Uzalendo ndio huu, Dar-New York kwa B787-8 gharama ya mafuta ni TZS 267M

Ningekuwa mshauri wa mama,ningemshauri atue airport kimya kimya na protocol ya kawaida TU Kama alivyoondoka.Hii ya kupokelewa kwa mbwembwe Kama wanavyotaka wapambe na wanaojikomba kupata vyeo ndo itamharibia mama badala ya kumpandisha chat.Itaonekana kwamba Kuna campaign ya kimyakimya ya 2025 ambayo ambayo imeanza,wakati hiki Ni kipindi Cha kuifanyia kazi ilani ya uchaguzi ya CCM Iliyotangazwa wakati wa campaign ya uchaguzi iliyopita ambao Ni mwaka Jana TU 2020.Wapambe mngesubiri kidogo mpaka angalao 2024 October(mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wa 2025).Ukiwa ataruhusu design hii ya campaign kwa Sasa,kazi na ahadi mlizotuahidi Sisi wananchi zitafanyikaje Sasa !
 
Dah....hebu acha ujinga....unajua chumba Cha watu mashuhuri pale Piere Guest house na kiasi gani kwa siku? 😂😂😂🤭
 
Vipi kama angeenda na Gulf Stream,hesabu ingekaaje?
 
Mkuu Jabali la Siasa , kwanza asante kwa bandiko hili, na pili asante kwa kutukokotolea gharama ya mafuta kulirusha lile li Dreamliner kwenda Marekani.
Mimi ni miongoni mwa tunaoshauri rais wetu akisafiri, maandam sasa tunazo hizo ndege, rais wetu atumie ndege zetu.

Hili pia nimelisema kwenye uzi huu

Kwenye andiko hilo, hiyo element ya gharama nimeisema.

Kama Tanzania, tumedhamiria kuukuza utalii wetu na kuutangaza kimataifa, hatuwezi kukwepa gharama!. Kama hiyo gharama wewe unaona ni fedha nyingi sana, nenda katafute gharama ya kuandaa Royal Tour kuutangaza utalii wa Tanzania kimataifa. Kama tumeweza ku justify kutumia gharama hizo kwenye Royal Tour, tutashindwaje kulirusha li dreamliner letu kwenda kututangazoa utalii wetu na ATC kuanzisha direct flights za Marekani?.

Jee unajua gharama za kurusha Tangazo la TV la 60 sec kwa mara moja tuu kwenye CNN?. Ukizisikia ndipo utakubaliana na mimi, kutangaza kitu chochote kimataifa ni gharama, kama Tanzania Tumedhamiria kwa dhati, kuutangaza utalii wetu kimataifa, hatuwezi kukwepa gharama!.
Chief Hangaya atakapokwenda Marekani kuizindua filamu yake ya Royal Tour, aende na Dreamliner, Watanzania wenye uwezo wa kuchangia gharama tupo, na tutamsindikiza Mama.

P
 
Mh!? Cognitive function loading, . Ni vile tu alie andika anaheshimika hapa janvini.
 

Mkuu kumekuwa na maombi ya mrejesho wa dege alilotumia pasipo na majibu.

Kwani tabia za kulisha watu matango pori mliziachia awamu ile?
 

Kwa maelezo haya yule wa jalalani na wote waliohusika:



warejeshe mafuta yetu waliyoendea kutalii Antananarivo!
 
UZALENDO NI VITENDO SIO MANENO,

HUYU MAMA NI KAMA NYERERE TU,

ANAJUA UCHUMI,

ANAJUA LUGHA,

ANAJUA DIPLOMASIA,

WALE MLIOKUWA MNAMPONGEZA YULE RAIS WA ZAMBIA NYIE SIO WAZALENDO KABISA,
Kumekucha Makunduchi, ingizo jipya, Watoto wa teuzi.
 



Mkuu,
Hesabu zako hazipo sahii. Kutoka Dar es salaam airport paka New York airport kwa kutumia Emirates ni Tshs 22,000,000 kwa First class, Tshs 9,800,000 kwa Business class na Tshs 4,200,000 kwa Economy class. Unaweza kuangalia hizi rate kwenye website ya emirates.

kwasabu walienda kwenye shughuli za serikali,bila shaka walichukuwa first class na Business class.

Kama umesema walienda watu 50, watu 15 nitakadiria walikuwa first class na watu 35 walikuwa business class
First class 15 x 22,000,000 = Tshs 330M
Business class 35 x 9,800,000=Tshs 443M

Gharama ya kwenda itakuwa ni Tshs 773M
Naweza kusema safari yote imechukuwa zaidi ya Tshs 1 Billion. Hii ninamaanisha pamoja na Posho na gharama za kujikimu.
 
Emirates amekodi au kapanda na abiria wengine?
 
Midege ilinunuliwa ili ikafanye nini kama haiwezi kuruka kwenda kwa wenzetu? Atapanda nani sasa kama Hangaya anaogopa? Mmenunua ndege ili ziende chato na kurudi sio + kwenda mikoa mingine ya Tanzania bara??
 
Kwani huko New York kaenda kufanya nini ambacho alishimdwa kufanywa kwa video conferencing? Tuanzie hapo kwanza
 

Acha yapande tu mama si anaupiga mwingi
 
speculative thinking..btw kila mtu siku hizi seems to be 'shujaa'!
 
UMECHANGANUA VIZURI SANA. NIKUONGEZEE KIDOGO KWAMBA HATA HAO WATU HAMSINI WENGI WAO NI WAFANYABIASHARA WALIOGHARAMIA SAFARI YAO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…