elfu kwa nauli ya Tsh 650. Hii ina maana mapato ya mradi kwa siku huwa ni Tsh 95,000,000 (146,000 X 650) kwa siku nzuri na Tsh milioni 71 kwa siku mbaya (95,000,00 X 0.75)

So kwa mwaka mradi huu una uwezo wa kuingiza hadi Tsh Bilioni 34 za kitanzania.

Kwa hiyo kwa upatikanaji wa soko lililo tayari (ready market) mradi huu ni financially viable.

Operational viability

Changamoto za mradi huu zinakuja sana sana kwenye upande wa uendeshaji wa mradi.

Changamoto za wizi wa mafuta, upotevu wa mapato unaotokana na utendaji wa watumishi wasio waaminifu, ubovu wa mabasi (Si unaujua tena Mchina) n.k ndio the weakest point ya mradi huu.

Laiti kama mradi huu ungeendeshwa kwa kutumia mabasi yaliyotengenezwa Japan au Nchi nyingine za Ulaya, kutokana na uimara wa mabasi mradi huu ungekuwa wa mafanikio makubwa.

Haya mabasi yaliyopo tu hata kwa kusikia mngurumo wa engine utatambua kuwa zile engine zinazunguka revolution nyingi sana per minute hivyo kuna uwezekano mabasi hayo yakawa na matumizi makubwa ya mafuta.

Utatuzi wa Changamoto za mradi

Kumekuwa na malalamiko makubwa kutoka kwa upande wa wasafiri hasa wakidai kukaa vituoni kwa muda mrefu. Kama kweli mradi umezidiwa na idadi ya wasafiri, ni bora wasimamishe uendeshaji wa ruti moja wapo na kuyajaza mabasi kwenye ruti mama ya Kimara KKoo na Kimara Kivukoni hadi pale watakapo kaa sawa. Pia waendeshaji wa mradi huu watafute namna ya kutatua changamoto ya ukusanyaji wa mapato ikiwemo kuweka makondakta ambao watakusanya nauli kama kwenye dala dala za kawaida... Hili litasaidia sana kusimamia upotevu wa mapata ambao kwa sasa naamini ni mkubwa sana...
Pia nawashauri wawekezaji waingie gharama za kubadilisha engine za yale mabasi na kuweka engine zinazotumia natural gas au kuweka engine nyingine za Mjapan au Mzungu ambazo naamini zitakuwa fuel efficient...

Kuwe na mabasi Ordinary na Express

Unajua gari linaposimama simama hutumia mafuta mengi Zaidi kuondoka mpaka lipate mwendo.
Kupunguza gharama za mafuta yale mabasi marefu yafanywe kuwa Express. Yani likitoka Kimara linasimama Ubungo, Magomeni, Fire na Kariakoo au Posta. Yale ordinary ndio yawe yanasimama vituo vyote. Kupunguza idadi ya vituo kwa mabasi ya express kutachangia kuokoa upotevu wa mafuta angalau kwa asilimia kumi kwa siku...
Mengine wana JF mtajazia...
 
Nimesikia kwenye magazeti wanalakamika hawa jamaa kuwa eti wanapata hasara.. Nijajua kuwa wanapataje hasara?
Ni poor management au?
Yani wanavyoonekana wanatokwa na mapovu wanataka kuongeza nauli nadhani....
Inatakiwa watuwekee incomes mapato yote na running cost ili tuone kuwa je ni kweli wanapata hasara?
 
1)(Over staffing)
2)Gari zinatumia sana mafuta kutokana na ukaribu wa vituo,taa za kuongoza magari,
3)Ubovu wa magari ni pasua kichwa na joto bado halijapanda ipasavyo
 
Nilipofika Dar na kuyaona/kuyatumia haya mabasi nilijiuliza papo hapo ni kwa nini mradi mkubwa kama huu wasingeingia na kampuni kama ya Mercedes ya Ujerumani?....sioni kabisa uhai wa haya mabasi baada ya miaka mitano.
 
Mtoa mada una uzoefu gani wa biashara?, isije ikawa ni kati ya wale ambao mmebobea kwenye theory za economics na kuja hapa luleta vijineno vya financial viable, maneno ya theory hayo
 
Nilipofika Dar na kuyaona/kuyatumia haya mabasi nilijiuliza papo hapo ni kwa nini mradi mkubwa kama huu wasingeingia na kampuni kama ya Mercedes ya Ujerumani?....sioni kabisa uhai wa haya mabasi baada ya miaka mitano.

