Uwezo wa wachezaji wa zamani, sijapata kuona kwa sasa

Uwezo wa wachezaji wa zamani, sijapata kuona kwa sasa

george aloyce

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2017
Posts
1,302
Reaction score
2,023
"Mara ya kwanza wakati nakutana na Ronaldo kwenye mechi nilikuwa naitumikia timu ya Parma. Dakika chache baada ya mechi kuanza, nilikutana nae macho kwa macho akiwa anafanya mikimbio huku anakokota mpira kwa kasi.

Sikuwahi kuona vitu kama vile kwa kipindi cha nyuma kwenye maisha yangu ya kucheza mpira (uwezo mkubwa wa Ronaldo). Akiwa anakokota mpira akawa analisogelea goli letu. nikajaribu kumkwatua lakini sikumpata, haraka nikamgeukia Fabio Cannavaro nikambwatukia muweke chini huyo, Cannavaro alilazimika kumkwatua Ronaldo bahati nzuri Refa alimuonya tu Cannavaro mechi ikaendelea.

Baada ya dakika kadhaa Ronaldo alikuja tena mbele yangu akiwa ana kokota mpira kwa kasi ile ile, sikuwa na cha kufanya maana alinipita na sikuweza kumzuia. Cannavaro akaniangalia na akaniambia. "Lily, tutamaliza mechi tukiwa wachezaji 9 usiku wa leo kama tusipokuwa makini, tunawezaje kuzuia hii hali?.

Kumbe wakati tunaongea haya yote, Ronaldo alikuwa anatusikiliza na ghafla aligeuka na kutufuata akatuambia, "Samahani, leo nasifiwa sana kuliko uwezo wangu"

Kwa maneno yale tulijiona kama watoto ambao hawana msaada, hayo ni maneno ya nguli Lilian Thuram akimuelezea Ronaldo de Lima jinsi ambavyo alikuwa bora pindi awapo uwanjani.

Dunia inakosa kabisa aina ya washambuliaji kama hawa waliowahi kutisha miaka ya nyuma, wanazungumzwa wachezaji wengi wa zamani akiwemo Pelle na Maradona kama ni moja ya wachezaji waliowahi kufanya vizuri kwenye medani ya kabumbu ulimwenguni, lakini jina la Ronaldo lina zungumzwa kwa herufi kubwa sana na wapenda soka kutokana na uwezo aliokuwa nao enzi zake.

Kasi ndani ya uwanja, maarifa, nguvu, uwezo wa kufunga magoli kwa kupiga mawe tena kwa kutumia miguu yote miwili kwa ufasaha, maono awapo uwanjani, ni moja ya vitu vilivyokuwa vinamtofautisha kwa kiasi kikubwa Ronaldo na washambuliaji wengine.

Familia ya soka na mitaa yote kwa ujumla bado tunaendelea kutukuza na kuhusudu uwezo wa Ronaldo kutokana na kile alichokuwa anakifanya enzi zake.
 
Baresi, Nesta, Cannavaro, Maldini, Matarazzi, Thuram, Blanc, Ayala, Panuci, Lucio

Hawa ma forward wa kisasa including akina Messi na C.Ronaldo wangelikuta na na hao defenders katika prime zao wangelifedheheka sana.
 
Hujui ama hufuatilii mpira.
Messi alianza kuchezea senior team Barcelona akiwa na 19 years.
Aliwahi kutana na baadhi ya mabeki nguli na hawakuweza kumkaba.
Game ya kwanza alipiga hat-trick mbele ya mabeki nguli wa real madrid kipindi cha kina Ronaldinho.
Kamfuatilie vizuri yule jamaa tokea akiwa kadogo miaka 6 akiwa analilia kucheza mpira mitaani licha ya kuwa mgonjwa.
Messi is a pure talented man in football kiuhalisia.
 
kuna yoyote kati ya hao niliowataja aliwahi kukutana nae akamnyanyasa wakiwa bado wapo kwenye prime zao?

memorible game za messi alikutana na Old age Roberto Carlos, Sylvester, Boateng
 
kuna yoyote kati ya hao niliowataja aliwahi kukutana nae akamnyanyasa wakiwa bado wapo kwenye prime zao?

memorible game za messi alikutana na Old age Roberto Carlos, Sylvester, Boateng
Kwako wewe hao ni wepesi!?
Pia katizame list vizuri.
 
sasa Sylvester mkuu ni mzima? unamkumbuka vizuri lakini?
Mkuu katizame kikosi cha 2006 cha Real madrid halafu useme wale viungo wakabaji mpaka mabeki walikua wepesi au sio wepesi?
Maana huo ndio mwaka Messi alipiga hat-trick kuiokoa Barcelona dhidi ya bao tatu za Real madrid.
Cannavaro na Roberto Carlos walikuwepo pia katika hiyo game.
 
cannavaro na carlo walikuwa ni wazee, hawakuepo tena kwenye ubora wao. yani carlo alikuwa ana kitumbo kabisa.
 
cannavaro na carlo walikuwa ni wazee, hawakuepo tena kwenye ubora wao. yani carlo alikuwa ana kitumbo kabisa.
Wote walikua na miaka 33 mkuu.
Hivi miaka 33 ndio uwe mzee hivyo kiasi cha kushindwa kutumia uzoefu kumzuia kijana mdogo anayeanza soka?
 
Back then wachezaji hawakuwa na mbeleko, they knew jitihada zao ndio zitawabeba and they have to work hard more kufika walipo fika. Modern day too much kudeka, too much mbeleko, too much rules
 
Back then wachezaji hawakuwa na mbeleko, they knew jitihada zao ndio zitawabeba and they have to work hard more kufika walipo fika. Modern day too much kudeka, too much mbeleko, too much rules
Kama mngesema baada ya kizazi cha Messi na Ronaldo Christiano hatutaona vipaji nguli hapo nakubali.
Ila mkiwatoa kizazi cha Messi na Ronaldo(including Iniesta,Xavi,Modric)e.t.c hamjatenda haki.
 
Kama mngesema baada ya kizazi cha Messi na Ronaldo Christiano hatutaona vipaji nguli hapo nakubali.
Ila mkiwatoa kizazi cha Messi na Ronaldo(including Iniesta,Xavi,Modric)e.t.c hamjatenda haki.
kizaz cha akina messi and ronaldo kiko class yake, hawa ni wale last batch natural talented individuals. After that itabidi tusubiri next 20 yrs or more mpaka wapatikane wengine
 
Wote walikua na miaka 33 mkuu.
Hivi miaka 33 ndio uwe mzee hivyo kiasi cha kushindwa kutumia uzoefu kumzuia kijana mdogo anayeanza soka?

unafahmu kitu kuwa hawakuwa tena kwenye ubora wao? wachezaji wa kisasa wapo more fit kuliko wa zamani, 34 kwa miaka ya zamani ni miaka mingi sana.
 
unafahmu kitu kuwa hawakuwa tena kwenye ubora wao? wachezaji wa kisasa wapo more fit kuliko wa zamani, 34 kwa miaka ya zamani ni miaka mingi sana.
Mmmmh!
Mkuu sio kwamba wazamani walikua wako fit kuliko wa sasa hivi!?
Anyway tufanye yametamatika.
 
Back
Top Bottom