Uwiano wa uwakilishi baina ya Zanzibar na Tanganyika

Uwiano wa uwakilishi baina ya Zanzibar na Tanganyika

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Leo tarehe 31 / 12 / 2012 Rais wa JMT Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katangaza matokeo ya idadi ya watu Tanzania.Tanzania ina jumla ya watu 44,929,002,Tanzania bara watu 43,625,434 na Zanzibar watu 1,303,568.

Bunge la JMT lina jumla ya wabunge 323 kati yao wabunge 232 ni wakuchaguliwa na wananchi moja kwa moja,wengine 10 wanateuliwa na Rais wa JMT, 75 ni viti maalum [wanawake],wabunge 5 wanachaguliwa na BLW Zanzibar.

Zanzibar ina jumla ya majimbo 50 ya uchaguzi,Tanganyika majimbo 182 ya uchaguzi.Sasa ukiangalia idadi ya watu baina ya Tanganyika na Zanzibar na idadi ya uwakilishi bungeni hauko sawa kabisa sijui ni vigezo vipi vilitumika kuwapatia nafasi waZanzibar uwakilishi mkubwa kupita kiasi !.Kama hiyo haitoshi wako baadhi ya wanasiasa mbumbumbu wanataka kiwepo kipengele kitakacho wahakikishia waZanzibar wawe na zamu ya kutoa Rais wa JMT.Yaani watu 1,303,568 wanataka kujenga uhalali wa kutwalawa watu 43,625,435 !.

Naomba tujadili baada ya miaka 50 ya kujitawala bado zipo sababu za huu muungano wa kulazimisha unaonufaisha upande mmoja ?.

Nakala: Nguruvi3 Ritz JokaKuu Mkandara chama Zitto Ben Saanane Crashwise Mwita Maranya AshaDii Raia Fulani Mzee Mwanakijiji Ab-Titchaz Rutashubanyuma Matola sweke34 Mag3 Mzee wa Rula Mimibaba Ogah Kibunango Jasusi Nyani Ngabu Pasco FJM Barubaru Kobello mohamed Shossi ....
 
Last edited by a moderator:
Ngongo, wiki iliyopita makam wa rais wa Zanzibar amelalamika kuwa katika balozi zetu wameajiriwa wazanzibar wachache sana. Ameshindwa kuelewa kuwa bungeni kuna wazanzibar wanaowakilisha nyumba kumi.

Malalamiko ya ZNZ kuonewa hayana msingi kabisa. Wao wanatafuta sababu kwa jicho la kengeza.
Fikiria makam wa rais katoka na data za ajira za ubalozi, bila kufikiria kuwa kuna WZNZ wameajiriwa huku bara bila ya manufaa yoyote kwa ZNZ kama wakurugenzi wa halmashauri n.k.

Sasa utashangaa katika tume ya katiba wamepiga kelele wanataka nusu kwa nusu.
Bajeti ya tume ambayo ni ya kifisadi ya bilioni 35 ZNZ inachangia Zero, I mean nothing.

Kwenye raha wanataka usawa, kwenye majukumu hawataki kuwajibika.

Haiwezekani watu wa wilaya moja ya Ilala watake Urais kwa zamu. Kwanza watueleze wanaweka nini mezani katika kuchangia gharama. Sio Urais tu, Urais unakuja na majukumu na je wapo tayari?
 
Asante Nguruvi3 nilidhani niko pekee yangu katika hili huu muungano hauna maana kabisa.

Ngongo, wiki iliyopita makam wa rais wa Zanzibar amelalamika kuwa katika balozi zetu wameajiriwa wazanzibar wachache sana. Ameshindwa kuelewa kuwa bungeni kuna wazanzibar wanaowakilisha nyumba kumi.

Malalamiko ya ZNZ kuonewa hayana msingi kabisa. Wao wanatafuta sababu kwa jicho la kengeza.
Fikiria makam wa rais katoka na data za ajira za ubalozi, bila kufikiria kuwa kuna WZNZ wameajiriwa huku bara bila ya manufaa yoyote kwa ZNZ kama wakurugenzi wa halmashauri n.k.

