Uwezo wetu wa kufikiri ni mdogo sana ndio maana tumeshindwa kuchambua hotuba ya kiongozi wa nchi na salamu za MO tumekimbilia kwa Robertinho

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Habari zote Leo ni Simba day na namna Robertinho alivyo na wasiwasi na uwezo wa Mosses Phiri.

Hotuba ya Mhe.Rais jana ilikuwa nzuri sana na imejenga msingi mzuri kwa timu zetu zinazokwenda kupambana kimataifa, Mhe.Rais ameongea mambo mengi ikiwemo serikali kuendelea kuunga mkono timu zetu ili zing'are kimataifa, aliipongeza yanga na akaahidi serikali yake itajenga complex nyingine zenye unyama mwingi kule Dodoma na Arusha.

Mo Dewji naye akapeleka salamu kwa kiongozi wa nchi, akamwambia mhe Rais msimu ujao atapambana kuhakikisha Simba inapeleka ndoo pale Ikulu.

Hotuba ya Rais na salamu za mwekezaji hazijapewa kipaumbele kabisa Leo, waaandishi makanjanja wanasubiri jamiiforums ianzishe mada wao wadakie.Sasa nawaambia hotuba ya Rais na Mo Dewji ni mambo ya msingi sana watanzania wakayajua, kujadili tamasha sijui Robertinho kutomchezesha Phiri ni uwezo mdogo wa kufikiri.

Am a think tank, cpend kuwachosha ngoja nichokoze mada.
 
Ni kweli...suala la ujenzi wa viwanja viwili vya michezo Arusha na Mwanza vyenye uwezo wa kuchukua watu Kila kimoja elfu thelathini halikupewa attention sana na vyombo vya habari.

Watu hupenda kujadili upuuzi na lawama kuliko maendeleo yenyewe
 
Kweli umetustua wengi, binafasi nilikuwa sijamsikia Mo, nimeenda kumsikiliza baada ya kukusoma wewe.

Kaongea maneno mazuri sana. Na sasa nakwenda mumsikiliza tena mama Samia.

Mama Samia Oyeeeee.
 
Kiongozi wa NCHI AMEPOTEZA MVUTO...

MO DEWUJI TAPELI WA B20...Hana Mpya...

Moses Phiri anafikirisha kwa wanaojua Mpira...

Mengine tupambane Mkataba tata wa Dp Wedi uondoshweee....

Siasa ktk Michezo zikome...
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji849]
 
Kiongozi wa NCHI AMEPOTEZA MVUTO...

MO DEWUJI TAPELI WA B20...Hana Mpya...

Moses Phiri anafikirisha kwa wanaojua Mpira...

Mengine tupambane Mkataba tata wa Dp Wedi uondoshweee....

Siasa ktk Michezo zikome...
Kweli,Bring back our Moses Phiri
 
Hatuwezi kaa tukajadili vitu hewa, ahadi za viongozi si za kuamini.
Mangapi waliahidi na hayajatimia, wapi uwanja wa Dodoma?
Hayo ni Mambo ya machawa wa mama

La phiri Sisi watu wa soka linatuhusu, phiri anakaa benchi kibu anacheza, saidoo anaruka ruka, anaingia mkongwe bocco ye anasugua.
 
Kiongozi angeanza kufafanua vifungu Tata vya mkataba Tata wa bandari, ndipo angeendelea na mengine.
 
Wewe mwenyewe ndiye umejaza threads za kumpopoa Kocha Robertinho kwa suala la kutomchezesha Phiri hivyo wewe ndiye mwenye upeo duni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…