Hiyo sio sababu. Mahesabu hayako hivyo, ishu ni kwamba ndani ya miaka 5 hilo basi la kichina litakuwa limerudisha pesa na kuleta faida? Faida ndio swala la msingi, unaweza kununua basi la kichina M80, lakini mpaka linachoka linakuwa limekupa M400 na ukanunua lingine.
 
Kiukweli mradi una changamoto nyingi lakini mi inayonikera zaidi na ambayo naiona kuwa itawaharibia ni uendeshaji mbovu wa mradi kwenye nysnja ya utoaji tikets , unaweza kaa kituoni zaidi ya saa moja unaambiwa tiketi zimeisha. Nadhani ni vizuri uwekwe mfumo wa kufanya tiketi ziwe zinapatikana kwa wakati wote katika vituo vyote
 
Kwanini usichukue kadi?
 
Tunapofanya evaluation ya viability ya mradi tunaangalia maeneo mbali mbali kama financial risks, operational risk etc.

Leo ningependa kuchambua haya maeneo mawili ili kuwasaidia kimawazo waendeshaji wa mradi huu wa mabasi ya 'mwendo basi'...

Financially mradi uko viable

Kulingana na takwimu walizotoa waendeshaji wa mradi huu wa mabasi, walisema kuwa kwa siku huwa wanasafirisha hadi abiria laki moja na arobain na sita elfu kwa nauli ya Tsh 650. Hii ina maana mapato ya mradi kwa siku huwa ni Tsh 95,000,000 (146,000 X 650) kwa siku nzuri na Tsh milioni 71 kwa siku mbaya (95,000,00 X 0.75)

So kwa mwaka mradi huu una uwezo wa kuingiza hadi Tsh Bilioni 34 za kitanzania.

Kwa hiyo kwa upatikanaji wa soko lililo tayari (ready market) mradi huu ni financially viable.

Operational viability

Changamoto za mradi huu zinakuja sana sana kwenye upande wa uendeshaji wa mradi.

Changamoto za wizi wa mafuta, upotevu wa mapato unaotokana na utendaji wa watumishi wasio waaminifu, ubovu wa mabasi (Si unaujua tena Mchina) n.k ndio the weakest point ya mradi huu.

Laiti kama mradi huu ungeendeshwa kwa kutumia mabasi yaliyotengenezwa Japan au Nchi nyingine za Ulaya, kutokana na uimara wa mabasi mradi huu ungekuwa wa mafanikio makubwa.

Haya mabasi yaliyopo tu hata kwa kusikia mngurumo wa engine utatambua kuwa zile engine zinazunguka revolution nyingi sana per minute hivyo kuna uwezekano mabasi hayo yakawa na matumizi makubwa ya mafuta.

Utatuzi wa Changamoto za mradi

Kumekuwa na malalamiko makubwa kutoka kwa upande wa wasafiri hasa wakidai kukaa vituoni kwa muda mrefu. Kama kweli mradi umezidiwa na idadi ya wasafiri, ni bora wasimamishe uendeshaji wa ruti moja wapo na kuyajaza mabasi kwenye ruti mama ya Kimara KKoo na Kimara Kivukoni hadi pale watakapo kaa sawa. Pia waendeshaji wa mradi huu watafute namna ya kutatua changamoto ya ukusanyaji wa mapato ikiwemo kuweka makondakta ambao watakusanya nauli kama kwenye dala dala za kawaida... Hili litasaidia sana kusimamia upotevu wa mapata ambao kwa sasa naamini ni mkubwa sana...
Pia nawashauri wawekezaji waingie gharama za kubadilisha engine za yale mabasi na kuweka engine zinazotumia natural gas au kuweka engine nyingine za Mjapan au Mzungu ambazo naamini zitakuwa fuel efficient...

Kuwe na mabasi Ordinary na Express

Unajua gari linaposimama simama hutumia mafuta mengi Zaidi kuondoka mpaka lipate mwendo.
Kupunguza gharama za mafuta yale mabasi marefu yafanywe kuwa Express. Yani likitoka Kimara linasimama Ubungo, Magomeni, Fire na Kariakoo au Posta. Yale ordinary ndio yawe yanasimama vituo vyote. Kupunguza idadi ya vituo kwa mabasi ya express kutachangia kuokoa upotevu wa mafuta angalau kwa asilimia kumi kwa siku...
Mengine wana JF mtajazia...
Cheki tena hesabu zako katika mapato;Angalau jaribu kutoa mafuta,tairi na malipo ya wafanyakazi.
Masuala ya Spares ndo kabisaa utaona huu mradi bora ungekuwa chini ya wamiliki wa madaladala na ninyi watu wa ma Theory muendelee kuweka data kwenye makaratasi
 
Hawa sio simon group hao wenye huu mradi??
147677366009488996006.jpg
 
Back
Top Bottom