Sasa utashangaa katika tume ya katiba wamepiga kelele wanataka nusu kwa nusu.
Bajeti ya tume ambayo ni ya kifisadi ya bilioni 35 ZNZ inachangia Zero, I mean nothing.

Kwenye raha wanataka usawa, kwenye majuku hawataki kuwajibika.

Haiwezekani watu wa wilaya moja ya Ilala watake Urais kwa zamu. Kwanza watueleze wanaweka nini mezani katika kuchangia gharama. Sio Urais tu, Urais unakuja na majukumu na je wapo tayari?
 
Last edited by a moderator:
Ngongo, Nguruvi3, Pasco,

..kwa kweli mimi huu muungano umenichosa kweli kweli.

..wa-ZNZ hawaishi kulalamika wakati wao ndiyo wanatunyonya.

..serikali ya muungano imekuwa mzigo kwa wananchi wa Tanganyika.

..mimi napendekeza tufanye majaribio kwa ZNZ wawe ndiyo serikali ya muuungano.

..ZNZ wabebe majukumu ya serikali hiyo ikiwemo kuidhamini Tanganyika wakati tunapohitaji mikopo.

..zaidi, ZNZ watulipie gharama za umeme kwa kubeba jukumu la kuendesha Tanesco, lakini mafuta na gesi viwe vya Tanganyika.

..sisi Tanganyika tubakie na serikali ndogo tu inayoshughulikia mambo yasiyokuwa ya muungano kwa upande wa Tanganyika.
 
Last edited by a moderator:
Joka kuu, ukishataja gharama tu hutapa mznz hata mmoja nakuhakikishia.
Ukitaka kuwapata tangaza nafasi za kazi maalum kwa ZNZ, nafsi za shule upendeleo kwa ZNZ, futa kodi kwa bidhaa zinzoingia kupitia kwao, chukua madeni lakini mkopo pasu pasu.

Ndio maana tunasema wanavyoleta hoja ndivyo wanavyowazindua Watanganyika.
Huko nyuma Watanganyika hawakujua kuwa wanabeba mzigo mzito namna hii.
Tulisikia kelele wananyonywa, wanaonewa, waachwe wapumue! Sasa hivi kimya!

Husikii anayekuja hapa kutetea upuuzi, wamebaki na mkataba mkononi.
Serikali 3 mkononi huku wengine wakiwa na vyote mkononi.
Sasa wamekuja na hoja mpya,''uhusiano wa kidugu wa siku nyingi kibiashara, kuoleana na uwekezaji'' hata kama muungano utavunjika. Hilo tumeling'amua. Tuna uhusiano na Kenya pia kama ilivyo uganda hata Nigeria tumeoa huko.

Tukutane EAC kama ndugu wa familia kubwa. Hakuna kujificha ubavuni kwa mwingine.

This time tunataka kuona wanaweka nini mezani kwanza.
Pili, sheria zirekebishwe. Kama Mtanganyika anahitaji kitambulisho cha Uzanzibar ukaazi basi Tanganyika nayo iweke sheria kulinda watu wake katika ajira.

Kuna hili la baraza la mitihani nalo laja. Kwa vile wan abaraza lao la mitihani, wanafunzi wa ZNZ watahiniwe upya kabla ya kujiunga na vyuo vya bara. Hakuna uhakika kama baraza lao linakidhi viwango.
Tunajua la Uganda, Kenya, Burundi n.k Hili ni jipya.

Halafu nafasi za upendeleo ziondolewe ili kutomnyima mtoto wa Kitanganyika haki kwa ubwete wa nafasi za upendeleo.
Division ndio kigezo tena division si za kupeana maana wameanzisha baraza lao kwa kudai wanaonewa.
Kabla ya kuchaguliwa wapitie NECTA kwanza kama hawataki wabaki Tunguu, kuna chuo pia.
 
Nguruvi3, Barubaru, Pasco, Nonda, Mzee Mwanakijiji,

..YES, YES, and YES, wa-Tanganyika na sisi tuanze kudai mapesa toka ZNZ.

..kwasababu tatizo la katiba na particularly muungano, kwanini hii tume ya katiba gharama zake zisibebwe na SMZ??

