GE2025 UWT yasema uchaguzi wa Oktoba 29, 2025 utakuwa mwepesi kwa CCM, yaeleza sababu

GE2025 UWT yasema uchaguzi wa Oktoba 29, 2025 utakuwa mwepesi kwa CCM, yaeleza sababu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Zainab Khamis Shomari, amesema kuwa uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu utakuwa mwepesi kwa chama hicho kutokana na maendeleo makubwa yaliyoletwa na Serikali.

Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Zainab Khamis Sh.jpg
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM katika Jimbo la Mtambwe, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Zainab amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuendelea kukiamini chama hicho, akieleza kuwa maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali yamekuwa yakithibitisha uongozi bora wa CCM kwa wananchi.

Aidha, amewahimiza wananchi wa Jimbo la Mtambwe kuchagua viongozi wa CCM kwenye nafasi zote.
 
Back
Top Bottom