Uwingi wa neno hili

Uwingi wa neno hili

rununu

Member
Joined
Jun 26, 2011
Posts
57
Reaction score
2
Tafadhali naomba mnisaidie UJUMBE (message) maana nimekuwa nikisikia baadhi ya watangazaji wakisema "Naanza kusoma JUMBE mlizotuma" je ni sahihi?
 
Jumbe: (Majumbe) noun Chief, village elder, Headman.
Ujumbe: Ujumbe noun message, petition, Meaning, Task, Delegation, Deputation, Mission,

Zamani babu zetu, walikuwa wakitaka kutuma taarifa, waliwatumia hawa watu walio waita Wajumbe (Mpeleka taarifa au habari) Vilevile neno Jumbe kama hapo juu ni kiongozi wa eneo kama vile mtaa. Vile vile linatumika kama wawakilishi kama wabunge ni wajumbe wetu kwa serikali, yaani ndio wenye kutupelekea malalamiko na mahitaji yetu
.

Sasa kile wanacho kiwakilisha au kukipeleka ndio Ujumbe... Huwe mwingi au mchache, maana neno Ujumbe hauna wingi, si kama Kiingereza.

Mf:
1. ujumbe ulioletwa na barua hii ni...
2. ule ujumbe uliyonituma Morogoro haukufaulu
3. ule ujumbe ulioutuma Morogoro haukufaulu
 
Nashukuru sana ndugu yangu maana huwa napata shida sana hasa kwa kuwa baadhi ya watangazaji wamekuwa wanatumia jumbe badala ya ujumbe. kuna haja ya kuangalia matumizi sahihi ya kiswahili katika vyombo vya habari.
 
Yani X-Paster akishajibu mimi nakasirika..unajibu kila kitu!!!
 
Ah ah ah ah ah ah..... Mentor, yaani nakudai togwa langu, maana umesababisha nimecheka mpaka nimepaliwa na kutema kile nilichokwisha anza kukitia mdomoni.

Mkuu, si unajuwa kuwa ndani ya JF kuna watu wa level tofauti tofauti, sasa inabidi wakati tunajibu tuwe waangalifu, ili atleast tueleweke na kila rika.

Najuwa umenielewa, I like u man.
 
Back
Top Bottom