Kwamashu pamechangamka. Kifupi manzunza alinogewa na penzi la zulu hadi ndoa yake ikavunjika. Mxolisi karudia maisha ya uhalifu kajiunga na nkunzi. Qabanga anapanga mpango wa kumuua nkunzi lakini haukufanikiwa. Sma na thobile wanakuwa na msuguano mkali kugombania kuongoza kwaya kwa ajili ya mashindano lakini mwishoni wanapatana. Mbatha anataka kumpindua mletshe lakini anafeli. Sma na khumbulani wanapanga kufunga ndoa karibuni. Kanisa linaandaa tamasha kubwa la kukomesha uhalifu kwamashu na vilevile kufanya harambee. Manzunza naye mambo ni magumu anaamua kurudi kwa mumewe kuomba msamaha. Nkunzi kaalikwa kama msemaji na mhalifu aliyestaafu, hapo ndio nkunzi ansema sasa kwamashu watanitambua, kawaamru vijana wake kuiba magari yoote yatakayokuwepo kanisani soku ya tamasha na kupora pesa zitakazokusanywa. Kukatokea kurushiana risasi kati ya polisi na wezi. Watu kadhaa wanajeruhiwa manzunza anafariki. Sma anapelekwa hospitali lakini naye anafariki. Mxolisi na zweli wanachanganyikiwa wameshiriki kwenye uhalifu uliowauwa wapendwa wao.
Ndipo ilipofika kwa sasa.