..Wont it be nice kama Watanganyika wajumbe wa tume ya katiba wakalipwa na serikali ya mapinduzi[SMZ] kila mmoja sh milioni 250 kwa mwaka??
 
Last edited by a moderator:
......Kama hiyo haitoshi wako baadhi ya wanasiasa mbumbumbu wanataka kiwepo kipengele kitakacho wahakikishia waZanzibar wawe na zamu ya kutoa Rais wa JMT.

Huo kweli ni umbumbumbu

.........Yaani watu 1,303,568 wanataka kujenga uhalali wa kutwalawa watu 43,625,435 !.....

....uhalali wa kutawala nchi hii kwa sasa unatokana na mfumo mzima wa uchaguzi wa wagombea kutoka kwenye vyama vyao....haijalishi unatoka bara au visiwani.......huu mfumo ninauunga mkono PLUS kuwepo na wagombea huru/binafsi
 
Ngongo,

Matokeo ya hii sensa yatasadia sana kujadili Muungano. Kwa kuanzia, tuweke wabunge wa viti maalum pembeni;

Tanganyika kuna majimbo 182, kwa maana hiyo kwa population ya 43,625,434 ni kwamba kila mbunge, on average, atakuwa anawakilisha watu 239,700. Zanzibar na population ya 1,303,568, wana majimbo 50. Hivyo, on average, kila mbunge wa Zanzibar atakuwa anawakilisha watu 26,071!

(Mbunge kama Mnyika anawakilisha majimbo 15 huko Zanzibar!)

Gharama zote za bunge anabeba Tanganyika ambaye anapunjwa kwenye 'representation. Lakini bado watu wanalalamika Zanzibar inanyonywa!
 
Nguruvi3, Barubaru, Pasco, Nonda, Mzee Mwanakijiji,

..YES, YES, and YES, wa-Tanganyika na sisi tuanze kudai mapesa toka ZNZ.

..kwasababu tatizo la katiba na particularly muungano, kwanini hii tume ya katiba gharama zake zisibebwe na SMZ??

..Wont it be nice kama Watanganyika wajumbe wa tume ya katiba wakalipwa na serikali ya mapinduzi[SMZ] kila mmoja sh milioni 250 kwa mwaka??
Au basi SMZ ichangie nusu.
Nakumbuka wakati wanadai wajumbe walisema wao ni nchi na kwavile ni pande mbili sawa hakuna kuangalia udogo au population.Tena aliyekuwa anapiga debe BBC alikuwa Ally Salehe ambaye ni mjumbe wa tume.

Hajarudi na kutueleza SMZ ilivyochangia katika tume hiyo.
Hawa ndugu zetu ni wepesi wa kudai nafasi za kazi za ubalozi, ubunge, ukurugenzi na kila kazi kutoka JMT.
Ukishawatajia wanaweka nini mezani, wanaingia mitini, utawasikia wakipiga domo kibanda maiti na mfenesini.

Unajua kwanini siku hizi hawasemi hoja ya kura ya maoni tena!
Wametahadharishwa kuwa kura ya maoni ni kwa upande wa ZNZ hivyo itabidi wabebe gharama.
Lakini kinachowatisha zaidi ni kuhusu maswali ya kura ya maoni. Unataka Muungano? YES / NO.

Hapo ni mtego maana wakisema YES ni kitanzi, hawatakuwa na mamlaka kamili.
Wakisema NO, basi wanachukua mabegi na kurejea kwao.

Nakumbuka SUDAN ilipogawanyika, siku iliyofuata watumishi wote na raia wote wa Sudan kusini waliachishwa kazi na kuambiwa wabeba mizigo yao ya nyumbani warudi kusini. Walitishia kuhusu haki za binadamu wakaambiwa midhali wameshapata nchi yao ni wakati warudi kwao kwasababu hakuna haki ndani ya nchi ya mwenzako.
Huko ndiko tunaelekea ni tarehe tu tunayoisubiri ndio maana kuna nyuzi ya kuwaombea dua wafanikiwe sana.

