ielewemitaa
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 10,764
- 9,477
Kwani huko EFM wana msifia Mondi ? acha watu wafanye mambo yaoKule si ana be controlled na remote hayupo huru tena kama zamani just imagine asiwasifie konde gang wala ali kiba hata wakitoa nyimbo nzuri kule ni kumsifia boss tu yaani ni sawa na mwanasiasa atoke chadema na kwenda CCM hata kama alikuwa anatoa madini kiasi gani akifika huko anakuwa mgonga meza.
Watu wa Twitter !!!
"Huyu jamaa anachojua saizi ni kusema "and stuff like that" basi 😁 "
Nimekuta caption hii huko twitter, aisee watu wa twitter wamefunguka mambo mengi sana kuhusu Mtangazaji Lil Ommy.
Kiufupi Inadaiwa kwamba uwezo wa Lil Ommy tangu aje Wasafi umeshuka sana, Jamaa akiwa Times Fm alikuwa moto sana Kuliko sasa Akiwa Wasafi. Watu wengi wanadai kwamba Hivi sasa Lil Ommy anavimaneno vyake ambavyo anaweza akaviongea hata mara 1000 katika Kipindi chake, Mfano, Yo Ready Know, Kizazi Sana, Ushindi ni Mwingi, Ladies and Gentlemen, Boys and Girls.
Watu wengi wanadai kwamba jamaa anaigiza sana anajikuta Black American Fulani hivi kumbe ni wa Tabora huko. Mbali na kudai kwamba uwezo wa Lil Ommy kushuka, wanadai pia kwamba Lil Ommy hajui kuvaa kabisa.
Maoni Yangu
Binafsi sizani kama uwezo wa @lilommy umeshuka, tatizo ni kwamba Ukiwa Wasafi tu utaonekana hujui tu, Imagine angekuwa Clouds Leo hii Angeonekana Mtangazaji bora. Wasafi inadamu fulani tu hivi ya kuchukiwa.
Lil Ommy bado ni bora sana tena upande wa Interviews. Kuhusu yeye kurudia rudia maneno, sizani kama ni Kosa, Of course kila mtangazaji inabidi awe na Catch Phrases zake ili ajibrand zaidi na ajitofautishe na Wengine. Leo hii ukisikia neno "KIZAZI SANA" Tayari unafikiria kuhusu Lil Ommy, kwahiyo hizi Catch Phrases ni muhimu ila hazitakiwi kuzidi sana wakati unatangaza.
Suala la Kuvaa siliingilii, ila suala la kujikuta mmarekani, sizani kama ni tatizo ni identity yake tu. Uwezo wa Lil Ommy bado ni mkubwa sana.
VIPI KWA MTAZAMO WAKO, uwezo wa @lilommy umeshuka au haujashuka?
Sio kweli mzee,,,Empire n pindi kali sana east AfricaBdozen ndo amekuwa kituko kabisa huyu...
Kwani bibie tunaangalia muonekano wake au kazi yake kiujumla?Katika watu siwaelewagi ni wanaume wanene waliovimbiana,, huyu Kaka wa kwenye picha Ni ana mashavu alivyo mfupi na hizo nguo zake anafanana diaba,, hana swagger
Mie nimejadili muonekano wake Kama kakijeba flani hivi, kanabeua ovyo tuKwani bibie tunaangalia muonekano wake au kazi yake kiujumla?
Sivizuri ujue mimi binafsi nilikuwa kama wewe niliwahi kujisemea zitakuwa na Mwanamke mwembamba kabisa maishani mwangu na nilikuwa nawabeza Sana Wanawake wa aina hii lakini huwezi amini nikajakufall in love na Mwanamke mwembamba kiasi ambacho sijitambui kwake hata marafiki zangu wakawa hawaamini ni mimi kweli lakini the end of the day tukawa kwenye mahusiano ya muda mrefu nilikuja kuachana ni kwasababu ya tofauti ya kidini na pressure nilizokuwa napata kwa ndugu zake maana manzi yeye alikuwa ni muislamuMie nimejadili muonekano wake Kama kakijeba flani hivi, kanabeua ovyo tu
Story yako hii sijakuuliza wala hainisaidii kitu,Sivizuri ujue mimi binafsi nilikuwa kama wewe niliwahi kujisemea zitakuwa na Mwanamke mwembamba kabisa maishani mwangu na nilikuwa nawabeza Sana Wanawake wa aina hii lakini huwezi amini nikajakufall in love na Mwanamke mwembamba kiasi ambacho sijitambui kwake hata marafiki zangu wakawa hawaamini ni mimi kweli lakini the end of the day tukawa kwenye mahusiano ya muda mrefu nilikuja kuachana ni kwasababu ya tofauti ya kidini na pressure nilizokuwa napata kwa ndugu zake maana manzi yeye alikuwa ni muislamu
🤣🤣🤣🤣🤣🤣Story yako hii sijakuuliza wala hainisaidii kitu,
Hii yupo nayo kitambo sana..👣"and stuff like that" basi 😁 "
Naunga mkono hoja, dogo yuko vizuri, namkubali sana!.Lil Ommy bado ni bora sana tena upande wa Interviews.