Uwezo wa kumiliki roho/mapepo yenye nguvu

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Tuna visa vingi sana vya mauaji ya kutisha ya watu wa kawaida na watu walemavu hasa wenye ulemavu wa ngozi
Tuna visa vingi vya mauaji ya kikatili na watu kunyofolewa viungo-tukio la karibuni kabisa likiwa la mjini Arusha ile maiti iliyokutwa chumbani kwenye hotel moja maarufu ikiwa haina kichwa na viungo kadhaa.

Tuna mauaji ya koromeo watoto wadogo na hata vikongwe na saa nyingine watu wenye nahitaji maalum tuna upotevu mkubwa sana wa watu hasa watoto tungekuwa tunaweka takwimu za siku wiki mwezi na mwaka tungetafuta chanzo na ufumbuzi wa haraka lakini bahati mbaya sana tunaishi kwa mazoea na kudhani kila kitu ni kudra za Mwenyezi Mungu Tunapotoka.

Dunia inaumwa!Madaraka utajiri maarufu na kupendwa vinaangamiza roho nyingi zilizokuwa na hatia tunaichosha dunia iliyokwishazeeka.Haya yote tunayoyatafuta ya kumiliki utajiri madaraka umaarufu na kupendwa yanatusababisha kumiliki roho zenye kisasi juu yetu kisasi cha ukatili tuliofanya kwenye miili yao Kwa ajili ya kupata damu na viungo.

Visa vya watu wanaokufa kimazingara, visa vya watu wanaokufa kwa ajali za kutengeneza visa vya watu wanaouliwa kwa Mateso na kuchukuliwa viungo yao roho zao hazina nguvu ya kutenda utakayo kama visa vya mtu anayepotea na kufa bila kujijua na ndugu na jamaa wakibaki na sintofahamu ya kwamba uko hai au umekufa.

Maneno huumba, ile hali tu ya maiti yako kuonekana na kuzikwa hupunguza nguvu ya roho yako kuleta matokeo yanayotakiwa na waganga na wachawi wa level ya chini ndio hutumia viungo halisi na reflections za maiti halisi kufunika ukweli watu wabaya kabisa na wa kuogopwa mno ni wale wanaopoteza watu na baadae kuwaangamiza na kutumia malighafi za mhanga kwa lengo kusudiwa.

Hii hurahisisha mengi kwakuwa katika ulimwengu wa physical bodies hajulikani kama umekufa au la na watu huogopa kuweka matanga wakihofia siku moja unaweza kuonekana. Kwahiyo hii trend ya kupotea kwa watu kila siku ina maana yake kubwa sana isiyosemwa wala kujulikana na wengine na kama kuna ndugu jamaa au rafiki alishawahi kupotea kimoja.

Tafakari post hii
 
'niuzie misukule wawili mzee wangu nahitaji wakanifanyie kazi kwenye shamba langu...'

'hakuna tatizo ila jambo moja muhimu, najua kuwa wee ndio kwanza unaingia kwenye hili suala la hii sayansi yetu, naomba ufate haya maelekezo vizuri ; itakapofika siku ya kufa kwao kiukweli unatakiwa uwapeleke kaburini kwao walipozikwa na ndugu zao sawa kijana...?'

'sawa mzee wangu nimekuelewa vizuri'

'usipofanya hivyo juwa kuwa utakufa wewe...!'

'sawa hakuna tatizo mzee wangu, sasa itabidi ukanioneshe hilo kaburi lake...'


Wakachukuzana na kupanda kwenye ungo wakiwa kama walivyozaliwa kwenda kumuonesha mteja wake kaburi la wale misukule anaotaka kumuuzia.

Walifika wakatua na ungo wao na kumuonesha sehemu waliyozikwa wale misukule na kisha akamkabidhi kwa ajili ya kwenda kumfanyia kazi shambani kwake. Kijana akawachukua tayari kwa kuondoka nao. (Hapa ikumbukwe kuwa mmiliki wa misukule ni lazima ajue makaburi ya misukule wake wote, hata kama wapo mia.)

...kwa bahati mbaya pia ndugu wa marehemu walichelewa kuwashughulikia ndugu zao ikawa maiti zao tayari zimeshakatwa ulimi ambapo huwa ni ngumu sana kurudi katika hali ya kawaida wakishafika kwenye hatua hiyo.




Ni moja ya mfano wa misukule hiyo.






'kwa kifupi sio viumbe wa kuwaogopa hata kidogo, ukiwaogopa shauri yako...'

Yule mzee alimuusia yule kijana kuwa hawa sio viumbe wa kuwaogopa hata kidogo, ukiwaogopa unawapa nafasi kubwa zaidi ya kuweza kukutawala kwa hiyo hakuna kuwaogopa.

Aliiondoka yule mzee bila ya kumuaga yule kijana, ni kufumba na kufumbua tu hakuwepo eneo lile akiwa amemuachia misukule yake pale, ikiwa ndio mara yake ya kwanza yule kijana kumiliki misukule...!.
 
nduki umenionjesha kidogo endelea tafadhali
 
Last edited by a moderator:
Duh mshana mada kama hz leteni asubuhi,
Me mchango naweza kusema kwa ni kweli kuwa matukio ya watu kupotea yameongezeka sana na kwa sababu agenda kuu ni uchaguzi basi yamekuwa hayazungumziwi,kuna familia zimepoteza mtu mpk sasa hawajampata...huko vijijin watu wana chinjana nje nje sio poa kwa kweli,itakuwa weng wanageuzwa kuwa misukule
 

Huku nilipo ni mchana joh mitazamo
 
Last edited by a moderator:
huyu jamaa sheria ya mtandao inamuhusu
 
mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmhhhhhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
nduki umenionjesha kidogo endelea tafadhali


...asubuhi ilifika yule mwanamke aliamka ambapo usiku aliskia sauti za watu wakiongea mule ndani kwake kwa lugha asiyoifaham na kila alipojaribu kumuamsha mumewe hakuamka kumbe alilala na gogo tu pale kitandani na wala sio mumewe.

'...baba midoli, wee baba midoli huskii sauti za watu zikiongea na nyayo zikitembea humu ndani, kulala gani huko mume wangu?'

Kumbe mumewe hakuwepo pale kiuhalisia alikwenda kufanya kazi za kichawi makaburini, hakujua kuwa pale kitandani kulikuwa na gogo tu na wala hakuwa mumewe, ila kwa macho ya kawaida tunayotumia binadam huwezi kugundua kama ni gogo, yeye aliona yupo na mumewe kama kawaida kitandani wamelala pamoja.

Kulipokucha alimuhadithia mumewe kuhusu jambo lililokuwa likiendelea usiku huo. Mumewe alikataa katakata kuhusu hilo suala na kumwambia kuwa labda ilikuwa ni ndoto tu pengine alikuwa anaota (Ikumbukwe pia kuwa misukule inapozungumza huwezi kuelewa chochote kinachozungumzwa hata kidogo)

Na pia, hata kama unalala na mchawi kitanda kimoja hata kama akitoka kwenda kuloga hutaweza kujua kama ametoka kwa sababu utaendelea kuona kuwa bado yupo pale kitandani wakati mwenzako tayari ameshaenda kucheza na maiti na kula nyama za watu na kunywa damu.




 
Last edited by a moderator:

Imekaa vizuri usikatishe uhondo 👆
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…