Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Mkuu Mag3, wawakilishi wapo kwa bahati mbaya hakuna mwenye kufikiria nchi kwanza, kila mmoja anafikiria jinsi ya kurudi bungeni next time.Wanajamvi, hizo hapo juu ni nukuu chache tu ndani ya kinachodaiwa ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...! Huu ni ubabaishaji...someone somewhere must be joking or we are being played for fools! Na usanii unazidi kuendelea hapa chini...
Pamoja na mapungufu yaliyomo kuna ndani ya hiyo katiba, kitu kimoja kiko wazi...hakuna popote ndani ya hii katiba anapotambuliwa Rais wa Zanzibar kama Rais wa nchi...! inashangaza nchi kuendeshwa bila hata kufuata hiyo katiba yenyewe...huyo anayeitwa Rais visiwani kwa kweli ni mkuu wa sehemu ndogo tu ya nchi inayojulikana kama Tanzania Zanzibar, yenye idadi ya watu wasiofikia hata asilimia 3% ya Watanzania wote!
The naked truth...Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Mrisho Kikwete anavunja katiba aliyoapa kuilinda na hivo kupelekea Rais wa Tanzania Zanzibar naye ku follow suit. Swali ninalojiuliza ni hili, je tunao wawakilishi bungeni? Where are they?
Pili, hizi siasa za uchama nazo zimezidi na kudumaza nchi. Mathalani, haiwezekani mbunge wa CCM kusimama na kuhoji au kuunga mkono hoja inayokinzana na sera za chama chake.
Wenzetu wengine duniani mbunge anakuwa mwakilishi wa watu kwanza kabla ya chama.
Pengine hili nalo linaongeza uzito wa kuwa na wagombea binafsi watakaokuwa na mawazo huru bila kufungwa pingu za vyama.
Umekumbusha kitu muhimu sana katika katiba. Baada ya tetesi za mafuta SMZ imekimbilia BLW na kurekebisha katiba yake inayoeleza Zanzibar na eneo lake ikiwa ni mkakati wa kulinda kile kilichosemwa ni mafuta.
Katika kufanya hivyo walijikuta wanakiuka katiba ya JMT kwakiwango cha hali ya juu sana.
Ndio maana tunasema hivi, ili kuondoa sintofahamu na maruwe ruwe haya ZNZ iliyo na uwezo wa kubadilisha mambo mengi bila kuulizwa ina uwezo wa kuamua hatima yake ndani ya muungano bila kutegemea Tanganyika.