Wakisema pasu pasu, hatuna shida tutaweka kila wakitacho mezani ikiwa ni pamoja na Trillion 20 za deni la taifa.
Tutaorodhesha kila senti waliochukua au waliodandia katika muungano kama hizi za tume, bilioni 32 ofisi ya makamu wa Rais, mishahara kuanzia masheha katika shehia hadi BLW n.k.

Nashangaa siku hizi hawapigi kelele tena maana kila wakipiga kelele tunapata habari za walipokuwa wamejibanza.
Please Zanzibarians talk! say something! mnatusaidia sana kila mkisema.
 
Nguvu kubwa ya kelele za Muungano ilitokana na 'silence' kuhusu gharama. Wanasiasa wa aina ya Maali Seif, pamoja na kwamba wanajua ukweli, wamekazana kuwaamisha wananchi kuwa Zanzibar inanyonywa. Lakini hasemi chochote kuhusu bajeti ya Polisi, gharama za kuendesha balozi, passport, Ulinzi, au elimu ya juu. Hasemi!

Na kwa bahati (mbaya) Tanganyika walikuwa kimya, lakini kitendo cha kuanza kutukana kuwa Tanganyika ni koloni, kimefanya watu waanze kumwaga mboga na ugali. Hapa tulipofika nyongo zimeshatibuka, anayetaka mazungumzo ya Mkataba anatakiwa atangulize list ya vitu gani vitakuwa kwenye mkataba na nani analipa!

Kuhusu hoja ya pasu kwa pasu, mimi sina tatizo nayo, lakini kuepuka kelele kila upande ulipe watu wake. Mfano kwenye balozi, kila (nchi) imlipie Afisa wake. Mambo ya mbeleko yaishe!
 
Ngongo,

Matokeo ya hii sensa yatasadia sana kujadili Muungano. Kwa kuanzia, tuweke wabunge wa viti maalum pembeni;

Tanganyika kuna majimbo 182, kwa maana hiyo kwa population ya 43,625,434 ni kwamba kila mbunge, on average, atakuwa anawakilisha watu 239,700. Zanzibar na population ya 1,303,568, wana majimbo 50. Hivyo, on average, kila mbunge wa Zanzibar atakuwa anawakilisha watu 26,071!

(Mbunge kama Mnyika anawakilisha majimbo 15 huko Zanzibar!)

Gharama zote za bunge anabeba Tanganyika ambaye anapunjwa kwenye 'representation. Lakini bado watu wanalalamika Zanzibar inanyonywa!
FJM, kuna kitu kingine hatujawahi kukiangalia vema.

Kuna Wabunge 10 kutoka BLW wanaokuja Bungeni Dodoma. Hawa wanamwakilisha nani?

Kuna wabunge wa Zanzibar tayari sasa hawa kutoka BLW wanamwakilisha mzanzibar yupi.

Kwanini basi tusiwe na Wabunge 10 kutoka bara ndani ya BLW? Halafu hao 10 wakivuka bahari wanalipiwa gharama na JMT sio SMZ au BLW. Of course hata kama itakuwa SMZ bado zinatoka bara lakini as a symbol of good gesture tungewaelewa japo, hawafanyi hivyo.

Sikiliza makamu wa Rais anasema kuna nafasi chache za Wazanzb ubalozini.
Hao wabunge 10 tu wanatosha kuziba nafasi za balozi achilia mbali wakurugezi wa halmashauri za bara zisizohusu ZNZ.

This time tutakuwa na mambo yafutayo
1. Mnataka mamlaka kamili, hewala! safari njema visiwani na karibuni sana Tanganyika mkiwa na vitambulisho.

2. Wanataka muungano
a] ZNZ inaweka nini mezani
b] Kwa mambo gani na yenye faida ipi kwa Tanganyika

Kama hakuna cha kuweka mezani, hakuna mamlaka kamili. Period.
Tukutane Kijenge Arusha EAC mkipenda.
 
Kwa upande wangu, naomba kutofautiana na nyinyi!.

Mfumo wa muungano wetu ni mfumo wa ndoa, Tanganyika ndiye mume amemposa Zanzibar ambaye ni mke! na kujenga familia inaitwa Tanzania!.

