Uzalendo: Pongezi kwa Jeshi la Magereza na Wizara ya Mambo ya Ndani

Uzalendo: Pongezi kwa Jeshi la Magereza na Wizara ya Mambo ya Ndani

Bishweko

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
4,985
Reaction score
3,493
Wadau na wazalendo wa Taifa ili bila shaka tunajua maana ya Uzalendo. Naomba kwa machache tu mimi kama mzalendo mmojawapo nitumie fursa hii adhimu na adimu kulipongeza jeshi letu la Magereza, wafungwa wetu pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani.

Kulipongeza jeshi la Magereza na Wafungwa wetu sina maana kua majeshi mengine hayafanyi mambo ya kizalendo. Ukweli lazima usemwe katika awamu hii Jeshi la Magereza na Wafungwa wetu kushiriki kazi za kisiasa kwa kufanya maandalizi ya mapambo mfano ya kufunga bendera kumeonyesha uzalendo ulio tukuka kabisa.

Sina uhakika kama kuna jeshi lolote liliwai kufanya hivi kabisa.Pongezi hizi ziendane pia na kuyashauri majeshi mengine kufanya zaidi ya apa angalau ata kuvaa mavazi ya chama tawala kabisa.

Mwisho kuna watanzania walitunga sheria eti chama cha siasa kisishirikishe vyombo vya dola na majeshi katika kufanya kazi zake za kisiasa watu hao wasisikilizwe kabisa na wapuuzwe tu maana sheria hiyo inakihuka misingi ya haki,usawa,zamani na umoja.
HONGERENI JESHI LA MAGEREZA NA WAFUNGWA WETU
 
Sasa hivi wamepewa tenda ya kufanya usafi mji wa Musoma. Wanafagia barabarani na kuzoa taka.
 
Sasa hivi wamepewa tenda ya kufanya usafi mji wa Musoma. Wanafagia barabarani na kuzoa taka.
Hizo ni kawaida sana,kushiriki siasa za chama tawala ni uzalendo uliotukuka
 
Serious??....mɓona ƙa masihara....!!!😎😎
 
watapongezwaje bana wakati wanavunja sheria? ila mi nimekuelewa kua hizi ni pongezi za kinafiki kiaina
 
CCM haina watu wanaipenda kwa dhati kuthubuti kujitolea kwa hiari bila malipo kazi za chama hicho!
Kwa ujinga na ulevi wa madaraka na kupungukiwa akili, ndiyo maana wanatumia wafungwa wasio na sauti juu ya maisha yao!
Pia kwa kuwa polisi nao wametiwa uoga kwa ahadi ya vyeo, wanafanya ujinga wanaufanya!
Mkakati madhubuti wa upinzani utakaodhibiti mabavu ya dola kuibeba CCM, October hakika kitaanguka! Hakina watu!
 
Sherehe zijazo za Uhuru wale wote wanapewa mdhamana wa rais
 
Back
Top Bottom