Nitaanza na maana ya kilimo mtandao.
KILIMO MTANDAO, hii ni huduma ya kilimo ambayo inatoa taarifa na kupokea taarifa kuhusu hali ya klimo, masoko ya mazao, hali ya hewa na mabadiliko ya nchi pamoja na matumizi mengine ya kiteknolojia kupitia mtandao. Hii inasaidia kurahisisha mawasiliano miongoni mwa wadau wa kilimo katika kutambua hali ya masoko ikoje, mazao yapi yanahitajika na soko lake liko wapi, bei za mazao na mengine kadhalika ili kurahisisha uzalishaji na uendeshaji wa kilimo.
Katika harakati za kujipambanua na umasikini vijana na wanawake wanapitia changamoto nyingi sana kuzifikia ndoto zao za mafanikio. changamoto hizo kama vile ulevi, madawa ya kulevya, uraibu wa kingono mambo ambayo yanapelekea kudhoofisha jitihada zao katika kuifikia kesho iliyo nzuri kwao na wanayoitamani. Hivo basi kuna haja ya kuwezeshwa katika nyanja tofauti ikiwemo kilimo mtandao ili waweze kujipambanua na kuukimbia umasikini. Basi kupitia makala hii nitaainisha mambo ambayo yakifanyiwa kazi yataweza kuleta manufaa kwa mtu binafsi na taifa kwa ujumla. katika makala hii ya uwezeshwaji wa vijana na wanawake kupitia kilimo mtandao, jitihada kutoka pande mbili zinahitajika ili kuyafikia malengo ya ndoto ya vijana na wanawake kupitia kilimo mtandao. pande hizi ni ;
1. Jitihada ya wahusika wenyewe ( vijana na wanawake) katika kilimo.
2. JItihada ya serikali kuwainua vijana na wanawake.
Nikianza na upande wa kwanza wa vijana na wanawake wanapaswa kutambua kilimo ni fursa kama zilivyofursa zingne za kibiashara ambapo inahitaji uwekezaji wa malengo ili kuweza kupata matokeo mazuri. yafuatayo yakizingatiwa, vijana na wanawake yanaweza kuleta manufaa na kuzifikia ndoto zao.
Serikali lazima ipange mipango na njia ambazo zitaweza kusaidia n kundi hili la vijana na wanawake ili kuweza kujitegemea na kuweza kupunguza kilio cha ajira serikalini na pia kutengeneza walipa kodi wazuri.
MWANZA TANZANIA

- Vijana lazima kutambua kilimo ni sehemu ya maisha ya mwafrika na sio adhabu. moja ya changamoto kubwa hasa kwa vijana wengi ni kutokutambua kuwa kilimo ni sehemu ya maisha yetu kama waafrika ambapo tunatakiwa kukipenda na kukithamini na kukifanya kama sehemu ya maisha yetu ya kila siku na sio kukichukulia kama adhabu ama kukichukulia kama kazi inayofanywa na watu ambao hawajasoma ama watu waishio vijijini.
- Vijana lazima watambue kilimo ni biashara. kuna aina mbalimbali za kilimo, kama vile kilimo cha mazao ya chakula ( subsistance) na kilimo cha mazao ya kibiashara (commercial crops). kilimo chochote kina manufaa kulingana na eneo ulipo, changamoto zilizopo pamoja uhitaji wa eneo ililopo. lakini kwa upande wangu napendekeza subsistance crops kulingana na Tanzania ilivyo. pia kuna faida zake moja wapo ni kwamba haupangiwi bei ya kuuza bali unapanga wewe mwenyewe, faida ya mbili uendeshaji wake hauna gharama kubwa ukilinganisha na mazao ya kibiashara, tatu uhitaji wake ni mkubwa na soko lake la ndani ni kubwa kwa hiyo hauna haja ya kutegemea soko la nje kama karafuu, kakao na pamba.
- Usawa wa kijinsia katika kilimo. hii ni changamoto sana miongoni mwa watanzania na waafrika kwa ujumla. suala la kijinsia katika kutekeleza majukumu linakuwa linaachiwa upande mmoja hasa upande wa wanawake ambao ndio wanaonekana kuwa wahusika wakuu katika kilimo. ushirikiano katika kilimo kwa jinsia zote ni chachu itakayopelekea kuongezeka kwa uzalishaji. Hivyo yafuatayo yazingatiwe moja, wanawake lazima wamiliki ardhi kama wanaume ili kutoa changamoto ya kwamba atatoa wapi ardhi ili azalishe. pili ushiriki wa wanaume ni muhimu ili kuongeza ufanisi wa uzalishaji.
