Tafsiri rahisi ya uzalendo ni kuwa na mapenzi na nchi yako, mzalendo ni yule mwenye mapenzi na nchi yake, yaani mfia nchi, aliye tayari kutetea nchi yake au kufanya lolote kwa ajili ya nchi yake. Kuna tofauti kati ya nchi, serikali na taifa, hao unaowasema wewe si wazalendo kwasababu wana mapenzi na serikali, lakini hawana mapenzi na nchi, wana mapenzi na kiongozi wa nchi au kiongozi wa chama lakini si nchi. Serikali ni kikundi cha watu watawala walipo madarakani kwa muda fulani, wanaweza kuwepo madarakani kwa muda na kisha huondoka(Kwa hiari au lazima) lakini nchi itaendelea kuwepo, hivyo tunapaswa tuwe na uzalendo (mapenzi kwa nchi) na si kwa serikali, Rais au chama.
Wenye mapenzi na serikali, au Kiongozi fulani, au mapenzi na chama fulani hufanya hivyo kwa masilahi yao binafsi na si kwa masilahi ya nchi.
Mifano ya watu uliowataja hapo hawakuwa na uzalendo na nchi yao bali walikuwa vibaraka wa kiongozi fulani au chama fulani au kundi fulani - kwa maslahi yao binafsi na si kwa masilahi ya nchi.