Japo ni mume ndiye aliyelipa mahari, mume ndiye mwenye kipato, mume ndiye anayemlisha mkewe na kununua mahitaji yote ya nyumba, na kugharimia gharama zote, hizi ni wajibu wa mume, lakini linapokuja suala la haki, mume na mke wana haki sawa ndani ya nyumba hiyo!, na hata ikitokea ndoa ikavunjika, watagawana mali pasu kwa pasu, japo ni mume ndiye aliyenunua kila kitu na mke alikuwa golikipa tuu!.

Ila ukiona mke anapewa kila kitu halafu bado anaanza kufanya visa na vitimbi, ili utoe talaka, ujue keshapata bwana anayemdanga, kama na wewe ukiona umemchoka usisubiri kuchoshwa na visa, mpe talaka yake muachane kwa amani na usalama, lakini kama bado unampenda, hata afanye visa vipi, talaka hutoi na sana sana utamuadabisha tuu!.

Tena mke huyu ni mtukutu wala hakumbuki fadhila!, ile December 1963, aliolewa na Mwarabu!, si unawajua tena Waarabu na ile michezo yao ya kwenda kinyume!, mke yakamshinda, tarehe 12 Januari 1964 akaasi ndoa ya Mwarabu akatoroka kwenye nyumba ya ndoa kwa kusaidiwa na yule Mganda Okello, mke huyo alijileta mwenyewe kwa Dume la Mbegu, Tanganyika, na kuomba ndoa ya mkeka ili kumzua Mume Mwarabu asimrudie maana hata talaka hakupewa!, Tanganyika hakufanya ajizi, akamposa na kumuoa chap chap!, tangu wakati huo kamfanyia mengi tuu sasa leo ndio vinajotokeza hivyo vibwana vinataka kumdanganyia peremende, eti ohh "nitakupendezesha kama Dubai", omba talaka nitakuoa mimi! na ahadi chungu tele!, hivyo hujakoma tuu?!.

Tanzania bado inampenda mke, hata alete chokochoko kupitia vitimbakwiri vya mwarabu, talaka hatoi!, ila mke huyu atashikishwa adabu na kunyoroshwa mpaka atanyooka na kutulia kwenye ndoa!.

P.
 
Kwa upande wangu, naomba kutofautiana na nyinyi!.

Mfumo wa muungano wetu ni mfumo wa ndoa, Tanganyika ndiye mume amemposa Zanzibar ambaye ni mke! na kujenga familia inaitwa Tanzania!.

Japo ni mume ndiye aliyelipa mahari, mume ndiye mwenye kipato, mume ndiye anayemlisha mkewe na kununua mahitaji yote ya nyumba, na kugharimia gharama zote, hizi ni wajibu wa mume, lakini linapokuja suala la haki, mume na mke wana haki sawa ndani ya nyumba hiyo!, na hata ikitokea ndoa ikavunjika, watagawana mali pasu kwa pasu, japo ni mume ndiye aliyenunua kila kitu na mke alikuwa golikipa tuu!.

Ila ukiona mke anapewa kila kitu halafu bado anaanza kufanya visa na vitimbi, ili utoe talaka, ujue keshapata bwana anayemdanga, kama na wewe ukiona umemchoka usisubiri kuchoshwa na visa, mpe talaka yake muachane kwa amani na usalama, lakini kama bado unampenda, hata afanye visa vipi, talaka hutoi na sana sana utamuadabisha tuu!.

Tanzania bado inampenda mke, talaka hatoi, ila mke huyu atashikishwa adabu na atatulia kwenye ndoa!.

P.

Halafu mume mwenyewe mzee na mke bado kijana, mume inabidi a "bow down" kwa kila atalodai mke, vinginevyo ukimuacha mke ataolewa lakini mume kidingi na kisicho na hela za "kutosha" kitapata wapi mke mwingie?
 
Kwa upande wangu, naomba kutofautiana na nyinyi!.

Mfumo wa muungano wetu ni mfumo wa ndoa, Tanganyika ndiye mume amemposa Zanzibar ambaye ni mke! na kujenga familia inaitwa Tanzania!.