- Vijana na mabadiliko ya kilimo katika nyanja ya kiteknolojia. Teknolojia ina mchango mkubwa katika kuongeza ufanisi wa uzalishaji. kwa mfano matumizi ya dhana za kilimo ambazo hazitumii gharama kubwa kuziendesha. Teknolojia pia ni muhimu kwan inarahisisha utafutaji wa masoko wa mazao anayozalisha hivyo kumwondolea usumbufu wa kutembea kwenda kutafuta masoko. kwa mfano kilimo mtandao ( E- agriculture) kinasaidia sana vijana na wanawake kuwasiliana na masoko moja kwa moja na kusaidia uzalishaji wao.
- kuunda vyama vyao vya kilimo. Vijana na wanake wanapaswa kuunda vyama vyao vya kilimo (AGRICULTURAL ORGANIZATIONS) zitakazowasaidia kupanga bei ya mazao yao ili kupunguza wizi unaofanywa na walanguzi pindi wanapoanza mauzo. pia vyama vitasaidia maelewano ya kibiashara ( burgaining power) kuliko kuuza mtu binafsi. Pia vyama vitasaidia kusimamia vipimo na kutoa dhana ya makadirio ya vipimo kama matumizi ya Lumbesa, Ndonya na kangomba vinavyoathiri wazalishaji. mambo haya yatasaidia vijana na wanawake kuweza kuzifikia ndoto zao.
- Matumizi ya mitandao katika kilimo. vijana na wanawake wana wigo mkubwa katika matumizi ya mitandao ambapo wakiitumia katika kilimo itawafungulia masoko ya ndani na nje na kuweza kupata fursa ambayo itawasaidia kufanya kilimo bora na uzalishaji wenye tija na kuachana na kilimo cha mazoea.
Serikali lazima ipange mipango na njia ambazo zitaweza kusaidia n kundi hili la vijana na wanawake ili kuweza kujitegemea na kuweza kupunguza kilio cha ajira serikalini na pia kutengeneza walipa kodi wazuri.
- serikali itengeneze mfumo utakao wezesha vijana kupata machine za kilimo kama vile matrekta, na machine zingine. kwa mfano kupitia mikoa, wilaya, na harimashauri ziratibu makundi ya vijana walimo kwenye maeneo yao ili waweze kuwapangia bajeti ambayo itawakwamua na uhaba wa mitaji ambayo wataitumia katika kuanzisha shughuli za uzalishaji. faida zake itasaidia vijana na wanawake kuongeza uzalishaji na serikali itapata mazao mengi ambayo yataongeza pato kwa serikali
- serikali itoe ruzuku ili kupunguza gharama za uzalishaji na hivyo kufanya upatikanaji wa mazao kwa bei nafuu ambayo yatachochea ushindani wa uzalishaji viwandani na pia bidhaa zitakazo zalishwa zitakua na bei nafuu kabisa.
- kuandaa mfumo mzuri wa masoko kuanzia soko la ndani na nje ili kuwezesha mzunguko mkubwa uzalishaji na kupunguza mrundikano wa mazao ambao unaweza kupelekea kuoza na kusababisha hasara kwa wakulima kwa ujumla.
- serikali isogeze huduma za kifedha maeneo ya karibu na uzalishaji ambapo vyama vya vijana na wanawake vitaweza kukopeshwa kwakuaminiwa kwa sababu taasisi za kifedha zitakua zinawatembelea wakulima na kuratibu uzalishaji wao ili waweze kuzalisha kilimo chenye tija.
- serikali iwaeleweshe vijana na wanawake kuhusu kilimo. kupitia taasisi ya mawasiliano serikalimlazima iandae makongamano, warsha mabilimbali zitakazosaidia kuwaelewesha vijana fursa zilizopo kwenye kilimo . hii itasaidia vijana kuwa na morali ya kuzalisha kuliko inavofanya sasa kuwaambia vijana wajiajiri kupitia kilimo bila jitihada zozote zile.
- Serikali iandae mfumo mzuri wa vipimo ambao utakua unatumika nchi nzima ili kutoa hali iliyopo sasa ya walanguzi kujipangia vipimo vyao ambavyo vinaumiza wakulima wadogo hasa vijana wanaojiajiri kupitia kilimo.
- serikali ipunguze makato na kodi katika kilimo ili kuweza kuwapa vijana unafuu wa kuweza kuzalisha na kupata faida kubwa ambayo itawasaidia kupanua wigo na mitaji yao katika biashara zao na hii itawasaidia kuweza kujitegemea.
- serikali kupitia vyama vya wakulima iwatafutie mirahaba na mikataba na makampuni ambayo yatawawezesha vijana na wanawake kupata pembejeo na uhakika kwa soko kwani hii itawapa hamasa vijana kujituma kwa sababu uhakika wa kile wanachozalisha tayari kinasoko tayari
MWANZA TANZANIA
Upvote
2