Shida ya nchi yetu ni kuwa na wasomi wengi wasio na elimu na nchi kuongozwa na siasa badala ya taaluma.
Kenya wana njaa kwa miaka si chini ya 7 sasa na hii inatokana na ukame na ardhi finyu isiyokidhi uzalishaji wa chakula. Naamini hii ingeweza kuwa nafasi kwa Tanzania kunufaika na soko la Kenya kwa muda wote huu, lkn tatizo limelala wapi:
Sera mbovu: Imekuwa sasa kwamba mkulima wa Tanzania ni mtumwa wa Urban Dwellers. Mkulima alime mazao yake lkn anapotaka kuyauza basi apangiwe amuuzie nani, kisa akiuza nchi itakumbwa na njaa. Je hilo ni jukumu la serikali au mkulima?
Suluhisho: (kwa seriali) nguvukazi kubwa sana inapotea kuwaweka wafungwa magerezani bila kuwapa kazi za kuzalisha mali. Inashangaza kuona miaka ya nyuma tulinunua maharage na mchele wa Magereza pale Keko lkn leo wakati dunia imepiga hatua kwenye teknolojia, wafungwa hawawezi kulima chakula. Kwanza ni mateso kwao na pia wanakosa nafasi ya kujifunza. Fikiria wale wahuni waliochoma makanisa juzi kama wangepatiwa elimu ya kilimo wakiwa magerezani, wakirudi unategemea hawatabadilika? Lkn badala yake wanawekwa tu magerezani na wakitoka huko wanakuwa manunda zaidi.
Nguvu kazi nyingine ni UJUZI walionao makamanda wetu wa JKT. Kwa serikali bunifu na yenye utashi lazima mikakati iwepo. Chukua vijana 200 (wapo wengi mijini), JKT 10 (nidhamu) medical staff 3 (afya), wataalam wa Kilimo 5 (wanaweza pia kutoka JKT) Matrekta 5 na ekari 1000. Tengeneza kambi ya mfano, lima mahindi kwa nguvu kazi hiyo kwa miaka 3 mpango ukiwa kwamba baada ya miaka 3 mapato ya kambi yagawanywe kwa vijana hao (baada ya kutoa management and investment cost) na waachie kambi kupisha vijana wengine kwani wao tayari watakuwa wana ujuzi na mitaji ya kwenda kufungua mashamba yao na kujitegemea.
Ikiwa kambi mfano itafanikiwa, basi inakuwa nafasi nzuri ya kufungua kambi zingine bora zaidi na kusaidia uchumi wa nchi kwa kiwango kikubwa ikiwa ni pamoja na ajira kwa vijana. Kwa utaalam uliopo sasa ekari moja yaweza kuzalisha gunia 25 -30 za mahindi kwa hiyo shamba darasa la ekari 1000 x 25(gunia) = 25,000 /10 = tani 2,500.
Sasa iangalie ile ardhi rutuba iliyopo toka mpaka wa Sirari hadi Tarime halafu jiulize kwa nini malori mengi yamekamatwa na chakula hapo mpakani!
Serikali ione aibu kuwapora wakulima haki yao ya kupata faida nono na kuwa na maisha bora. Wafungwa wafanye uzalishaji wa maana, JKT watumike kuinua uchumi na nidhamu ya nchi, na vijana wapatiwe ajira mashambani. Kama Kenye imetuzidi viwanda na kutugeuza soko la Blue Band, Colgate, Omo, Kiwi n.k, kwa nini na sisi tusiigeuze soko la Mchele, Mahindi na Maharage?