Uzalendo wetu uko wapi?

Uzalendo wetu uko wapi?

FIKRA HAI

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2013
Posts
231
Reaction score
79
Uzalendo ni hali ya mtu kuwa na uchungu hasa juu ya nchi naJamii kwa ujumla. Shana hii ni Pana na pengine ilipaswa kufundishwa kwenye shule zetu kwa ngazi zote.

Msingi wa hoja yangu ni dhidi ya ubinafsi mkubwa uliojaa kwenye jamii zetu ikiwa ni pamoja na wale wote wenye fursa ya kuhubiri Uzalendo kukosa Uzalendo huo.

Kwa asili Jambo hili limekuwa gumu zaidi hasa kwa jamii za Kiafrica kwa Shana tu kuendekeza umimi, ukabila na pengine hata udini.
Hatua hii hupelekea migogoro mingi ndani ya nchi na hupelekea nchi nyingi za Magharibi kutulaghai na kutupora rasilimali zetu.

Viongozi wengi wa Kiafrica wanapopata nafasi ya kuwa kiongozi anawaza namna ya kuwapora wananchi wenzake Kodi zao badala ya kuwa na uchungu na kuwatumikia kwa kukutatua changamoto hizo.

Mwisho wa tamaa hizi ni kujilimbikizia Mali ambazo hazina maana yoyote, kumbe angeweza kuwa mzalendo na kujitoa hata kwa ajili ya wenzake.

Tunapoona kila Rais anayeingia madarakani anaanza kuwatafuta marafiki zake na kusuka upya utawa ni kupoteza Uzalendo na misingi ya kulisukuma gurudumu la Maendeleo ambalo tumekuwa tukiliimba.

Hivi Sasa Mambo mengi Sanaa hasa ya maendeleo yanaenda taratibu Sana kwa misingi ya kwamba SERIKALI iliyopo Madarakani sio ya Kibabe Kama ya Mwendazake. Ujenzi wa barabara unasuasua changamoto ni nyingi mno.

Je ni kweli hakuna haja kuongeza ukali angalau misingi iliyowekwa mwanzo ya maendeleo yakaenziwa?
 
Unataka tukalikaripie kaburi lake kwa kukausha hazina ya Taifa iliyotumika kuanzisha na kujenga miradi isiyo na tija kama uwanja wa ndege wa kimataifa wa Chato, daraja la la Coco Beach nk!
 
Hakuna Mtanzania hata mmoja ambaye yupo kwa ajili ya mtu mwingine au mwenzake wote hasa Wanasiasa wapo kwa ajili ya matumbo yao tuu.

Ndio maana hakuna usawa katika utumishi wa Umma kuna grades za kufa mtu halafu wanataka kodi tulipe sawa.

Inawezekana vipi watu wenye degree mmoja analipwa 5M ( kisa ni kiongozi wa kisiasa ) na mwingine 500K ( mtumishi wa wanyonge au maskini )...???
 
Uzalendo ni wito wa kijeshi tuu. uzalendo wa aina nyingine yoyote ile ni upuuzi fulani hivi.
 
Dhana ya uzalendo ni pana sana. Ni kweli inaanzia katika kuipenda nchi yako na kuwa tayari kwa lolote kwa ajili ya ustawi na maendeleo yake. Sasa unapokosea ni pale unaponasibisha uzalendo na alichofanya hayati pekee.

Wewe unahesabu uzalendo kama maendeleo ya vitu pekee lakini huzingatii kuwa ustawi wa wananchi nao ni moja ya matokeo ya uzalendo. Unapojenga Barbara elfu moja wakati wananchi hawana furaha na amani unajenga kimoja huku ukibomoa kingine. Huwezi kuitwa mzalendo hapo. Unakuwa mbinafsi tu kama wabinafsi wengine tu.

Kwa Sasa watu wengi Wana furaha na amani hata kama hawana Barbara kwa sababu Wana tumaini kuwa na nafasi ya kuchangia kwa mawazo kwenye maendeleo ya vitu vya nchi bila kuhofia uhai wao
 
Back
Top Bottom