Uzalishaji na biashara ya mchele EA

simplemind

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2009
Posts
16,418
Reaction score
9,209
According to USDA uzalishaji wa mpunga(mchele) EA 2012 ni kama ifatwavyo(Tonnes)

Kenya 120,000 (79,000)
Tanzania 1500,000(990,000)
Uganda 233,000(151,000)
Rwanda 85,000(55,000)

Kwa mujibu wa ripoti hii Kenya inaagiza/import zaidi ya tani 300,000 za mchele kutoka Asia. Tanzania ipo njiani kujitosheleza katika uzalishaji wa mpunga. Siyo siri mchele wa TZ upo in demand kutokana na ladha /quality nzuri. Swali kwa wazoefu wa biashara ya mchele ni nini kikwazo/vikwazo biashara ya mchele kati ya nchi za Afrika Mashariki.
 
Ngoja Tusubiri Wajuzi Watudadavulie Mambo!!
 
kikwazo cha kilimo cha mchele ni kuendelea kutegemea kilimo cha mvua, badala ya kuja na mbinu mpya za kilimo cha umwagiliaji.
 
Ndo maana wanalilia kuja huku kumbe wakenya wanaumendea mchele wetu
 
Mzee unaulizia kikwazo wakati kipo wazi pakia lori lako la mchele uone kama kuna mpaka utakoruhusiwa kuvuka nao,Ni marufuku kusafirisha chakula nje ya nchi hiyo ruhusa anayo rizmoko & co tu
 
kikwazo cha kilimo cha mchele ni kuendelea kutegemea kilimo cha mvua, badala ya kuja na mbinu mpya za kilimo cha umwagiliaji.

umwagiliaji wa maji kidogo.Sio mimaji kibao tuliyoozea ktk maeneo ya mpunga.
 
muulize atawezaje saidia CUF isijekuwa chama cha kigaidi?
 
Sabayi umenena kweli. Tunaambiwa kilimo kwanza, wakulima wakipata mazao na serikali kutosheleza maghala kwa kununua bei rahisi wanazuia wakulima kuuza mazao nje, sababu kutakuwa na njaa. Kuna wakati nafaka zinaoza nje ya maghala ya serikali, kuwe na free market na hakuna mkulima ambaye atalima na kuuza mazao yake yote bila kuacha akiba, kuwe na uhuru wa kuuza mazao masoko ya nje pale tu serikali itakapojaza maghala yake ya chakula cha akiba.
 
we umesahau serikali ya chichiemu imekataza kuuza chakula nje ya nchi.
sukari, mchele, mahindi. wamekataza
kwanza kuyatoa shambani mpaka Dar au Arusha unamaliza hela yote kulipa hongo kwa traffic na Mizani
tuombe Mwenyezi Mungu treni irudi
 
Shida ya nchi yetu ni kuwa na wasomi wengi wasio na elimu na nchi kuongozwa na siasa badala ya taaluma.

Kenya wana njaa kwa miaka si chini ya 7 sasa na hii inatokana na ukame na ardhi finyu isiyokidhi uzalishaji wa chakula. Naamini hii ingeweza kuwa nafasi kwa Tanzania kunufaika na soko la Kenya kwa muda wote huu, lkn tatizo limelala wapi:

Sera mbovu: Imekuwa sasa kwamba mkulima wa Tanzania ni mtumwa wa Urban Dwellers. Mkulima alime mazao yake lkn anapotaka kuyauza basi apangiwe amuuzie nani, kisa akiuza nchi itakumbwa na njaa. Je hilo ni jukumu la serikali au mkulima?

Suluhisho:
(kwa seriali) nguvukazi kubwa sana inapotea kuwaweka wafungwa magerezani bila kuwapa kazi za kuzalisha mali. Inashangaza kuona miaka ya nyuma tulinunua maharage na mchele wa Magereza pale Keko lkn leo wakati dunia imepiga hatua kwenye teknolojia, wafungwa hawawezi kulima chakula. Kwanza ni mateso kwao na pia wanakosa nafasi ya kujifunza. Fikiria wale wahuni waliochoma makanisa juzi kama wangepatiwa elimu ya kilimo wakiwa magerezani, wakirudi unategemea hawatabadilika? Lkn badala yake wanawekwa tu magerezani na wakitoka huko wanakuwa manunda zaidi.

Nguvu kazi nyingine ni UJUZI walionao makamanda wetu wa JKT. Kwa serikali bunifu na yenye utashi lazima mikakati iwepo. Chukua vijana 200 (wapo wengi mijini), JKT 10 (nidhamu) medical staff 3 (afya), wataalam wa Kilimo 5 (wanaweza pia kutoka JKT) Matrekta 5 na ekari 1000. Tengeneza kambi ya mfano, lima mahindi kwa nguvu kazi hiyo kwa miaka 3 mpango ukiwa kwamba baada ya miaka 3 mapato ya kambi yagawanywe kwa vijana hao (baada ya kutoa management and investment cost) na waachie kambi kupisha vijana wengine kwani wao tayari watakuwa wana ujuzi na mitaji ya kwenda kufungua mashamba yao na kujitegemea.

Ikiwa kambi mfano itafanikiwa, basi inakuwa nafasi nzuri ya kufungua kambi zingine bora zaidi na kusaidia uchumi wa nchi kwa kiwango kikubwa ikiwa ni pamoja na ajira kwa vijana. Kwa utaalam uliopo sasa ekari moja yaweza kuzalisha gunia 25 -30 za mahindi kwa hiyo shamba darasa la ekari 1000 x 25(gunia) = 25,000 /10 = tani 2,500.

Sasa iangalie ile ardhi rutuba iliyopo toka mpaka wa Sirari hadi Tarime halafu jiulize kwa nini malori mengi yamekamatwa na chakula hapo mpakani!

Serikali ione aibu kuwapora wakulima haki yao ya kupata faida nono na kuwa na maisha bora. Wafungwa wafanye uzalishaji wa maana, JKT watumike kuinua uchumi na nidhamu ya nchi, na vijana wapatiwe ajira mashambani. Kama Kenye imetuzidi viwanda na kutugeuza soko la Blue Band, Colgate, Omo, Kiwi n.k, kwa nini na sisi tusiigeuze soko la Mchele, Mahindi na Maharage?
 
kikwazo cha kilimo cha mchele ni kuendelea kutegemea kilimo cha mvua, badala ya kuja na mbinu mpya za kilimo cha umwagiliaji.

Kikwazo kikuba kabisa cha kilimo Tanzania ni wale wasiolima kuwapangia waliolima bei na mahali pa kuuza walicholima.
 
Kuhusu agri production Tanzania bila shaka has a comparative advantage over the rest of EA countries. Mfano kilimo cha mpunga tunayo mabonde na mito ya kutosha pia modern rice mills morogoro mjini( former nmc) , Wami Dakawa,shinyanga,mwanza, na mbeya pia. Tatizo nahisi sera mbovu ya kilimo and lack of desicive leadership to take advantage of God given opportunity.
 
mkuu nimelima pamba bei ikiwa sh 1200,leo naenda sokoni naambiwa sh 600 kwa kilo!jee nitarudi tena shambani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…