MimiNiMakini
Member
- Jun 19, 2022
- 7
- 20
"Huyu jamaa anachojua saizi ni kusema "and stuff like that" basi 😁 "
Nimekuta caption hii huko twitter, aisee watu wa twitter wamefunguka mambo mengi sana kuhusu Mtangazaji Lil Ommy.
Kiufupi Inadaiwa kwamba uwezo wa Lil Ommy tangu aje Wasafi umeshuka sana, Jamaa akiwa Times Fm alikuwa moto sana Kuliko sasa Akiwa Wasafi. Watu wengi wanadai kwamba Hivi sasa Lil Ommy anavimaneno vyake ambavyo anaweza akaviongea hata mara 1000 katika Kipindi chake, Mfano, Yo Ready Know, Kizazi Sana, Ushindi ni Mwingi, Ladies and Gentlemen, Boys and Girls.
Watu wengi wanadai kwamba jamaa anaigiza sana anajikuta Black American Fulani hivi kumbe ni wa Tabora huko. Mbali na kudai kwamba uwezo wa Lil Ommy kushuka, wanadai pia kwamba Lil Ommy hajui kuvaa kabisa.
Maoni Yangu
Binafsi sizani kama uwezo wa @lilommy umeshuka, tatizo ni kwamba Ukiwa Wasafi tu utaonekana hujui tu, Imagine angekuwa Clouds Leo hii Angeonekana Mtangazaji bora. Wasafi inadamu fulani tu hivi ya kuchukiwa.
Lil Ommy bado ni bora sana tena upande wa Interviews. Kuhusu yeye kurudia rudia maneno, sizani kama ni Kosa, Of course kila mtangazaji inabidi awe na Catch Phrases zake ili ajibrand zaidi na ajitofautishe na Wengine. Leo hii ukisikia neno "KIZAZI SANA" Tayari unafikiria kuhusu Lil Ommy, kwahiyo hizi Catch Phrases ni muhimu ila hazitakiwi kuzidi sana wakati unatangaza.
Suala la Kuvaa siliingilii, ila suala la kujikuta mmarekani, sizani kama ni tatizo ni identity yake tu. Uwezo wa Lil Ommy bado ni mkubwa sana.
VIPI KWA MTAZAMO WAKO, uwezo wa @lilommy umeshuka au haujashuka?