BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Uwezo mdogo wa wauguzi kutambua mapema ugonjwa wa saratani kwa watoto umetajwa kuwa changamoto mojawapo inayotatiza matibabu ya ugonjwa huo.
Katika kutatua changamoto hiyo, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas) ikishirikiana na Taasisi ya Global Hope ya nchini Marekani imeandaa kongamano la siku mbili (Februari 21 -22) kuwajengea uwezo wauguzi namna ya kutambua na kuwatibu watoto wenye saratani mapema.
Akifungua kongamano hilo leo Jumanne, Februari 21,2023 Mkurugenzi wa Huduma za uuguzi na ukunga Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Redemptha Matinde amesema changamoto ya matibabu ya saratani kwa watoto inatokana na ugonjwa huo kutogundulika mapema.
"Jambo lingine ni kukosekana kwa vifaa vya kutambua ugonjwa huu mapema na upatikanaji wa dawa kutibu maradhi hayo, kutokana na utafiti wa kisayansi saratani ya watoto inatibika kwa kiasi kikubwa tu Kwa nchi zilizoendelea asilimia 80 ya watoto kwenye nchi zilizoendelea wanapata matibabu, kwa nchi zinazoendelea matibabu ipo chini ya asilimia 30,"amesema.
Redemptha amesema upatikanaji wa takwimu za watoto wenye saratani ni mdogo kutokana na uwezo wa wananchi na wataalamu kuufahamu ugonjwa huo mapema kuwa mdogo.
Akizungumzia kongamano hilo amesema lina umuhimu mkubwa katika kuwajengea uwezo wataalamu ambao watakwenda kuielimisha jamii namna ya kugundua ugonjwa huo mapema kwa watoto. Amesema tatizo la saratani hurithiwa na mtoto kutoka kwa wazazi wake na zipo aina mbalimbali za ugonjwa huo kulingana na eneo linaloshambuliwa.
"Zipo saratani zinazoathiri damu, kinga ya mwili, ubongo hivyo saratani zote zinaelezeka kulingana na eneo lililoathiriwa," ameeleza.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya uuguzi Muhas, Dk Dikson Mkoka amesema kongamano hilo ni njia ya kuwaongezea weledi watalaamu wa afya.
“Mafunzo haya yameanza kutolewa muda si mrefu na hii ni baada ya kuona kuna uhitaji mkubwa wa wanafunzi kusaidiwa uweledi katika kutambua magonjwa ya saratani kwa watot, Muhas na Taasisi ya Global health tukashirikiana kuwaongezea uweledi wataalamu wetu hasa kutambua dalili za awali kabisa za saratani kwa watoto,"ameeleza.
Dk Mkoka amesema kutoka na na changamoto ya wataalamu kutambua saratani ya watoto mapema, utambuzi wa ugonjwa huu kwa kundi hilo ni chini ya asilimia 30.
Kongamano hilo la siku mbili limeshirikisha wataalamu mbalimbali kutoka Botwana, Kenya, Malawi Uganda pamoja na mikoa mbalimbali ya Tanzania na Zanzibar.
Kulingana na mapendekezo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) hadi kufikia 2030 utambuzi wa watoto wenye saratani unapaswa kufikia asilimia 60.
Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na Utafiti wa Saratani (IAR) linaonyesha hadi 2020 watoto na vijana 280,000 wenye umri wa miaka 0-19 wametibiwa saratani, 110,000 wakipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.
MWANANCHI