MulegiJr
Senior Member
- Sep 5, 2018
- 125
- 88
Sitamani kuingia ndani Sana katika maana ya maneno matatu hapo Juu, #Uzalendo ni dhana ya mtu kusimama kwa ajili ya Taifa lake na si kwa maslahi ya kikundi au yeye mwenyewe.
#Itikadi ya vyama vya siasa ni Mlengo wa uendeshaji na usimamizi wa Mwenendo mzima wa utawala, imani itegenezayo mifumo ya kiutawala na mazingira ya yategenezayo maisha ya watu ndani ya chama na Taifa kwa ujumla, Itikadi za Mlengo wa kushoto, au kulia.
#Usaliti Dhana ya kukiuka makubaliano, utamaduni na Malengo yenu kitaifa, kikundi au kati ya mtu na mtu.
DHANA POTOFU, kuna dhana POTOFU Kati ya Uzalendo, usaliti na Itikadi za Vyama, Watu waliowengi hata hapa Javini wanaupofu Juu ya uhalisia na maana halisi ya nini kinasimama wapi na kipi kina simama kusaidia kigine!!
#Uzalendo hauna Itikadi za chama bali Utaifa na Malengo ya Taifa bila kujali nani kasimama au kakaa, bali kasimama kwa ajili ya nini? Taifa?, Kikundi au yeye kama yeye?
Hapa ndo kumekuwa na dhana POTOFU ya kuamini CHAMA A NI WAZALENDO KULIKO CHAMA B, mtu akiachana na Itikadi Fulani(Chama) anaonekana Msaliti anaonekana siyo Mzalendo maana ameenda kuhudumu Itikadi tofauti na yao😄😄😄, actually kuna uhitaji wa watu kuelewa #Uzalendo ni Nafisi ya mtu na siyo Itikadi!
Kuna mtu yupo chama A lakini anafanya Usaliti mchana kweupe lakini anaendelea kulindwa kwa sababu kibao zisizo na Mashiko.
KUONDOA DHANA YA USALITI KWA ITIKADI ZA VYAMA.
Ni Muda sasa watu kuamini mtu kutoka chama A kwenda B ni suala la utashi na siyo Usaliti au kutokuwa na Uzalendo KWA Taifa lake, nchi yetu imepita katika Hamahama ya viongozi wadamizi wa Vyama, lakini leo tunaona wanalitendea Taifa maajabu ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. ITIKADI siyo Uzalendo au Usaliti.
Ni wakati sasa tutegeneze WAZALENDO, na uzalendo utegenezwe kupitia watu na siyo Itikadi za Vyama( Chama Siyo Mama yangu au Baba yangu) kuachana na chama iko liwe jambo la kawaida kwa kila mtanzania bali apimwe Uzalendo wake ndo asemwe na kuibwa KWA ubaya pasi upendeleo.
Kaondoka, Lowassa karudi sababu za Usaliti, kaondoka Mtatiro leo anafanya kazi nzuri, kaondoka Patrobus Katambi anafanya vizuri sana!
Ameondoka Anna Mghwira(R.I.P) alifanya vizuri sana wote hawa leo nawashukuru kwa sababu wamefanya Mambo makubwa na ya kizalendo.
Uzalendo na ufahari wa Itikadi.
Naomba kuhitimisha kuheshimu Njia za Kutafuta nafasi za kuitumikia Taifa usifahamike kama Usaliti, maana Itikadi haina Picha halisi ya Uzalendo wa Kweli.