Japo ni mume ndiye aliyelipa mahari, mume ndiye mwenye kipato, mume ndiye anayemlisha mkewe na kununua mahitaji yote ya nyumba, na kugharimia gharama zote, hizi ni wajibu wa mume, lakini linapokuja suala la haki, mume na mke wana haki sawa ndani ya nyumba hiyo!, na hata ikitokea ndoa ikavunjika, watagawana mali pasu kwa pasu, japo ni mume ndiye aliyenunua kila kitu na mke alikuwa golikipa tuu!.

Ila ukiona mke anapewa kila kitu halafu bado anaanza kufanya visa na vitimbi, ili utoe talaka, ujue keshapata bwana anayemdanga, kama na wewe ukiona umemchoka usisubiri kuchoshwa na visa, mpe talaka yake muachane kwa amani na usalama, lakini kama bado unampenda, hata afanye visa vipi, talaka hutoi na sana sana utamuadabisha tuu!.

Tanzania bado inampenda mke, talaka hatoi, ila mke huyu atashikishwa adabu na atatulia kwenye ndoa!.

P.

Hii mipasho ndio wanaipenda. Subiri waraka!
 
Pasco huo mfano wako utaandikiwa barua! oh
Barua wanaandikiwa wale wanaoonekana kama mwiba mfano wa Mzee Mwanakijiji, tena mimi ndio kabisa hawanigusi, hapo Mzalendo Net, mimi shemeji yao kwa dada yao mmoja wa wamiliki!.
P.
 
Hivi kwanini hata Jimbo dogo la hapa Marekani linatoa idadi sawa na Jimbo kubwa? Inaonyesha wakati mwingine Nyerere alikuwa ahead of time.
 
hivi mnawawazia hawa wazanzibar kama watu?? subirin mtajionea wenyewe.
 
PASCO.. Akija Jussa hapa hapatoshi...yy anataka ndoa ya mkataba na mme awe na nyumba yake na mke awe na nyumba yake (i mean maamuzi) sasa huyu mme amekuwa kigeugeu maana ameposa wake wengine (east africa community) kiasi kwamba bmkubwa anaona wivu maana naye anamendewa na wengine lakin masharti ya ndoa magumu.. Mil 1.3 mnataka equal rights na mil 43?...ndoa na ivunjike tu
 
  • KATIBA hii IMETUNGWA NA BUNGE MAALUM LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia na ujamaa.
  • Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa.
  • Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano... Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.
  • Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano...Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.
  • Mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatahusu utekelezaji na hifadhi ya Katiba hii na pia mambo mengineyo yote ambayo Bunge lina mamlaka ya kuyatungia sheria.
  • Kila Rais mteule na kila mtu atakayeshikilia kiti cha Rais, kabla ya kushika madaraka ya Rais, ataapa mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, kiapo cha uaminifu na kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
Wanajamvi, hizo hapo juu ni nukuu chache tu ndani ya kinachodaiwa ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...! Huu ni ubabaishaji...someone somewhere must be joking or we are being played for fools! Na usanii unazidi kuendelea hapa chini...
  • Kutakuwa na Serikali ya Zanzibar itakayojulikana kama Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo itakuwa na mamlaka katika Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo mambo ya Muungano kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
  • Kutakuwa na Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambaye ndiye atakuwa Rais wa Zanzibar na Mkuu wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na vile vile Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar.
  • Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Jaji Mkuu wa Zanzibar kiapo cha kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano...

Pamoja na mapungufu yaliyomo kuna ndani ya hiyo katiba, kitu kimoja kiko wazi...hakuna popote ndani ya hii katiba anapotambuliwa Rais wa Zanzibar kama Rais wa nchi...! inashangaza nchi kuendeshwa bila hata kufuata hiyo katiba yenyewe...huyo anayeitwa Rais visiwani kwa kweli ni mkuu wa sehemu ndogo tu ya nchi inayojulikana kama Tanzania Zanzibar, yenye idadi ya watu wasiofikia hata asilimia 3% ya Watanzania wote!

The naked truth...Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Mrisho Kikwete anavunja katiba aliyoapa kuilinda na hivo kupelekea Rais wa Tanzania Zanzibar naye ku follow suit. Swali ninalojiuliza ni hili, je tunao wawakilishi bungeni? Where are they?
 
Back
Top Bottom